Chuo
cha tiba ya miguu nchini Uingereza kinasema karibuni kumekuwa na ongezeko la
maambukizi ya maradhi yanayosababishwa na kuvu kutokana na kuvuma kwa mtindo wa
kuvalia viatu bila soksi, hasa miongoni mwa vijana.
Mtaalamu
Emma Stephenson anasema amekuwa akipokea wanaume wa kati ya miaka 18-25 walio
na matatizo kwenye miguu yao ambayo yametokana na kutovalia soksi au kuvalia
viatu visivyowatosha vyema.
Kutovalia
soksi siku hivi kumekuwa mtindo maarufu wa mavazi, na mwanamuziki Sam Smith ni
miongoni mwa watu wanaojitokeza hadharani wakiwa na viatu bila soksi.
Wanaume wengi
katika maonesho ya mitindo pia mara nyingi huonesha mavazi wakiwa na viatu bila
soksi.
Mwanamuziki
Tinie Tempah amejishindia tuzo nyingi kwa sababu ya mitindo na mara nyingi
katika maonesho ya mitindo ya Londo huketi viti vya mbele.
Yeye
pia huwa mara nyingi havai soksi - lakini anafahamu madhara yake?
"Miguu ya
binadamu kwa kawaida hutoa nusu painti (ambayo ni sawa na lita 0.28) ya jasho kila
siku," Emma Stephenson anasema.
"Unyevu
mwingi na joto unaweza kusababisha maambukizi ya maradhi yanayotokana na kuvu
mfano ugonjwa unaosababisha mwasho na kuchubuka kwa ngozi (kwa Kiingereza
athlete's foot)."
Kwa
mujibu wa Emma, madhara yake yanaweza kuwa mabaya
"Moja ya
visa vibaya nilivyowahi kukumbana navyo ni cha mwanamume mmoja wa miaka 19
aliyefanya kazi ya kuosha magari. Miguu yake ilikuwa inatokwa na jasho sana na
ilikuwa imechubuka sana."
Lakini
bila shaka itachukua ujasiri kumwambia bingwa wa UFC Conor McGregor kwamba
anaweza kupata matatizo kutokana na mtindo wake wa kuvalia viatu.
Emma anashauri
kwamba siri ni kutozidisha, iwapo bado utataka kutovalia soksi.
Jaribu
usivae viatu bila soksi kwa muda mrefu.
Jaribu pia
kuweka kitu cha kukausha jasho kwenye soli ya kiatu chako kabla ya kukivalia
bila soksi.
Kadhalika,
kuwa makini kuchunguza miguu yako. Ukigundua unaumwa pahali tafuta usaidizi
upesi.
CREDIT
: BBC SWAHILI
Comments
Post a Comment