Mkufunzi wa Mazoezi kutoka Shirika la Vyama
vya Magonjwa Yasiyoambukiza (NCD), Dk. Waziri Ndonde amesema katika kukabiliana
na magonjwa yasiyoambukiza kwa mwanamke anayenyonyesha mwenye uzito kupita
kiasi, anatakiwa kutumia dakika 150 kwa wiki kufanya mazoezi.
Dkt. Ndonde alitoa angalizo hilo jana wakati wa
kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza
kilichofanyika mkoani Mwanza na kudhuriwa na watu mbalimbali.
Alisema dhana kubwa ya kujikinga na kuzuia
magonjwa hayo ni pamoja na kuzingatia masuala ya lishe, kutokutumia tumbaku na
kuushughulisha mwili kwa kufanya mazoezi.
"Kuushughulisha mwili na kufanya mazoezi ni
kitu cha msingi cha kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na lishe,
ukiwa na tabia bwete, kuishi bila kuushughulisha mwili ni moja ya sababu ya
kupata magonjwa haya," alisema.
Mtaalamu huyo alisema serikali katika kutambua
hilo, mwaka jana kwenye wiki kama hiyo, Wizara ya Afya ilizindua mwongozo wa
kushughulisha mwili na kufanya mazoezi katika kuepuka tabia bwete.
"Mwongozo huu tayari umeshachapishwa na wadau
mbalimbali wamepewa wanaendelea kupata elimu, moja ya lengo kubwa la wiki hii
kwa mwaka huu ambapo tunaadhimisha hapa Mwanza, ni kuelimisha watu zaidi
mapendekezo ambayo yapo ndani ya mwongozo huo," alisema
Aliongeza kuwa mwongozo upo wazi kwa watu wa rika
zote, mfano wenye magonjwa sugu na wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU),
umeelekeza namna gani ya kuushughulisha mwili kwa kufanya mazoezi.
Pia alisema kulikuwa na shida nyingi kwa
wajawazito na waliojifungua, zinazotokana na mila na desturi wanakuwa na uzito
uliokithiri baada ya kujifungua kutokana na lishe wanayopewa.
"Mwongozo unamtaka huyu mama atumie angalau
dakika 150 kwa wiki wakati anatunzwa kupewa chakula bora ili apate maziwa ya
kumnyonyesha mtoto, dakika hizo azitumie kwa wiki kuhakikisha hatapata unene
uliokithiri, dakika hizo atatakiwa kufanya mazoezi yote muhimu," alisema.
Pia alisema mwongozo huo umetoa maelekezo kwa
wazee, yaani watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65, kuhusu nini wanapaswa kufanya
ili kuepuka magonjwa hayo.
Chanzo: IPP
Kitambi, unene na
uzito kupita kiasi ni miongoni mwa mambo yanayo tajwa kuwaweka watu katika
hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo. Kufahamu
jinsi kitambi, unene, uzito ulio
zidi kinavyo tokea na jinsi kinavyo weza kudhibitiwa kwa
kutumia dawa za mimea ya asili,
tembelea link hii hapa chini :
https://neemaherbalist.blogspot.com/2016/12/fahamu-jinsi-kitambi-kinavyo-patikana.html
Comments
Post a Comment