Skip to main content

NJIA SAHIHI YA KUTUMIA VIMIMINIKA MBALIMBALI KATIKA KUANDAA NA KUTAYARISHA DAWA ZA ASILI

Image result for asali ya  tende images  neema  herbalist
Asali ya  tende.  Asali  ya  tende  ni  moja  kati  ya  vimiminika  vinavyo  tumika  kuandaa  na  kutayarisha  dawa za  asili  zenye  kutibu  magonjwa  mengi  kwa  wakati  mmoja.
Dawa  za  asili na  lishe  mbalimbali za  asili, huweza  kuandaliwa  na  kutayarishwa  kwa  kutumia  vimiminika  mbalimbali kulingana na  lengo  la  kutumia  dawa  husika.
Dawa  za asili  zinaweza  kuandaliwa  kwa  kutumia vimiminika  mbalimbali  kama  vile :
1.    Maziwa  fresh  ya  n’gombe : Baridi, vuguvugu  au  ya  moto
2.   Maziwa  fresh  ya mbuzi  : Baridi, vuguvugu   au  ya  moto
3.   Maziwa  fresh  ya ngamia : Baridi , vuguvugu  au   ya moto,
4.   Maji ya  baridi, vuguvugu  au ya  moto
5.   Mafuta  ya  nyonyo
6.   Mafuta  ya  habbat soda
7.   Mafuta  ya  mzeituni
8.   Asali mbichi ya  nyuki  wadogo au  nyuki wakubwa
9.   Asali  ya  tende
10.                     Siki  za  aina  mbalimbali  kama vile, siki ya  Zabibu, Apple  Cidar  Vinegar  nakadhalika.
11.                     Maji  ya  Rose  ( Rose  Water )
12.                     Thyme  Water
13.                     Tui  la  Nazi
14.                     Ute  wa  mayai  ya kuku  wa  kienyeji
15.                     Mafuta  ya  n’gombe ( samli )
16.                     Juisi  za  matunda  mbalimbali kama  vile mananasi, miwa ,maembe, maparachichi, matango nakadhalika
17.                     Juisi  ya  vitunguu  maji
18.                     Juisi  ya  vitunguu swaumu
19.                     Juisi  ya  tangawizi 
20.                     Mvinyo mwekundu
21.                     Pamoja  na  vimiminika  vingine  ambavyo  havijatawa hapo juu.

Mtumiaji wa  tiba  asilia  anatakiwa  kuzingatia   kutumia  vimiminika sahihi  na kufuata  taratibu  na  njia  sahihi  katika  kutumia vimiminika  hivyo  katika kuandaa  na kutayarisha  dawa  yake kwa ajili ya  matumizi.
Hii  ni kwa sababu  kila kimiminika  kinacho  tumika katika  kutayarisha  dawa  za  asili, huwa  na  faida  zake  katika  mwili wa  mwanadamu endapo  kitatumika kwa  kufuata  utaratibu  sahihi.

Unapokuwa  unaandaa  na  kutayarisha  dawa  ya  asili  ambayo  inatumika  kwa  kunywa  kwa  ajili  ya  matumizi  yako  unatakiwa  kuzingatia  yafuatayo:

1.   Aina  ya  kimiminika   kinacho takiwa  kutumika  kuandaa  na  kutayarisha  dawa yako.
2.   Hali  ya  kimiminika  hicho.Hapa  unatakiwa  kujiuliza  hicho kimiminika  chako  kinatakiwa  kuwa  katika  hali gani ?  Kinatakiwa  kuwa  cha  baridi? Vuguvugu ? au  cha  moto ?
3.    Kitu  kingine  unacho  takiwa kuzingatia  ni namna  ya  kuandaa na  kutayarisha  dawa  yako  kwenye  kimiminika  hicho..  Hapa  unatakiwa  kuzingatia   whether  unatakiwa    kuchemsha  dawa  yako  kwenye  moto   mdogo ( moto  unaowaka taratibu  )  au  unatakiwa  kuchemsha dawa  yako  kwenye  moto  mkali .

Hii  ni  kwa  sababu  zipo  baadhi  ya  dawa  hutakiwa  kuchemshwa  kwenye  moto  mdogo  au moto  unaowaka  taratibu   wakati  dawa  zingine  hutakiwa  kuandaliwa kwenye    moto  mkali  ili  ziive kwa  haraka.

Endapo  utashindwa  kuzingatia  taratibu  zilizo tajwa  hapo  juu, basi  unaweza  kushindwa  kupata  virutubisho  vya  dawa  unayo  taka  kuitumia  na  hivyo  kushindwa  kupata  matokeo  unayo  yahitaji.

Hii  ni  kwa  sababu  namna   au  njia unazo  tumia  kuandaa  na  kutayarisha  dawa yako   ya  asili  inaweza  kuimarisha  ama  kuua  virutubisho  au  nguvu  ya  dawa  ya  husika.

Zipo  dawa  za  asili  ambazo  ili zitoe  matokeo  mazuri  ni  lazima  zichemshwe  kwenye  moto mdogo,  nyingine  lazima  zichemshwe  kwenye moto  mkali, wakati  nyingine  zinatakiwa  kulowekwa  tu  kwenye  maji  ya  uvuguvugu  au  ya  baridi,nyingine  zinatakiwa  kukorogwa  kwenye  maji  ya  moto  na  kunywewa  papo hapo, nyingine  zinatakiwa   kulowekwa  kwenye  maji  usiku  kucha  kabla  ya  kuchemshwa  au  kunywewa  bila  kuchemshwa.

Dawa  za  asili  nyingine  zinatumika  kwa  kulamba  tu, nyingine  zinatumika  kunusa  wakati  nyingine  zinatumika  kwa  kutafuna  au  kupaka.

Dawa  nyingine   zinatakiwa  kutumiwa zikiwa  mbichi. Kama  ni  kupikwa  basi  zinatakiwa  kupikwa  zikiwa  mbichi  ( fresh ).

Hizi  mara  nyingi  ni  dawa ambazo  hutumika kwa wengi  kama  chakula.

Wakati  dawa nyingine  hutakiwa  kukaushwa  kwanza  kabla  ya  kuanza  kutumika.

Hapo hapo  kwenye  kukausha , mtumiaji  wa  dawa  unatakiwa  kujua  njia  sahihi  ya  kukausha  dawa  zako.

Kujua  njia  sahihi  kutakuhakikishia  kutumia  dawa  katika  namna  ambayo  itakuwa  na  manufaa  kwako, kwa  sababu   zipo  dawa  ama  vyakula  dawa  vingine, havitakiwi  kukauka  kwa  mwanga  wa jua wakati   dawa  nyingine  ni lazima  zikaushwe ama zianikwe  kwenye  mwanga  wa  jua.

Mfano  ipo dawa  moja  ya  asili  ina  nguvu sana  na  ina  uwezo  wa  kutibu  maradhi  mengi  sana.

Dawa  hii  hutakiwa  kutumika  ikiwa  imekaukau lakini  haitakiwi kukaushwa kwa  kutumia  mwanga  wa jua  kwa sababu  mwanga  wa  jua  huuwa  virutubisho  vilivyomo  ndani  ya  dawa  hiyo.

Ili dawa  hii iweze  kuwa  na  manufaa  inatakiwa  kukauka  kwa joto  tu  bila  kupata mwanga  wa  jua. 

Dawa  hii  hukaushiwa  ndani  bila  kupata  mwanga  wa  jua, na pindi  inapokauka, hutoa  matokeo mazuri sana  kwa mtu  anae  itumia.

Mfano  mwingine  ni   dawa  ambazo  lazima  zikaushiwe  kwenye  mwanga  wa  jua kabla  ya  kuanza  kutumika.

Zipo  dawa  za  asili  ambazo  ili  zitumike  kwa  manufaa, lazima  zipikwe  ama kuvundikwa kwenye  wine  nyekundu  tamu  (  Sweet  Red  Wine  )

Zipo  dawa  za  asili  ambazo ni  lazima  zipikwe  kwenye  juisi  ya  miwa.
Zipo dawa  ambazo  hutakiwa  kupikwa  pamoja na  samli, jibini  au  nta.

Zipo  dawa  nyingine za  asili , ili ziweze  kuwa  na  manufaa   kwa mtumiaji  ni  lazima zitwangwe  kwanza  kabla ya   kuchemshwa    au  kulowekwa  kwenye  maji  au  kutengeneza  juisi.

Mfano  mzuri  ni  mchaichai.Huu  ni mmea  wenye  uwezo  wa  kutibu  maradhi  mengi sana lakini  watu wengi  wanashindwa  kunufaika  na  faida  za  mmea  huu  kwa  sababu  ya  kushindwa  kujua  njia  sahihi  za  kuuandaa  mmea  huu.

Mmea  wa  mchaichai   unatakiwa kutwangwa  au kusagwa  kwa  blenda   kwanza  kabla  ya  kuchemshwa  kwenye  maji  kwa  ajili  ya  matumizi  ya  dawa.

Mfano  mwingine  ni  matembele.  Matembele  yanasifika  kuwa  na uwezo  mkubwa sana  wa kuongeza  damu  mwilini  hususani kwa  wanawake  wajawazito, lakini  ili  mmea  huu  huweze  kuwa  na mafuaa  hayo  ni lazima  utwangwe  kwanza    au  usagwe  kwa  blenda  kabla  ya  kuuchemsha.

Kwa  mahitaji  ya  dawa  mbalimbali za  asili fika  katika  duka  la  kuuza  dawa  za  asili  la  NEEMA HERBALIST.
Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO NATIONAL  HOUSING, nyuma ya  jengo la UBUNGO PLAZA.

AU  WASILIANA  NASI  KWA  SIMU NAMBA 
0766 538384
Na  kwa  Makala  kuhusu  tiba  mbalimbali za  asili, tutembelee  kila  siku : www.neemaherbalist.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...