Inaaminika kuwa asilimia 1 hadi 3 ya idadi ya watu hawana hisia
zozote za kingono.
Kwa miaka kadhaa Stacey alishindwa kufumbua fumbo la ni kwa nini
hakutaka kushiriki ngono na mtu yeyete hata mumewe.
Kama anavyoelezea hapa ni daktari wake aliyemwambia ukweli.
Kwa muda mrefu sana nilidhani nina matatizo ya kiakili na
kiumbile.
Nilihisi kwamba sio jambo la kawaida kutoshiriki ngono.
Marafiki zangu wangezungumza kuhsu marafiki zao wa kiume ama
hata watu maarufu ambao wangependa kushiriki nao ngono lakini mimi sikuwa na
mtu yeyote akilini ambaye nahisi tungeshiriki naye ngono.
Wakati nilipokuwa katika miaka yangu ya ishirini nilianza kuona
tofauti niliyo nayo , lakini singeweza kuambia mtu yeyote kwa sababu yalikuwa
mawazo, watanifikiria mimi sio mtu wa kawaida, kwa hivyo nikaamua kunyamaza.
Kutokuwa na hisia zozote za ngono ACE sio jambo la kawaida
ijapokuwa mara nyengine uhisi kuvutiwa ki-mahaba.
Nilikutana na mpenzi wangu ambaye sasa ni mume wangu wakati
nilipokuwa na miaka 19, na sikujua maana ya kutokuwa na hisia za kushiriki
ngono, hivyobasi nilidhani niko nyuma na kwamba sielewi mambo.
Nilikuwa nikifikiria kwamba nampenda sana mwanamume huyu na
iwapo atanichumbia nitakubali asiliia 100 kwa sababu najua ningependa kutumikia
maisha yangu yote naye, lakini kwa nini sitaki kushiriki naye ngono? ni jambo
la kushangaza.
Tulizuru maeneo mbali mbali na aliniambia kwamba yeye atasubiri
hadi siku ninayohisi kushiriki ngono naye.
Alinisaidia sana na hakutaka kunilazimisha kufanya kitu ambacho
sikupendelea.
Nilifanya makosa makubwa kwa kutafuta katika mtandao sababu za
kimatibabu ambazo husababisha mtu kutokuwa na hisia za kushiriki tendo la
ngono.
Maadili ya kijamii yanaelezea kwamba ngono na watoto ndio sababu
ya ndoa na marafiki zangu wote walikuwa wakiolewa na kupata watoto.
Nilifikiri mungu wangu kuna hili tarajio kwamba ninafaa kushiriki
tendo la ngono na mumewe wangu ili kupata watoto.
Nilianza kuota ndoto za ajabu kwamba mumewe wangu huenda
ataniwacha kwa msichana mwengine anayefanana nami lakini ambaye atakubali
kulala naye na ikafikia kiwango ambacho wasiwasi wangu nilishindwa kuuvumilia.
Nilifikiria, wajua nini? ni muhimu kusuluhisha swala hilo ,
nilitaka kujua ni nini kilichokuwa kikiendelea, wakati huo nikiwa kati ya miaka
27 ama 28.
Nilifanya makosa ya kufanya utafiti katika mtandao na hayo
yalikuwa makosa makubwa sana, kulikuwa na mambo mengi ambayo yalikuwa ya
kawaida kama vile homoni zilizokuwa zikitoweka mara kwa mara , lakini kile
ambacho niliiona ni kuwa na uvimbe katika ubongo.
Nilisema, mungu wangu nitafariki kutokana na uvimbe katika
ubongo.
Nilienda kwa daktari wangu na kusema, tazama ni hatari?,
nitafariki?
Aliniambia, tulia una tatizo la kutokuwa na hisia za kushiriki
ngono.
Nilisema, ni nini hiyo? nini?
Sijawahi kuhisi kile watu wengi hutaja kuwa na hisia za kingono.
Hivyobasi alinielekeza katika mitandao na hapo ndipo
nilipokutana na watu kama mimi.nilifurahi.
Sikuwahi kusikia kwamba kuna watu wasiokuwa na hisia za ngono.
Nilifanya utafiti zaidi na kuanza kujihisi kawaida, hivyobasi
nilizungumza na mume wangu kuhusu swala hilo.
Na alisema, nilidhani kwamba kila kitu kilikuwa sawa .
Amekuwa mtu mzuri sana, amekuwa akinielewa sana.Baadhi ya watu
walio na tatizo kama langu walikuwa na haya ya kusema:
Nina umri wa miaka 60 na sijawahi kukutana na mtu mwengine
ambaye yuko kama mimi. Sijawahi kusikia hadharani .
Nilipotambua kwamba sina hisia za kushiriki ngono nilizungumza
na watu kadhaa na huku wengine wakijitokeza na kuliangazia swala hili kwa uwazi
nimepata majibu mabaya sana.
Kundi moja la wachezaji wenzagu katika chuo kikuu waliamua
kunipangia kwenda kujiburidisha usiku kwa lengo la kutaka nishiriki ngono
walipogundua kwamba sijashiriki ngono bila kujali kwamba nilikuwa na tatizo.
Kuna watu wengi wasio na hisia za ngono ambao wanapoanza
uhusiano na mtu mwengine wanashiriki ngono na wanaendelea kama kawaida , lakini
kwangu mimi kila wakati ninapokaribi kufanya tendo hilo mwili wangu unakataa
kabisa.
Ni utoto mwingi na watu ninapowaambia hushangaa na kuniuliza ni
vipi unaweza kupata watoto.
Ijapokuwa kuna njia nyingi za kupata watoto iwapo ninataka, ni
swala ambalo linawezekana.
Nimegundua tatizo lango kwa miaka mitatu sasa.
Nasherehekea kuwa mtu mwenye tatizo hili, nafurahia na napenda
kuzungumza na wengine ili watu zaidi kuelewa na sio kuwahukumu watu wasio na
hisia za kufanya ngono.
Nadhani iwapo ningejua kwamba nina tatizo hili nilipokuwa na
miaka 18 ama 19 nadhani afya yangu ya kiakili ingekuwa bora wakati mwingi wa
miaka yangu ya 20.
La kushangaza zaidi ni kwamba wakati kabla ya kugundua tatizo
langu mume wangu alikuwa akiniita Stace Ace
CREDIT :
BBC SWAHILI
Comments
Post a Comment