Skip to main content

FAHAMU UKWELI KUHUSU DHANA YA UKUBWA WA MAUMBILE YA KIUME VS UDOGO WA MAUMBILE YA KIUME KATIKA KUWARIDHISHA WANAWAKE……





Kuna  idadi kubwa  sana  ya  wanaume  duniani, wanao  tafuta  namna  ya  kuongeza  ukubwa   wa maumbile  yao  ya  kiume.

SABABU  GANI   HUWAFANYA  BAADHI  YA  WANAUME  KUTAFUTA  DAWA  ZA  KUONGEZA  UKUBWA  WA  MAUMBILE  YA  KIUME  ?

Sababu  kuu  ni  moja  nayo  ni  kutafuta  heshima   kwa  wapenzi  wao.

 



KWANINI   WANAUME  HAWA  WANAFIKIRI  KUWA  KUWA  NA  MAUMBILE  MAKUBWA  YA  UUME  KUTAWAPA  HESHIMA  KWA  WAPENZI  WAO  ?


Sababu  kuu  ni  moja , nayo  ni    imani  potofu  “. Wanaume  hawa wanaamini  kuwa  wakiwa  na  maumbile  makubwa  ya  kiume, watapata  heshima  kwa  wapenzi  wao.

Kabla  hatujajiuliza  je  ni  kweli   kuwa  na  maumbile  makubwa  ya   kiume  humletea  mhusika  heshima  kwa  mpenzi wake,  kwanza  tujiulize  dhana  au  imani  hii  inatoka  wapi.
Katika  kujua  mahali  inakotoka dhana  ya  kwamba  kuwa  na  maumbile  makubwa  ya  kiume  huleta  heshima  kwa  wanawake, ni  vyema  tukaitazama  historia  ya  dawa  za  kuongeza  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume.

HISTORIA  YA  DAWA  ZA  KUONGEZA  UKUBWA  WA  MAUMBILE  YA  KIUME.
Dawa  za  kuongeza  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume  ziligunduliwa  kwa  mara  ya  kwanza  nchini  Marekani  mnamo  karne  ya  19.
Katika  kipindi  hicho, dhana  ya  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume  haikuwa  na  mashiko  sana.
Kampuni  za  kibepari zilizo  hodhi  ugunduzi huo, zilitafuta  njia  ya kuuza dawa  hiyo.
Moja  kati  ya  njia  kuu  zilizo  pendekezwa  ilikuwa  ni  pamoja  na  kutengeneza   na  kusambaza  propaganda    inayo  tukuza  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume.
Propaganda  hiyo  ili  sambazwa  kwa  njia  ya  vyombo  vya  habari ( media ),  vitabu , filamu  pamoja  na  filamu  za  ngono.
Mada  za  wanawake   kutoridhishwa  na wapenzi  wao  kwa  sababu  wana  maumbile  madogo  ya  kiume  zili  tamalaki  kwenye vyombo  mbalimbali  vya  habari  hususani magazeti.
Kwenye  filamu  za  ngono  “ pornography “ wahusika  wanaume  wote  walionekana  kuwa  na  maumbile  ya  kiume  makubwa  kupita  kiasi  na  wahusika  wanawake  walionekana  kufurahia   mapenzi.
Wanaume  walio  semekana  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume  walichekwa  na  kudhihakiwa  sana.

Taratibu  propaganda  hii  ili  enea  nchini  Marekani  na  hatimaye  kusambaa  katika  sehemu  kubwa  ya  ulimwengu.
Nia , lengo  na  madhumuni  yao  ni  kujenga  hofu  kwenye   fikra  za  wanaume  wanao  jiona  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume, na hatimaye  kuwafanya  kuwa  wateja  wa  dawa   walizo  gundua  za  kuongeza  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume.
Wamefanikiwa  kwa  kiasi  kikubwa  sana. Wanaume  wengi  duniani   hata  wale  wasio  na  maumbile  yanayo itwa  madogo  wamekuwa na  wasiwasi  juu  ya  uana  ume  wao  na  matokeo  yake  wamekuwa  wakihangaika  huku  na  kule  kutafuta  tiba  ya  kuongeza  ukubwa wa  maumbile  ya  kiume.

ATHARI  YA  DHANA  YA  UKUBWA  WA  MAUMBILE  YA  KIUME  KWA  WANAUME  WA  KITANZANIA.
Uchunguzi  na  utafiti  wetu  umetuwezesha  kugundua  kuwa, dhana  ya    maumbile  makubwa  ya  kiume  kuleta  heshima  kwa  wanawake    imeenea  na  kumea  mizizi  miongoni  mwa  wanaume  wengi sana  hapa  Tanzania.
Kama  matabibu  wa  dawa  asilia, tumekuwa  tukipokea  simu  na  emails  nyingi sana  kutoka  kwa  wanaume  wanao  sema  wana  maumbile  madogo  ya  kiume  na  kwamba  wanatafuta  tiba  ya  kuongeza  ukubwa  wa maumbile  yao.
Wengi  wa  wateja walio  katika  kundi  hili, tumekuwa  tukiwasikiliza  na  kuwapa ushauri ambao  wengi  wao  hushukuru sana  baadaye.
Nina  amini  wewe  unaye  soma  makala  haya, unaweza kuwa mwanaume  ambaye  upo  katika  kundi  la  wanaume  wanao  jiona  wana  maumbile  madogo  ya  kiume  na  unatafuta  namna  ya  kuongeza  ukubwa  wa  maumbile  yako.
Nina  amini  unajua  namna  dhana  ya  ukubwa   wa  maumbile  ya  kiume  ilivyo  ota  mizizi  katika  jamii  yetu, hivyo  sina  sababu  ya  kuelezea  sana  namna  ambavyo  dhana  hii  imemea  na  kuota  mizizi  ila  ninataka    ufahamu  mambo  ya  msingi  kuhusu  ukweli na  uhalali  wa  dhana  hiyo.
Katika  kuhakikisha  una upata  ukweli na  uhalali kuhusu  dhana  ya  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume  katika  kuleta  heshima   ya  mwanaume  kwa  mwanamke, nimekusudia  usome   mambo  yafuatayo.

JE!  NI  KWELI  UKUBWA  WA  MAUMBILE  YA  KIUME   HULETA  HESHIMA   KWA  WANAWAKE ?
Kabla  sijakueleza  kuwa  hakuna    “definition”   yoyote  ya  kisayansi  inayo  “ define “  ukubwa wa  maumbile  ya  kiume  ni  kitu  gani  na  udogo  wa  maumbile  ni  kitu  gani,  ninapenda  kukufahamisha  kuwa  hakuna  utafiti  wowote  wa  kisayansi  unao  thibitisha  kwamba, ati  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume  ndio  huleta  heshima  ya  mapenzi  kwa  wanawake.
Kama  sayansi  haija   define  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume  ni  kitu  gani, udogo  wa  maumbile  ni  kitu  gani, hali  kadhalika  haija  thibitisha  kwamba  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume  ndio huleta  heshima   ya  mapenzi  kwa  wanawake, basi  mtu  hatakiwi  kusikika  akisema  kuwa  maumbile   makubwa  ya  kiume  ndio huleta  heshima  ya  mapenzi  kwa  wanawake  unless  otherwise  aje  na  authority  inayo  mpa  kibali  cha  kusema  hivyo.

Mbali  na  ushahidi  wa  kisayansi, tukija  katika  hali  halisi, uchunguzi wetu  umetuwezesha  kugundua  kuwa, ukubwa wa  maumbile  ya  kiume  si  miongoni  mwa  mambo  yanayo weza  kuleta  heshima  ya  mapenzi  kwa mwanamke.
UDOGO  WA  MAUMBILE  YA  KIUME  NI  NINI ?
Kama  tulivyo  sema  hapo awali, hakuna  definition  ya  kisayansi  inayo  define  nini  udogo  wa  maumbile  ya  kiume. Definition zilizopo   zinatokana na  mawazo   ya  kimapokeo  ya  watu.

DEFINITION  YA  MWANAUME  MWENYE  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME.
Tumeisha  ona  hapo  juu  kuwa  hakuna  definition  yoyote  iliyo  thibitishwa  kisayansi  ambayo  ina  define   udogo  ama  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume.
Kwa  kuwa  hakuna  definition  ya  udogo  wa  maumbile  ya  kiume, basi  ipo definition  ya  mwanaume  mwenye  maumbile  madogo  ya  kiume.
MWANAUME  MWENYE  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME  ni  mwanaume  anaye dhani  au  anaye  amini  kuwa  ana  maumbile  madogo  ya  kiume.

Maana  yake  hapa  ni  kwamba, suala  la  udogo  wa  maumbile  ya  kiume, halipo  katika uhalisia  wake  bali  lipo  katika  mawazo  ama  fikra  zake.
Yeye  ana  amini  tu  kuwa  ana  maumbile  madogo  ya  kiume  lakini  kiuhalisia  hana  hayo maumbile  madogo  ya  kiume, kwa  sababu  udogo  wa  maumbile  ya  kiume  ni  dhana  ya  kufikirika.
Anacho  takiwa  kufanya  mwanaume  huyu  ni  kubadilisha  fikira  na  mtazamo wake  kuhusu  size  ya  maumbile  yake  ya  kiume.

KITU  GANI  KINALETA  HESHIMA  YA  MAPENZI  KWA  MWANAMKE.
Kinacholeta  heshima  ya  mapenzi  kwa  mwanamke  ni  uwezo  wa  kumridhisha  kimapenzi  bila  kujalisha  size  ya    maumbile  yako  ya  kiume.  Kama  mwanaume, unachotakiwa  kuwa  nacho  ni  nguvu  za  kutosha  za  kiume  zisizo  na  mashaka  yoyote  pamoja  na uwezo  wa  kuhakikisha  mpenzi  wako  anafika  kileleni  wakati  wa tendo  la  ndoa.
Anacho  taka  mwanamke  wakati  wa  tendo  la  ndoa ni  kufika  kileleni, “ ukubwa “  au  “ udogo “  wa  maumbile yako  haumsaidii  chochote.


ATHARI  ZA  KUWA  NA  KUAMINI  UNA  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME.
Mwanaume  anaye  amini  ana  maumbile  madogo  ya  kiume, hupatwa  na  changamoto nyingi sana.
Chache  kati  ya  changamoto  hizo  ni  kama  ifuatavyo:

i.                     Kushindwa  kujiamini  kama  anaweza  kumiliki  mwanamke; Matokeo  yake  anakuwa  hawezi  kuwa  na  uhusiano  wa  kimapenzi  na  wanawake  wa  mtaani  kwake  ama  ofisini  kwake  kwa  sababu  eti  anaogopa  watamdhihaki  kwa  kuwa  na  maumbile  madogo.
Mwisho  wa  siku, huwa  wateja  wazuri  wa  madada  poa  kwa  sababu  huko  wana  amini  madada  poa  hawawajui  na  hawawezi  kuwa  interested  na  size  ya  maumbile  yao.
ii.                   Kuwa  wateja  wa  madadapoa  kuna  waweka  katika  hatari  kuu  ya  kuambukizwa  magonjwa  ya  zinaa  na  ukimwi.
iii.                  Kupoteza  muda  wao  mwingi  wakifikiri  kuhusu  kuongeza  ukubwa  wa  maumbile  yao. Hapa  unaweza  kukutana  na  mwanaume  ana miaka zaidi  ya  arobaini  na  tano  lakini  bado  ana  amini  siku  moja  atapata  fursa  ya  kuongeza  ukubwa  wa  maumbile  yake  ya  kiume  na  kujenga  heshima  kwa  mpenzi  wake..
“ Dokta. Wanawake wameni  nyanyasa  sana  kwa  sababu  ya  udogo  wa  maumbile  yangu, ila  naamini  siku  moja  mambo  yangu  yatakuwa  mazuri  na  mimi  nitakuwa na  maumbile  makubwa “….. Haya  ni maneno  ya  mwanaume mwenye  umri  wa  miaka  49, na  inawezekana  amekuwa  na  ndoto  hiyo  tangu  akiwa  na  miaka  kumi  na  nane.

iv.                  Kwa  ufupi  mwanaume  anaye  amini  kuwa  ana  maumbile  madogo  ya  kiume, hupunguza  furaha  yake  kwa  asilimia  kubwa  sana. Imani  hiyo  huwa  sehemu  ya  maisha  yake  na  humfanya  kuwa  mnyonge  sana.,Hata  anapokuwa  katika  mahusiano, huwa  mtu asiye  jiamini. Haamini  kama  mwanamke  wake  anaweza  kuvumilia  kuwa  na  mwanaume  mwenye “ maumbile  madogo”  kama yeye  na  siku zote  huamini  mke  wake  ana  mpenzi  ana  mpenzi  wa  pembeni. Wivu hutawala. Kila  kitu  kisicho  na  majibu  ya  kueleweka  kitakuhishwa  na  kucheat  kwa  sababu  yeye ana  amini   ana  maumbile  madogo.

FACTS  KUHUSU  “ MAUMBILE  MAKUBWA  YA  KIUME    VS   “ MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME 

1.           Wanaume  wenye  maumbile  madogo  ya  kiume  hufanya  sex  mara  nyingi  sana  kuliko  wanaume  wenye  maumbile  makubwa  ya  kiume.
Mfano  mzuri  ni  wachina. Wao  ndio  wana ongoza  kwa kuwa  na  idadi  ya  watu  duniani  na  ndio  wanao  semwa  kuwa  na   maumbile  madogo  ya  kiume  kuliko  watu  wote  duniani.

2.           Wanawake  wengi  hawapendi  kuwa  na  mahusiano  na  wanaume  wenye  maumbile  makubwa  ya  kiume  kupita  kiasi  kwa  sababu  wanadai  yanawaharibu maungo yao.
3.           Wapo  wanawake  wengi  wanao  wa acha  wanaume  zao  ambao  wana  maumbile  makubwa  ya  kiume  na  wanakwenda  kuwa  na  wanaume wenye  maumbile  madogo  ya  kiume  na sababu  inaweza  isiwe  pesa.
4.           Mwanaume  mwenye  maumbile  madogo  ya  kiume  yenye  nguvu za  kutosha  ni  bora  na  ataheshimika  kuliko  mwanaume  mwenye  maumbile  makubwa  ya  kiume  yasiyo  na  nguvu.


KUSINYAA   KWA   UUME   VS   MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME.
Wanaume wengine  hawana  maumbile  madogo  ya  kiume, bali  wana  maumbile  yaliyo  sinyaa  kwa  sababu  ya  vitu  mbalimbali  kama  vile punyeto  ya  muda  mrefu  au  kuugua  magonjwa  kama  vile  chango la  kiume  nakadhalika.
Tatizo hili  linatibika  kwa  kunywa  dawa  maalumu  inayo  imarisha  mishipa  ya  uume  ulio  legea  na  kuufanya  urudi  katika  hali  yake  ya  kawaida.

KUKUZA  MAUMBILE  YA  KIUME  KWA  DAWA ASILIA.
Nawashauri   wanaume  wano  fikiria  kukuza  maumbile  yao  ya  kiume, wafikirie  zaidi  kuongeza  nguvu  za  kiume  kuliko  kukuza  maumbile  yao ya  kiume.
Lakini  kama  unafikiri  ni  lazima  ukuze  ukubwa  maumbile  yako  kwa  dawa  asilia, basi  unaweza  kufanya  hivyo  kwa  kutumia  mchanganyiko  wa  dawa  zifuatazo ;
i.                     Unga  wa  Fil  fil  ab yadh  au  fil  fil  nyeupe
ii.                   Unga  wa  kiberiti  upele
iii.                  Unga  wa  mti wa  mvunge
iv.                  Pamoja  na  ambari  orijino  ile  ya  rangi  nyeupe.
Vitu  hivyo  vinachanganywa  pamoja  na  asali  halafu  mhusika  anakuwa  anatumia  kujichua  sehemu  husika  asubuhi  na  jioni  kwa  siku  thelathini. Maumbile  yake  yataongezeka.
MAKALA  HAYA  YAMEANDALIWA  NA  NEEMA HERBALIST  BLOG . TUNAPATIKANA  UBUNGO  DAR  ES  SALAAM  KWA  SIMU NAMBA  0766  53  83  84.

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...