Siku chache zilizopita nilieleza kuhusu sababu kubwa zinazowafanya
wanaume wengi kupoteza uwezo wa kutungisha mimba hata kama nguvu zao za jinsi
zipo sawa.
Hata hivyo, utafiti unaonyesha kuwa hivi sasa asilimia kubwa ya
wanaume husumbuliwa na tatizo hilo bila wao kujijua.
Lakini kutokana na maswali mengi niliyoyapokea, nawapongeza
wasomaji wetu kwa mapokeo ya somo lile lililosababisha niandike makala haya.
Ni ukweli usiopingika kuwa tatizo la kupoteza uwezo wa kuzaa
linawaathiri kwa kiasi kikubwa wanawake kuliko wanaume.
Wanawake wengi ndiyo waathirika wakubwa kuliko wanaume inapofikia
suala zima la afya ya uzazi na matatizo yake kwa ujumla.
Dalili kubwa inayoonyesha mwanamke hana uwezo wa kuzaa inaanzia
pale anapopoteza uwezo wa kushika mimba baada ya kujaribu kwa kipindi cha miezi
6 na kuendelea.
Kupata hedhi inayozidi siku 35 na kuendelea na kupata pia hedhi
iliyo chini ya mzunguko (chini ya siku 21), kuyumba kwa tarehe za hedhi au
kutopata hedhi kwa baadhi ya miezi, kuna tafsiri kwamba mwanamke anakosa
urutubishwaji wa mayai yake.
Wanawake wengi wamejikuta wanaangukia kwenye matatizo haya kutokana
na sababu mbalimbali ambazo wakati mwingine zinachangiwa na aina ya maisha
wanayoishi au hata matatizo ya kurithi na kupatwa na aina nyingine ya magonjwa
ambayo yanaenda kuathiri mfumo wa uzazi moja mkwa moja.
Sababu zinazowafanya kutoshika mimba
Sababu ya kwanza ni matatizo katika urutubishwaji wa mayai.
Matatizo katika urubishwaji wa mayai yanajitokeza baada ya mayai yanayokua
hayajakomaa kwenye ovari zake au ovari zenyewe zinashindwa kuachia mayai
yaliyokomaa hadi tarehe ambazo mwanamke zinamruhusu kushika mimba. Kitaalamu,
tatizo hili linaitwa premature ovarian failure.
Tatizo hili huwa linawapata wanawake wengi na ni vigumu kwao
kushika mimba.
Dalili za tatizo
Zipo dalili zinazoashiria kuwa mwanamke ana tatizo hilo ambazo ni
pamoja na kukosa baadhi ya mizunguko yake ya hedhi.
Nyingine ni pale anapokaribia kupata hedhi, hujisikia maumivu ya
kawaida ya tumbo au maumivu ya kawaida au muwasho kwenye matiti na maumivu ya
kiuno.
Sababu nyingine ni baadhi ya matatizo yanayojitokeza kwenye mfuko
wa uzazi.
Hata hivyo, wataalamu wa magonjwa ya wanawake wanasema wakati
mwingine tatizo la kutopata ujauzito husababishwa na mwanamke mwenyewe.
Kwani baadhi yao wana tabia ya kutoa mimba kiholela bila kujua kuwa
kufanya hivyo kunaweza kuwasababishia matatizo kwenye mfumo wa uzazi.
Kwani wengi wao hutoa mimba bila kufuata ushauri wa wataalamu wa
afya.
Tatizo hilo linapaswa kufahamika kwa wanawake wenyewe kuwa utoaji
wa mimba na hasa mara kwa mara bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya au
madaktari husababisha kuacha baadhi ya mabaki ya uchafu wa mimba zilizoharibiwa
kwenye mfuko wa uzazi bila wao kujua.
Hivyo, si ajabu kwa mwanamke huyu akashindwa kushika ujauzito hapo
baadaye atakapoamua kuzaa, kutokana na mfuko wake wa uzazi kuvurugika.
Lakini pia baadhi ya matatizo mengine yanayojitokeza kwenye mfuko
wa uzazi ni uwapo wa uvimbe ambao kitaalamu huitwa fibroids.
Na wakati mwingine nje ya ukuta wa mfuko wa uzazi kunaweza
kujitokeza baadhi ya tishu zinazojijenga kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi.
Tishu hizo zikikua na kuongezeka zinaweza kumletea mwanamke tatizo
la kushindwa kubeba ujauzito.
Tatizo hilo kwa jina la kitaalaamu linaitwa endometriosis na ni
muhimu kupata ushauri wa daktari ili kuchunguza uwezekano wa kuwapo kwa tatizo
hilo.
Endometriosis mara zote huambatana na dalili za maumivu makali
wakati wa hedhi au wakatiwa tendo la ndoa au kutokwa na damu nyingi wakati wa
hedhi ikiambatana na mabonge mazito na maumivu kwenye mfumo wa uzazi hadi
kwenye kiuno.
Ni vema kuwaona watoa huduma za afya ukiona dalili hizi mara moja.
Tatizo lingine ni mabadiliko yanayojitokeza kwenye mfumo wa homoni.
Wanawake wengi wanasumbuliwa na tatizo hilo bila kujijua. Kuyumba
kwa uwiano wa mfumo wa homoni mwilini ni tatizo lingine ambalo kwa asilimia
kubwa pia huwakumba wanawake.
Kisayansi, imethibitika kuwa kuyumba kwa mfumo wa homoni ni moja ya
matatizo makubwa yanayowafanya wanawake washindwe kushika mimba.
Mchakato mzima wa upevushwaji na urutubishwaji wa mayai kwenye
mfumo wa uzazi wa mwanamke kisayansi, unaratibiwa na mfumo wa homoni.
Hivyo, kuyumba kwa mfumo huo huathiri moja kwa moja mchakato mzima
wa utungishwaji mimba.
Ni vema kumuona daktari kwa ajili ya vipimo kama ikitokea mwanamke
anashindwa kupata ujauzito ili kubaini kinachosababisha tatizo hilo.
Sababu nilizozieleza ni chache kati ya nyingi zinazosababisha
matatizo haya. Ushauri wangu ni kujenga ukaribu na watoa huduma za afya kwa
ajili ya msaada wa uchunguzi na matibabu.
CREDIT :
MWANANCHI NEWSPAPER
MAKALA NYINGINEZO
JINSI KISUKARI KINAVYO SABABISHA MARADHI YA NGUVU ZA KIUME
JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA NA JINSI UNAVYO WEZA KUKIONDOA KWA TIBA ASILIA
JINSI PUNYETO INAVYO SABABISHA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
IJUE SAYANSI YA NGUVU ZA KIUME
UHUSIANO KATI YA UNENE ULIO ZIDI NA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZAP KIUME
KISA UGONJWA WA KISUKARI MWANAMKE AMKIMBIA MUMEWE WA NDOA NA KWENDA KUISHI NA JIRANI
KUTANA NA MWANAMKE AIYE JITOLEA KUMTIBU MUMEWE MARADHI YA AJABU
PUNYETO ILISABABISHA NINUSURIKE KWENDA JELA
Comments
Post a Comment