Tafiti: Wagonjwa wa moyo nchini waongezeka kutoka 60
hadi 500 kwa siku
Wataalam wa moyo wamesema magonjwa ya moyo
yanazidi kuongezeka Nchini huku imani potofu zikiendelea kusambaa kuhusu tiba
ya magonjwa hayo.
Mkurugenzi wa Tiba katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Tatizo Waane amesema awali walikuwa wakipokea wagonjwa
50 hadi 60, lakini hivi karibuni wagonjwa wamefikia 300 hadi 500 kwa siku huku
Watoto wakiwa 30 hadi 40.
Amesema: “Takwimu zinaonesha karibu asilimia 30 ya
vifo Duniani vinasababishwa na magonjwa ya moyo.
“Takwimu za hapa Nchini zinaonesha takribani
asilimia 30 ya Watanzania wana shinikizo la juu la Damu, asilimi 30 wana tatizo
la ongezeko la lehemu kwenye damu na asilimia 33 hadi 35 wana uzito uliokithiri
na hivyo wako katka hatari ya kupata magonjwa ya moyo.”
Ameongeza kuwa mtindo mbaya wa maisha ukiwemo
ulaji mbaya, unjwaji pombe, matumizi ya tumbaku na kutofanya mazoezi vinachania
magonjwa ya moyo kwa kiasi fulani.”
Chanzo: Swahili Times
Kitambi, unene na
uzito kupita kiasi ni miongoni mwa mambo yanayo tajwa kuwaweka watu katika
hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo. Kufahamu
jinsi kitambi, unene, uzito ulio
zidi kinavyo tokea na jinsi kinavyo weza kudhibitiwa kwa
kutumia dawa za mimea ya asili,
tembelea link hii hapa chini :
https://neemaherbalist.blogspot.com/2016/12/fahamu-jinsi-kitambi-kinavyo-patikana.html
Comments
Post a Comment