Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya maadhimisho ya Siku
ya Moyo Duniani tarehe 29/09/2022. Katika kuadhimisha siku hiyo wataalamu wa
JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano ya
uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa
jirani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi amewataka wananchi hususani wa mkoa wa
Arusha kuacha matumizi makubwa ya chumvi inayosababisha shinikizo la juu la
damu ambalo moja ya madhara yake ni kutanuka kwa moyo.
Prof. Janabi ambaye pia ni daktari bingwa wa
magonjwa ya moyo ametoa wito huo leo tarehe 29/09/2022 wakati wa maadhimisho ya
siku ya moyo duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medica
Centre.
Alisema watu wengi wanapenda kutumia chumvi nyingi
katika chakula hasa chumvi mbichi ambayo inaongezwa baada ya chakula kuiva,
unywaji wa juisi za kusindika au kuongeza sukari pindi wanapotengeneza juice
pamoja na kula kwa wingi vyakula vyenye wanga vitu ambavyo ni hatari kwa afya
ya moyo.
Mkurugenzi huyo mtendaji alisema ukanda wa Arusha
unawafugaji wengi na nyama inapatikana kirahisi kutokana na hali hii watu wengi
wanapenda kula nyama choma ambayo asilimia kubwa ya chumvi inayotumika ni
mbichi kitu ambacho kitasababisha changamoto ya afya kwa siku za usoni.
“Magonjwa ya kisukari na Shinikizo la damu
yanatokana na mtindo wetu wa maisha hivyo tupunguze sana ulaji wa chumvi na
matumizi makubwa ya sukari kwani asilimia 32 ya vifo vinatokana na magonjwa
yasioambukiza hususani moyo na matibabu yake ni gharama kubwa”,.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya maadhimisho ya siku
ya moyo duniani leo tarehe 29/09/2022. Katika kuadhimisha siku hiyo wataalamu
wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano
ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na
mikoa jirani.
“Ili kukabiliana na magonjwa ya moyo wananchi
tujitahidi kufuata mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kuacha uvutaji wa
sigara, kuacha unywaji wa pombe uliokithiri, kufanya mazoezi ikiwa ni pamoja na
kutembea hatua elfu 10 kwa siku pamoja na kula vyakula bora”, alisema Prof.
Janabi.
Aidha Prof. Janabi aliwataka wananchi kukata bima
za Afya kwani gharama za matibabu zimekuwa zikiongezeka kadri siku
zinavyokwenda lakini kama mtu atakuwa na bima ya afya itamsaidia kulipia
gharama za matibabu pindi atakapoumwa.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha Lutheran Medical
Centre (ALMC) Elisha Twisa aliwashukuru wataalamu ya JKCI ambao wako katika
hospitali hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo
kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani.
“Tunawashukuru wenzetu wa JKCI ambao wametuletea
huduma za kibingwa za matibabu ya magonjwa ya moyo katika mkoa wetu wa Arusha,
tutazidi kushirikiana nao ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii mara kwa
mara”, alisema Twisa.
Mkurugenzi huyo mtendaji wa ALMC alisema hospital
hiyo ipo mbioni kuanzisha kitengo cha matibabu ya moyo ili kuwasaidia wananchi
waweze kupata huduma hiyo karibu zaidi.
Mmoja wa wananchi aliyepata huduma za upimaji na
matibabu Kulwa Mayombi alisema yeye pamoja na wenzake wamefurahia kupata huduma
hiyo sanjari na elimu ya afya itakayowasaidia kuondokana na magonjwa yasiyo ya
kuambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo.
Katika kuadhimisha siku ya moyo dunia ambayo kauli
mbiu yake ni “fanya uamuzi sahihi kuhusu moyo wako” wataalamu wa JKCI kwa
kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano iliyoanza
tarehe 26 hadi 30 mwezi huu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa
wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani.
Credit : Mitandao mbalimbali
ya kijamii.
Kitambi, unene na
uzito kupita kiasi ni miongoni mwa mambo yanayo tajwa kuwaweka watu katika
hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo. Kufahamu
jinsi kitambi, unene, uzito ulio
zidi kinavyo tokea na jinsi kinavyo weza kudhibitiwa kwa
kutumia dawa za mimea ya asili,
tembelea link hii hapa chini :
https://neemaherbalist.blogspot.com/2016/12/fahamu-jinsi-kitambi-kinavyo-patikana.html
Comments
Post a Comment