Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Balozi Amina Salum
Ali amesema sababu kubwa ya wanawake wengi kubakwa wakiwa wanaokota karafuu ni
kutokana na kujipamba vizuri wakati wakifanya kazi hiyo shambani.
Balozi Amina amesema hayo leo Jumatatu katika kikao cha Baraza la
Wawakilishi kinachoendelea Zanzibar wakati akijibu swali la nyongeza la
Mwakilishi wa Kikwajuni, Nassor Salum Ali.
Mwakilishi huyo alitaka kujua kuna sababu gani za msingi kwa
Serikali kupiga marufuku uokotaji wa karafuu za mpeta wakati zilikuwa
zinawaingizia fedha watu hasa wanawake.
Akijibu swali hilo Balozi Amina amesema kutokana na malalamiko
mengi ya wanajamii kwa kuibuka matendo ya ubakaji kwa wanawake wanaokota
karafuu za mpeta ndio maana kwa makusudi Serikali imeamua kupiga marufuku
uokotaji wa aina hiyo.
“Utakuta wanawake wanatoka nyumbani kwao
wakielekea Mkoani kuokota karafuu za mpeta huku wakiwa wamejipamba, hali ambayo
huwa ni kishawishi kikubwa kwa wanaume kuwafanyia vitendo viovu vikiwamo vya
ubakaji, hivyo upigaji marufuku huu tunaamini utasaidia sana kurudisha heshima
za wanawake,” amesema.
Amesema kutokana na agizo hilo Serikali imeandaa adhabu kali kwa
yule atakayepigana na agizo hilo kwa kuchukuliwa hatua za kisheria.
CREDIT : MWANANCHI NEWSPAPER
MAKALA NYINGINEZO
JINSI KISUKARI KINAVYO SABABISHA MARADHI YA NGUVU ZA KIUME
JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA NA JINSI UNAVYO WEZA KUKIONDOA KWA TIBA ASILIA
JINSI PUNYETO INAVYO SABABISHA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
IJUE SAYANSI YA NGUVU ZA KIUME
UHUSIANO KATI YA UNENE ULIO ZIDI NA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZAP KIUME
KISA UGONJWA WA KISUKARI MWANAMKE AMKIMBIA MUMEWE WA NDOA NA KWENDA KUISHI NA JIRANI
KUTANA NA MWANAMKE AIYE JITOLEA KUMTIBU MUMEWE MARADHI YA AJABU
PUNYETO ILISABABISHA NINUSURIKE KWENDA JELA
Comments
Post a Comment