Muhimbili waanza kutoa huduma kupunguza uzito, watatu wenye kilo 100+ wamepata huduma kwa Sh milioni 3.5 hadi 4
HOSPITALI ya Taifa ya
Muhimbili-Mloganzila,iliyopo jijini Dar es Salaam, imeanza kutoa huduma ya
kupunguza uzito uliokithiri, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na magonjwa
yasiyoambukiza.
Hadi sasa watu watatu wenye uzito zaidi ya
kilogramu 100 wamepata huduma hiyo inayogharimu kiasi cha Sh milioni 3.5 hadi
Sh milioni 4.
Akizungumza na waandishi wa Habari Leo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Muhimbili, Prof Mohammed Janabi, alisema hawatoi huduma hiyo kwa
sababu ya urembo bali wanalenga kusaidia watu.
“Hii ni operesheni yetu ya tatu leo na siku ya leo
tumewafanyia watu wawili hawa wote ni kilo 100 kwenda juu, wa kwanza kilo 160
na wengine kilo 105, hawajafanya kwa sababu ya urembo.
“Wiki moja iliyopita tulifungua kliniki ya mafuta
tunawakaribisha hospitali zingine ziweze kuleta wagonjwa wake kupata
huduma,”amesisitiza Prof Janabi.
Amesema utoaji huduma hiyo utahusisha tumboni
kupitia mdomo hali itakayopunguza kiwango cha chakula kwa muhusuka.
“Tutaweka kwa miezi nane, tutaingiza kupitia mdomo
hadi kwenye tumbo hakuna upasuaji tutatumia mitambo ifike mahali pake tutajaza
dawa linapunguza ukubwa wa tumbo ukila kidogo utashiba hivyo tunategemea uzito
utapungua.
Prof Janabi ameeleza kuwa faida kubwa ni kusaidia
kukukinga na magonjwa ya kisukari, kiharusi, moyo, kushindwa kupumua.
Amebainisha kuwa matibabu yatakayotolewa ni siri
ya mgonjwa, ambapo pia matibabu hayo huchuku siku mbili tu.
“Siku ya kwanza unaweza kusikia kama unavidonda
vya tumbo, lakini baada ya muda utaendelea kawaida, hospitali hatukaribishi
watu lakini tunawaomba wale wenye uzito mkubwa wafike kliniki, tuna kliniki ya
siku mbili hapa Mloganzila na siku mbili Muhimbili Upanga,” amesisitiza.
Pamoja na hayo amesema pindi mgonjwa anapopatiwa
huduma hiyo na kupungua atapata usaidizi wa mtaalamu wa lishe, ili asiongeze
tena kiwango cha kula na uzito kuongezeka tena.
“Kabla ya kumuhudumia tutapima vitu vingine vyote
ndo utakuja kupata huduma, faida kubwa ni kitu ambacho baada ya miezi nane
tutatoa na hali ya kula kidogo itaendelea na akirudi tabia ya mwanzo anaweza
kuwekewa mara nyingine hivyo ni vyema kuweka kiasi,” amesema.
Amesema mfumo wa Bima ya afya bado haujaanza
kutumika hata hivyo watu wafanye mazoezi, wale mlo unaotakiwa.
“Na matatizo mengine ni ya kurithi ukiwa na mtoto
ana uzito mkubwa mleteni wakati mwingine unaweza kukuta mtoto amezaliwa na kilo
nne watu wakaona ni kitu sahihi kumbe sio kweli,” amesema.
Amesema gharama ya huduma hiyo kwa India ni Sh
milioni 15 hadi Sh milioni 20 na Ulaya ni kuanzia Sh milioni 30 kwenda juu.
Amesema mwaka 2023 kwa kipindi cha Januari
wanatarajia kuwahudumia wagonjwa 12 kwa gharama ya Sh milioni 3.5 hadi Sh
milioni 4.
“Hii ni sehemu ya utalii tiba, hivyo nchi za
jirani tunatoa huduma hizi waje kupata huduma ni tiba salama kama
tunavyopandikiza figo, uloto na zingine wakitaka kupata huduma hapa ni
rahisi,”ameeleza Prof Janabi.
Credit : Habari Leo
Tatizo la
kitambi au unene/uzito kupitia
kiasi linaweza kudhitiwa
kwa kutumia dawa
zitokanazo na mimea
ya asili. Kufahamu jinsi tatizo
la kitambi na unene/uzito uliozidi
linavyo weza kudhibitiwa kwa
kutumia dawa za asili
zitokanazo na mimea, tembelea link hii hapa chini:
https://neemaherbalist.blogspot.com/2015/11/fahamu-jinsi-kitambi-kinavyo-patikana.html
Comments
Post a Comment