Bamia za kukaanga na mafuta,Hapo naongeza na nyanya. Mimi hupenda na Ugali. Bamia za Kuchemsha[Mrenda] Waungwana hivi ni kwanini mboga hii ya Bamia Wanaume wengi Hawali/Hawaipendi? Jee wewe Unapenda Bamia na Unapikaje?Wengine wanatia na nyanyachungu,Kwenye Samaki Wakavu na....Jee Unaweza kula Bamia na Ugali wa Muhogo? Karibuni LEO NDIO NIMEJUA BAMIA KWA KIINGEREZA INAITWA ''LADIES FINGER'' Nilijua inaitwa okra lakini kumbe marekani ndio wanaita hivyo ila kwa kiingereza Ladies finger. Kwa nini ziliitwa ladies finger?inasemekana ni kwasababu ya umbo lake lilivyo kama vidole vywa mwanamke. Bamia hukatwa na kupikwa kwa mapishi tofauti tofauti Ukaipika kwa urefu kwa maana ya kukata kikonyo na ncha yakekisha kuiunga na nazi . Hizi zimewekwa tayari kwa kuokwa.Zimepasuliwa katikati halafu kwa ndani ukawekwa mchanganyiko wa vitunguu maji,jeera,coriender,pilipili ya unga,chumvi,mafuta ya kula,tangawizi na nazi vikachanganywa na kutiwa humo.Hii ni...