ATOA USHUHUDA JINSI URAIBU WA KUVUTA SIGARA NA POMBE KALI ULIVYO SABABISHA RAFIKI YAKE KUPATA SARATANI YA MAPAFU ( Je Kuna Tiba ya kumsaidia mraibu wa sigara na pombe kuacha kutumia tena vitu hivyo?)
Rafiki yangu amebakiza
mwezi mmoja kuishi kutokana na uraibu wa sigara na pombe kali iliyosababisha
saratani ya mapafu
Habar za muda huu wana Jf.
Usiku huu nimepokea taarifa zilizonishtua sana
kutoka Kwa rafiki yangu (Mdogo wangu) kuhusu Afya yake.
Alichoniambia mpaka sasa sijaelewa kinawezaje
kumuathiri haraka hivyo kutokana na mimi nilivyokuwa nafahamu.
Iko hivi, huyu dogo ni mraibu wa sigara na pombe
kali. Sasa anachoniambia kutokana na matumizi yake ya vilevi hivyo kuwa makubwa
amepatikana na tatizo la Saratani ya mapafu na ipo katika stage mbaya Sana,
naweza kusema ya mwisho kabisa.
Sikupata Nafasi ya kumuhoji mambo mengi kutokana
na hali aliyokuwa nayo (Alikuwa amelewa sana leo, pia alikuwa analia Kwa
uchungu sana) Hivyo muda mwingi niliutumia kumbembeleza kumfanya asijisikie
vibaya zaidi.
Kwa maelezo Aliyonipa anasema tatizo limeanza muda
kidogo lakini wakati anakwenda Hospital lilikuwa limeshamla zaidi ya 75% hivyo
Madaktari, Wamemweleza ukweli hapo alipofikia haiwezekani tena too late, hivyo
kwa kipindi chote hicho Amekuwa mtu Wa kutumia sindano ili kupunguza makali Ya
tatizo kumpelekea kwenye kifo.
Ameendelea kunieleza sindano anazochoma ni gharama
Sana na ni kila wiki hivyo imempelekea Kuuza baadhi ya vitu vyake kwa ajili ya
kuendelea na matibabu. Sasa kitu Walichomueleza hospital hizi siku za hivi
karibuni ni kwamba Stage aliofikia now hata hizo sindano haziwezi msaidia.
Uwezekano wa kuishi zaidi ya siku 30 kuanzia sasa labda itokee muujiza na neema
za Mungu. Kutokana na nature ya tatizo.
Kumbe dogo Aliambiwa apunguze matumizi ya hivyo
vitu hususani sigara ikiwezekana aache kabisa itamsaidia kwa kiasi fulani
lakini yeye akawa anapiga kama kawa.
Kilichonifanya nije jukwaani Hapa, Kwanza nafahamu
kama sigara zina madhara lakini chalii ni mdogo under 30, imewezekanaje
zimalize mapema hivyo?
Kama jibu ni ndio, basi kuna vifo vya wetu wengi
sana kutokana na matumizi ya sigara.
Kingine wataalamu wanieleze hii issue imekaaje
kuhusu upande wa matibabu, pia naamini kuna watu wamewahi experience hii issue
yaweza kuwa imempata rafiki, ndugu, jirani whatever..je ilikuwaje?
Dogo ndio amezidi kuchanganyikiwa anakunywa
mapombe hovyo anauza mali Zake hovyo amejikatia taamaa haoni tena thamani ya
haya maisha. Kilichoniuma Ananiambia ameniita kuniaga siku 😭 😭 😭
siku nikisikia amekufa basi sababu ni hiyo.
Hivyo kwa sasa Anahesabu siku na masaa kiukweli
roho imeniuma. Aisee wale wa vitaji wa sigara na mapombe makali, jifunzeni
kutokana na kisa hicho.
Nimepitia google kwenye chanzo fulani cha habari
kinasema Watumiaji wa tumbaku kuanzia Miaka ya 2005+ imeonekana kuwa na adhari
kubwa zaidi kuliko hizo za miaka ya nyuma.
Hivyo vifo vimeongezeka tena zaidi ni vijana na
jinsi ya kiume. Serikali iangalie kwa makini sana hili jambo tutapoteza nguvu
kazi ya taifa, wasiangalie tu kwenye kodi waangalie na maisha ya watu.
Karibu kwa mawazo, hoja ushauri. Nawasilisha🙏
CREDIT:
Jamii Forums.
KUTOKA NEEMA HERBALIST : Je zipo dawa ambazo
zinaweza kumsaidia mraibu wa sigara na pombe kurejea katika hali yake ya
kawaida? Yani kuacha kabisa kuvuta sigara na/au kunywa pombe ? Jibu ni NDIO
zipo dawa mbalimbali za asili zitokanazo
na mimea ambazo zina uwezo wa kumfanya mraibu pombe na/au sigara kuacha kabisa. Kazi kubwa ya dawa hizo
ni ku reverse addiction . Kufahamu
zaidi kuhusu tiba hii, wasiliana na duka
la Neema Herbalist kupitia simu namba 0766 53 83 84. Tunapatikana Dar Es
Salaam, Ubungo nyuma ya UBUNGO PLAZA jirani na shule ya Msingi UBUNGO NATIONAL HOUSING.
Comments
Post a Comment