Wakati Watanzania na wadau wa masuala ya afya
na lishe wakisubiri ripoti ya Utafi ti wa Afya ya Uzazi na Mtoto (THDS) na
Utafi ti wa Kitaifa wa Lishe (TNNS) zote za mwaka 2022, yapo mambo makubwa
matatu yanayoikabili sekta ya lishe ikiwemo uzito uliokithiri, viribatumbo au
vitambi na udumavu.
Kwa upande wake, Ofisa Utafiti wa Taasisi ya
Chakula na Lishe (TFNC), Walbert Mgeni anasema kuwa katika utafiti walioufanya
mwaka 2018, kulingana na kipimo cha Body Mass Index (BMI) kinacholinganisha
kati ya urefu na uzito ulibaini kwamba asilimia 7.3 ya wanawake wenye umri kati
ya miaka 15 hadi 49 ni wembamba au wana uzito pungufu kiwango ambacho ni cha
juu ukilinganisha na mwaka 2014.
Anasema asilimia 10 ya wanawake waliobainika kuwa
na uzito pungufu ni kutoka Unguja Kaskazini, Pemba, Manyara, Kagera na Singida.
Kwa mujibu wa TNNS 2018, asilimia 31.9 ya wanawake wana uzito uliokithiri
ambayo inaonesha ongezeko kutoka asilimia 29.7 mwaka 2014.
Kiribatumbo kimeongezeka kwa asilimia 20. Mgeni
anasema kuwa mikoa inayoongoza kwa kuwa na wanawake wenye uzito uliokithiri na
viribatumbo ni Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mwanza na Kusini Unguja (Zanzibar).
Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa lishe wa mwaka
2018 ambao ulibainisha kuwa wanawake ndio wanaoongoza kwa kuwa na viribatumbo
kuliko wanaume kwani takwimu za THDS zinaonesha kuwa uzito uliokithiri
umeongezeka kutoka asilimia 28 mwaka 2015 hadi asilimia 32 mwaka 2018.
Kwa upande wa kiribatumbo wanawake wanaongoza kwa
kiwango cha asilimia 15 na wanaume asilimia 2.5.
Inaelezwa kuwa uzito uliokithiri ni moja ya
viashiria vya ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani, magonjwa ya
moyo na kisukari.
Kwa upande mwingine, magonjwa hayo ya lishe yamekuwa
fursa kwa wafanyabiashara wengi ambao huuza bidhaa zao kwenye mitandao ya
kijamii wakieleza namna ya kupunguza tumbo na nyama uzembe hususani kwa
wanawake.
Hivi sasa dawa zinazodaiwa kuondoa vitambi
zinauzwa kila kona. Kama hiyo haitoshi, ‘diet’ ndio neno pendwa kwa wanawake
huku wengi wao wakipata ushauri wa watu wasio wataalamu wa afya na
kuwasababishia athari kedekede.
Hata hivyo, mapinduzi ya sayansi na teknolojia,
kutofanya mazoezi na kutozingatia lishe bora kwa kula vyakula vyenye madini,
vitamini, wanga na protini huchangia kwa kiasi kikubwa matatizo hayo.
Athari za kiuchumi pia hutajwa kusababisha ulaji
usiofaa kwani huchangia upatikanaji wa vyakula vilivyoandaliwa kwa haraka,
unywaji wa vimiminika vya viwandani na kutozingatia mazoezi.
Maadhimisho ya Siku ya Uzito Uliozidi na
Kiribatumbo Duniani hufanyika Novemba 26, kila mwaka. Kwa mujibu wa utafiti wa
Shirika la Afya Duniani (WHO) uliochapishwa Juni 2021 kuhusu unene
uliopitiliza, umebaini zaidi ya watu bilioni 1.9 wenye umri kuanzia miaka 18
wana uzito uliopitiliza na watu milioni 650 wana vitambi duniani kote.
WHO ilibainisha kuwa wanawake ndio wanaongoza kwa
kuwa na vitambi kuliko wanaume kwa sababu ya asili ya miili yao kuwa na uwezo
mkubwa wa kuhifadhi mafuta mwilini (excess fat).
Mganga Mfawidhi wa Nsambo Health Care Polyclinic,
Dk Boaz Mkumbo anasema kitambi ni sukari ya ziada iliyohifadhiwa na homoni ya
insulini katika mfumo wa mafuta kwani kadri hifadhi ya sukari inavyozidi
mwilini ndivyo seli za mwili zinavyodumaa kitaalamu inaitwa insulin resistance.
Dalili za usugu wa homoni hiyo ni weusi shingoni
na sehemu kwenye mikunjo, kuwa na mikunjo usoni na shingoni, hali ambayo
inabadilisha damu na kuonesha kuwa homoni ya insulini ipo juu.
“Kitambi hakitokani na vyakula asili vya mafuta na
si sehemu ya mwili. Madhara ya kitambi hutokana na muda ambao umeishi na mafuta
ya ziada,” anasema Dk Mkumbo.
Anaeleza kuwa mwili haupendi mazingira ya sukari
nyingi hivyo mwili hujiendesha salama kwa wastani wa gramu tano za damu na
kwamba sukari yoyote ya ziada, mwili huifadhi.
Dk Mkumbo anasema homoni ya insulini kwenye damu
muda wote inatakiwa iwe chini na hupanda pale tu mtu anapokula chakula endapo
mtu atakuwa na lishe duni, homoni hiyo huwa juu hali inayosababisha homoni ya
Testosterone kushuka na kuongeza uzalishaji wa homoni ya kike ya Estrogen.
Pia anasema kwa kawaida kitambi kinaathiri msukumo
wa damu wa moyo ambao husukuma lita 5.6 za damu kila dakika (80mls kwa kila
mdundo).
“Ukiwa na kitambi unapunguza uwezo wa moyo kufanya
kazi ya ziada unakuwa na mapigo mabaya ya moyo, kupumua haraka haraka, ganzi
mwilini, kuvimba miguu inayobonyea na kukosa pumzi unapotembea au kupanda ngazi.
“Hiyo ni dalili mojawapo ya mwili kuzidiwa maji ya
ziada kwenye damu. Mtu mwenye uzito mkubwa homoni inayohifadhi na kushikilia
mafuta na inayozuia chumvi na maji visitoke, hushindwa kufanya kazi hiyo na
badala yake huzidisha kumimina ndani ya damu yako,” anasema Dk Mkumbo.
“Uzito uliokithiri ni moja ya viashiria vya
ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa moyo, saratani na
kisukari. Lazima tuhakikishe lishe bora inazingatiwa kwa kuendelea kutoa elimu
ili kupunguza magonjwa yanayoambukiza ambayo yanaligharimu taifa na familia kwa
ujumla,” anasisitiza.
Mkazi wa Dar es Salaam, Princess Dominic, anasema
hakuna siri kubwa ya kufuata katika maisha kama lishe bora. Anasema kuwa
kufanya mazoezi ya kupunguza mwili hususani kitambi bila kuzingatia lishe ni
kazi bure hivyo ili mtu aone mafanikio ya mazoezi anayofanya kwa ajili ya
kupunguza uzito, anatakiwa kufuata lishe bora.
“Baada ya kujifungua niliongezeka kilo hadi
kufikia 110 na hata umbo langu lilibadilika sikuvutiwa nalo, kuna wakati
nilikuwa natumia mkanda wa kupunguza tumbo ili ninapokwenda kwenye matukio
mbalimbali ya sherehe nionekane nimependeza. “Sikuwahi kuzingatia masuala ya
lishe kwani chakula changu pendwa ni chipsi mayai, mishikaki na pepsi baridi,
hali ilikuwa mbaya baada ya muda nilianza kutafuta watu wanaotangaza dawa za
kupunguza mafuta na uzito kwa haraka ingawa gharama zake ni ghali lakini
nilinunua ili kutimiza azma yangu ya kupunguza mwili, anaeleza Princess.
Anasema alitumia dawa nyingi ambazo nyingine
zilimsababishia kuharisha kama ambavyo wataalamu hao walimuelekeza, alianza
‘diet’ lakini alishindwa kuendelea ndipo daktari alimwelekeza kufuata lishe
bora ndipo alipata matokeo.
Jesika Sauli anasema kuwa tangu alipoacha kutumia
vyakula vyenye wanga, mafuta mengi na sukari ame- punguza mwili wake kwa hara-
ka na kwamba ataendelea kuzingatia ulaji unaofaa sambamba na kuelekeza familia
yake ili kuepuka magonjwa.
Credit: Mitandao mbalimbali ya kijamii
Kitambi, unene na uzito kupita kiasi ni miongoni mwa mambo yanayo tajwa
kuwaweka watu katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo.
Kufahamu jinsi kitambi, unene, uzito ulio zidi kinavyo
tokea na jinsi kinavyo weza kudhibitiwa kwa kutumia dawa
za mimea ya asili, tembelea link
hii hapa chini :
https://neemaherbalist.blogspot.com/2016/12/fahamu-jinsi-kitambi-kinavyo-patikana.html
Comments
Post a Comment