Imeelezwa kuwa kila vifo 33 kati ya 100
vinavyotokea nchini vinasababishwa na magonjwa hayo na robo 3 ya wananchi
hawajitambui kuwa wana tatizo hilo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasiyoambukiza
Dkt. James Kiologwe amesema Mjamzito mwenye Magonjwa hayo yupo hatarini
kujifungua watoto wenye uzito pungufu na kurithisha vizazi 4.
Takwimu za WHO zinaonesha Magonjwa yasiyoambukiza
yanachangia 74% ya vifo vyote duniani huku 86% ya vifo vikitokea katika nchi za
kipato cha chini na kati.
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanasababisha
vifo 33 kati ya vifo 100 ambavyo ni takriban vifo vinne katika kila vifo kumi
vinavyotokea Tanzania.
Hayo yamesemwa leo Novemba 9,2022 na Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya katika maadhimisho ya kudhibiti
magonjwa yasiyoambukiza (NCD) katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Amesema magonjwa yasiyo ya kuambukizwa nchini
yanachochewa na tabia bwete ya watu wengi wakiwamo vijana kutoshughulisha miili
huku wengi wakiwa hawafanyi mazoezi.
"Kuna tabia imejengeka miongoni mwa vijana,
wakitoka kazini badala wajishughulishe na mazoezi au kujadili mambo ya
maendeleo, wanaenda baa kunywa pombe kali na wengine wanatengeneza mchanganyiko
wa pombe kali wanakunywa, wanajitengenezea bomu mwilini bila kujijua,” amesema
Mmuya.
Aidha, amewataka wananchi kujenga tabia ya kupima
afya mara kwa mara ili kujua hali ya afya zako ikiwa ni pamoja na kuzingatia
ulaji unaofaa wa vyakula.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa
Yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Dk James Kiologwe amesema zaidi ya robo
tatu ya wananchi hawajitambui kuwa wana magonjwa yasiyoyakuambukiza na kutaka
elimu zaidi itolewe.
Amesema mwanamke mwenye magonjwa yasiyoambukiza
yupo katika hatari zaidi ya kujifungua watoto wenye uzito pungufu na pia wapo
kwenye hatari zaidi ya kurithisha vizazi vinne, cha kwanza, cha pili, cha tatu
na cha nne.
Katika maadhimisho hayo yenye kaulimbiu: ‘Badili
Mtindo wa Maisha Boresha Afya.’ Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
ambaye ni Mratibu Wadau Sekta ya Afya, Leticia Rweyemamu, amesema asilimia 74
ya vifo vinavyotokea duniani vinasabishwa na magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa mujibu wa Rweyemamu, mwaka 2012 kulikuwa na
vifo milioni 157 kati ya hivyo, milioni 41 vilichangiwa na magonjwa
yasiyoambukiza. Tangu mwaka 2016 takwimu hizo zimekuwa zikiongezeka na kufikia
asilimia 74.
“Kila mwananchi akijitambua, tutafika lengo la
kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa hayo ambayo ni mzigo mkubwa kwa familia
na taifa kwa kuwa licha ya kuwaathiri wagonjwa, huchangia ongezeko la
umaskini,”amesema.
Amesema mtindo usiofaa wa masiaha ukiwamo ulaji
mbovu ni miongoni mwa mambo yanayoongeza kasi ya magonjwa hayo ambayo ni pamoja
na kisukari, presha na moyo.
Credit : HABARI LEO
Kitambi, unene na
uzito kupita kiasi ni miongoni mwa mambo yanayo tajwa kuwaweka watu katika
hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo. Kufahamu
jinsi kitambi, unene, uzito ulio
zidi kinavyo tokea na jinsi kinavyo weza kudhibitiwa kwa
kutumia dawa za mimea ya asili,
tembelea link hii hapa chini :
https://neemaherbalist.blogspot.com/2016/12/fahamu-jinsi-kitambi-kinavyo-patikana.html
Comments
Post a Comment