Ngipeni, mwanamke raia wa Afrika Kusini, anaye daiwa kuwa bikira katika umri wa miaka 64. |
Ngipheni kutoka
KwaMafunze ,Pietermaritzburg,Afrika
Kusini ni bikira
mwanamke bikira mwenye
umri wa miaka
64. Alilazimika kubaki
bikira kwa muda
wote huo kwa
sababu hiyo ndio ilikuwa njia pekee ya
kushiriki katika ngoma za
utamaduni wa kabila
lake, ngoma inayo fanyika
kila mwaka kwa
ajili ya mfame
wao Goodwill Zwelithini ambaye huitwa
Umkosi Womhlanga.
Amekuwa sehemu
ya ngoma hiyo
tangu akiwa teenager
“
Kabla hatujaenda kwenye
sherehe za ngoma, walezi
wetu walitumia kuhakikisha
kuwa tupo bikira
kwa sababu ngoma
hizo ni kwa
ajili ya wanawake
bikira “alisema .
Ingawa
bado yupo bikira, Ngipheni anasema amekuwa
akipata hamu ya
kufanya mapenzi kwa muda
mrefu.
“ Njia
pekee niliyo itumia
kujizuia na hamu ya
kufanya mapenzi, ni kwa
kukumbuka ushauri wa
wazazi wangu kwamba kupatwa na
hamu ya kufanya
mapenzi ni jambo la asili
kwa kila mwanadamu.
Anasema alipokuwa msichana, vijana wengi
walijitokeza kumchumbia. “
Wote niliwatolea nje
kwa sababu nilitaka
kuendelea kuwa bikira.”
Ngipheni anatoboa pia
aliwahi kuwa na
rafiki wa kiume
ambaye baadaye alikuja
kuwa mchumba wake.
“ Enzi zetu wachumba zetu hawakuwa na haraka ya ngono. Walituheshimu sana. Niliachana na mchumba wangu kwa sababu ali cheat.”
Ngipheni anaongeza
kuwa yupo salama
na magonjwa ya
zinaa. Anasisitiza kuwa hamaanishi
kuwa wasichana wasifanye
mapenzi au wasiolewe.
“ Kama unafanya
mapenzi, fanya mapenzi salama
na ufanye hivyo
baada ya kufunga
ndoa. Utakapo funga ndoa
mwambie mume wako
muende mkapime v.v.u.
Hii itasaidia kupunguza
kasi ya maambukizi
ya v.v.u pamoja
na mimba za
utotoni. “
Mlezi wa Ngipheni, Zithobile Mbhele
anasema amefanya kazi
na Ngipheni kwa
zaidi ya miaka
thelathini na anamsifu
kwa kuwa mfano
mzuri kwa wanawake wanaoishi
katika jamii yake.
CREDIT : MASHIRIKA
MBALIMBALI YA HABARI
Comments
Post a Comment