Ukerewe. Mlinzi wa Kampuni ya
Ulinzi ya Jitegemee ya Mwanza, Stephano Imbuhu (39), amejiua kwa kujipiga
risasi kutokana na kile kinachodaiwa mgogoro katika ndoa.
Habari zilizopatikana kutoka kituo chake cha kazi, Kisiwani Kweru
Mto, Ukerewe zinadai kuwa marehemu alijiua juzi saa tisa alasiri baada ya
mkewe, Edita Makalanga akiwa na watoto wao wawili kuondoka nyumbani na kwenda kusikojulikana.
Inadaiwa kuwa, Edita aliondoka nyumbani bila kumtaarifu mume wake
na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi haikupatikana.
Majirani walidai kuwa uamuzi wa mke kuondoka bila kutoa taarifa,
ulimchukiza marehemu na kuamua kujipiga risasi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo alithibitisha kutokea tukio hilo.
Alisema marehemu alijiua kwa kutumia bunduki aina ya Rifle yenye
namba 70526 mali ya kampuni aliyokuwa akifanya kazi.
Kamanda Mkumbo alisema marehemu alijipiga risasi kifuani akiwa
chumbani.
“Kabla ya kujiua, aliandika ujumbe kupitia simu yake ya mkononi akieleza kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na mgogoro wa ndoa na mke wake,” alisema Kamanda Mkumbo.
“Kabla ya kujiua, aliandika ujumbe kupitia simu yake ya mkononi akieleza kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na mgogoro wa ndoa na mke wake,” alisema Kamanda Mkumbo.
Alisema ujumbe wa kuamua kujiua aliutuma kwa baba mkwe wake, baadhi
ya ndugu zake na rafiki yake.
Kamanda Mkumbo alisema ujumbe huo ulikutwa kwenye simu yake ya
mkononi.
Ujumbe huo uliandikwa hivi: “Baba mkwe wangu,
sistahili kuishi duniani kwa sababu ya mwanao kanifanya mimi kama mwanamke na yeye kuwa mwanaume. Naomba
uhudhurie mazishi yangu na usiwaache wanangu, Gadina na Majid. Asante.”
Mlinzi huyo alikuwa akilinda mali za mfanyabishara mmoja kutoka
Kisiwa cha Kweru Mto, aliyetajwa kwa jina la Osward Mwandumisya.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ukerewe, Ally Mkalipa alisema
amesikitishwa na tukio hilo na kuwataka wananchi kuomba msaada wa ushauri
wanapokumbana na matatizo ya kifamilia.
“Kwenye maisha kuna matatizo mengi tunakumbana
nayo, mengine yako nje ya uwezo, lakini hata hivyo hakuna sababu ya kujiua.
Nawaomba wananchi kutafuta ushauri wanapokabiliwa na matatizo mbalimbali,” alisema Kamanda Mkalipa.
CREDIT :
MWANANCHI NEWSPAPER
MAKALA NYINGINEZO
JINSI KISUKARI KINAVYO SABABISHA MARADHI YA NGUVU ZA KIUME
JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA NA JINSI UNAVYO WEZA KUKIONDOA KWA TIBA ASILIA
JINSI PUNYETO INAVYO SABABISHA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
IJUE SAYANSI YA NGUVU ZA KIUME
UHUSIANO KATI YA UNENE ULIO ZIDI NA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZAP KIUME
KISA UGONJWA WA KISUKARI MWANAMKE AMKIMBIA MUMEWE WA NDOA NA KWENDA KUISHI NA JIRANI
KUTANA NA MWANAMKE AIYE JITOLEA KUMTIBU MUMEWE MARADHI YA AJABU
PUNYETO ILISABABISHA NINUSURIKE KWENDA JELA
Comments
Post a Comment