Hivi ulishawahi kujiuliza matunda yapi yawe rafiki kwako na familia
yako? Jibu usinipe ila bado hujachelewa naomba uanze sasa kwa kula Stafeli
kwani ni tunda lenye faida nyingi mwilini kama yalivyomatunda mengine. Asilimia
12 ya tunda hilo lina sukari ya asili ambayo ni salama kwa mlaji na kwamba ni
chanzo kikuu cha Vitamini C, madini ya chuma na Niacin Riboflavin.
Stafeli hustawi katika ukanda wa kitropiki na tunda hilo hufanana
kidogo na tunda la topetope ambalo nalo lina kiasi kikubwa cha sukari ya asili.
Tunda hili hutibu matatizo ya mfumo wa fahamu, shinikizo la damu,
msongo wa mawazo na saratani.
Utafiti uliowahi kufanyika unaonyesha juisi yake pia hutibu
saratani kwa haraka, kwa sababu inanguvu mara 10,000 zaidi ya tiba ya mionzi
katika kuzuia seli za saratani.
Hata hivyo, wagonjwa wa saratani wanapokuwa katika tiba ya
hospitalini wanashauriwa kula tunda hilo kwa ajili ya kupunguza makali ya dawa
za saratani anazotumia pamoja na maumivu.
Stafeli linakirutubisho aina ya Annona Muricata kinachoweza kukabiliana
na maradhi ya saratani katika mwili wa binadamu.
Mbali ya kuwa ni chanzo kikubwa cha vitamini, tunda hilo hutibu
maumivu ya nyama za mgongo, hurekebisha usawa wa kiasi cha damu na sukari
mwilini na huongeza kinga ya mwili.
Faida nyingine hudhibiti ukuaji wa bakteria, virusi, vijidudu
nyemelezi na hutibu majipu na uvimbe, huongeza stamina ya mwili na kurahisisha
kupona haraka na hufukuza chawa.
Majani yake hutumika kama chai.
Majani hayo hutibu pia kuharisha damu, mafua na husaidia mfumo wa
umeng’enyaji wa chakula.
yanatumika pia kutibu maumivu ya mishipa. Mtumiaji unatakiwa
kuyasaga mpaka yalainike kisha yapashe jikoni na kupaka katika eneo la mshipa
wenye maumivu.
CREDIT :
MWANANCHI NEWSPAPER
MAKALA NYINGINEZO
JINSI KISUKARI KINAVYO SABABISHA MARADHI YA NGUVU ZA KIUME
JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA NA JINSI UNAVYO WEZA KUKIONDOA KWA TIBA ASILIA
JINSI PUNYETO INAVYO SABABISHA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
IJUE SAYANSI YA NGUVU ZA KIUME
UHUSIANO KATI YA UNENE ULIO ZIDI NA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZAP KIUME
KISA UGONJWA WA KISUKARI MWANAMKE AMKIMBIA MUMEWE WA NDOA NA KWENDA KUISHI NA JIRANI
KUTANA NA MWANAMKE AIYE JITOLEA KUMTIBU MUMEWE MARADHI YA AJABU
PUNYETO ILISABABISHA NINUSURIKE KWENDA JELA
Comments
Post a Comment