Nianze lini kumpa mtoto
wangu maji na nimpe kiasi gani ni swali ambalo
kinamama wengi wenye watoto wachanga hujiuliza.
Mara Nyingi sana
nimesikia kinamama wakijadiliana juu ya hili na kubadilishana uzoefu.Ingawa
nimesikia wengi wakiliongelea kinachoshangaza ni kwamba sijawahi kusikia jibu
moja ambalo naweza sema ndilo jibu sahihi au laa basi kuambiwa kwamba hili
ndilo jibu sahihi na kupewa sababu za kuridhisha .
Kwakua lengo langu ni
kukuza mapishi nyumbani na kuhakikisha afya ya familia iko vizuri,niliamua
kufanya Utafiti binafsi kwa kusoma vitabu,majarida na kuongea na baadhi
ya madakitari wa watoto ninaowafahamu.Si kuishia hapo tu,nimeongea na akina
mama waliolea watoto miaka yazamani na wanaolea watoto hivi sasa.Na haya ndio
majibu niliyopata.
Majibu kutoka taasisi za
afya.
Taarifa za wataalam wa
afya kutoka kwenye taasisi zinazoaminika duniani kama World health
organization na Association of American Pedietrisions,zinasema Mtoto mdogo kati
ya siku moja adi miezi sita(1-6) hatakiwi kupewa maji wala chakula
kingine chochote zaidi ya maziwa ya mama au maziwa maalum ya watoto(baby
formula) au maziwa ya Ngombe.
Wameelezea kwamba kiasi
cha maji mtoto anachopata kwenye maziwa kinatosha kabisa .Kumpa mtoto maji si
salama kwani yataharibu uwezo wa mwili wa mtoto kunyonya virutubisho kutoka
kwenye maziwa.Maji pia yatafanya mtoto ashibe na ashindwe kunywa maziwa kwa kiasi
kinachohitajika,Mbaya zaidi ni kwamba maji mengi kwa mtoto wakati mwingine
huweza kuleta hali iitwayo water intoxication,hali hii huweza kumfanya mtoto
azimie na wakati mwingine kuingia katika coma.Hali hii huja pale ambapo
wingi wa maji mwilini utapunguza kiasi cha sodium mwilini(low sodium
concentration).
Taarifa inasema
kwamba,ingawa unaweza kumpa mtoto maji baada ya miezi 6,wanashauri mtoto apewe
maji kidogo na kwa kipimo maalum adi pale atakapo timiza mwaka mmoja ambapo
anaweza kunywa maji kwa kiasi atakacho.
Majibu kutoka kwa
madaktari wetu.
Madktari wanne tofauti
niliyobaatika kuongea nao,majibu yao yalifanana kwa kiasi kikubwa.Kwanza
waliunga mkono taarifa za World health organization(taarifa hapo juu) .Lakini
pili walikua na yao yakuongeza.
Walisema kwamba maziwa ya
mama na formula zinamtosha mtoto endapo tu mtoto huyo anapewa maziwa
yanayomtosha kushiba na yenye virutubisho vyote.Walieleza kwamba kina mama
wengi hawanyonyeshi mtoto adi akashiba.Si kwasababu hawana maziwa au hawataki
bali ni kwasababu hawajui mtoto anaitaji maziwa kiasi gani ili ashibe na
anyonyeshe kwa muda gani ili mtoto apate kiasi hicho cha maziwa.Na kwasababu
wakati mwingine maziwa ya mama yenyewe hayana virutubisho vyakutosha
kwani mama mwenyewe hali, au mwimili wake hauna virutubisho vyakutosha na
wakati mwingine anapungukiwa baadhi ya virutubisho .
Walisema kua hali hii
hufanya maziwa ya mama yasitoshe kabisa kwa mtoto na kulazimu mtoto aanze
kupewa uji mwepesi mapema kabla ya miezi sita ili kufidia lishe yake.Na Pale tu
unapoanza kumpa mtoto chakula zaidi ya maziwa basi ni vyema ukaanza kumpa
maji kwani uji na vyakula kama hivyo huesabika kama vyakula vigumu kwa
mtoto.Moja alisema kwamba endapo mtu analazimika kumpa mtoto uji mapema basi
ni vyema mtoto afikishe angalao miezi minne.
Mwingine alisema
kwamba,moja ya sababu zinazochangia kabisa kuwakataza kina mama kuwapa watoto
maji ni pamoja na uwezekano mkubwa wa mtoto kupata magonjwa kutoka kwenye maji
ya kunywa. Mara nyingi maji hayawi safi na salama.Alinieleza kwamba,magonjwa ya
tumbo yanayoleta kuhara kwa mtoto ni moja kati ya magonjwa yanayosababisha vifo
vya watoto kwa haraka.
Majibu ya Mama aliyelea
watoto miaka ya 60 – 80
Mama huyu aliyeanza kulea
mtoto wake wakwanza mwaka 1967 alikua na haya yakusema.Alisema enzi zile
walikua wanafundishwa namna ya kulisha mtoto kila wanapoenda kliniki.Alisema
Walikua wakipewa karatasi yenye picha za vyakula na majina ya vyakula
hivyo na kuambiwa zaidi ya kunyonyesha ni lazima wawape watoto wao vyakula
hivyo.Wakati mwingine walienda kwenye vikundi vya akinamama na kufundishwa
namna ya kuandaa vyakula hivyo kwaajili ya mtoto.
Alinieleza kua vyakula
hivyo viliwekwa kwa makundi,na kulikua na kundi lenye maji ya kunywa na maji ya
matunda.Hivyo wao waliwapa watoto maji na maji ya matunda kama kadi
ilivyoelekeza,aliniambia kua walikua wakipewa karatasi hizo miezi miwili
baada ya kujifungua.(akimaanisha mtoto akiwa na miezi miwili).
Kwa maana hiyo ,walianza
kuwapa watoto uji,maji na maji ya matunda wakiwa na miezi miwili.
Majibu ya Mama anaelea
watoto hivi leo.
Niliongea na mama wawili
tofauti,mmoja anawatoto wanne na mwingine ana wawili.
Mwenye watoto wanne,alisema
watoto wake wote walianza kunywa maji na uji mwepesi wakiwa na miezi
miwili.Alisema kwamba ingawa watoto wake walikunywa maziwa bila shida aliona
wazi kabisa kwamba hawashibi na ndipo alipoamua kuongeza uji mwepesi kwenye
lishe yao.
Alinieleza kwamba huandaa
uji huo na kisha kuuchuja na kuhakikisha ni mwepesi kama maziwa na kisha kumpa
mtoto kwenye chuchu kama anavyompa maziwa.Uji huo huandaliwa kwa maziwa,maji na
unga.
Mwenye watoto wawili alikua
na haya yakusema.Alisema kwamba watoto wake walikunywa maziwa tu adi
walipofikisha miezi 6.Pale alipoona maziwa ya mama hayatoshi aliongeza maziwa
ya ng’ombe ili kuhakikisha mtoto anashiba.
Alinieleza kwamba,ili
kuhakikisha mtoto anakunywa maziwa kwa kipimo sahihi,alikamua maziwa yake
kwakutumia pampu maalum na kuyaweka kwenye chupa ili apime kipimi sahihi.Na
kwakua mtoto wake hushiba vizuri na wataalam husema mtoto asipewe maji basi
hakua na sababu yoyote ya kumpa mtoto maji kabla ya wakati uliothibitishwa.
Mtizamo wangu
Baada ya kukusanya yote
haya na kutafakari ,nimegundua kwamba pale ambapo mtoto anapewa chakula
chochote zaidi ya maziwa basi ni sawa apewe maji kwa kiasi Fulani,kwani
tayari mwili wake unapokea chakula kigumu na huitaji maji zaidi.
Kwa upande mwingine,sioni
sababu ya kumpa mtoto maji endapo anapata maziwa katika kiasi kilicho sahihi
kwa mwili wake na anashiba.kinachonitia wasiwasi ni uwezekano wa mtoto
kupata maziwa yakutosha.
Kwa maisha yetu ya
kitanzania Gharama ya kumlea mtoto kwa kumpa maziwa ya kopo ni kubwa sana
na wazazi wengi hawawezi mudu gharama hizo.Gharama za maziwa ya ng’ombe pia
ziko juu na maziwa niyashida hasa kwenye miji mikubwa hivyo ni ngumu kwa
mwananchi wa kipato cha kawaida na cha chini kufidia lishe ya mtoto kwa
kuongeza maziwa hayo yakununua.Hii humlazimu mzazi kumuanzisha mtoto uji mapema
ili kufidia lishe yake.Jambo linalopelekea mtoto kula chakula kigumu na kunywa
maji akiwa chini ya miezi sita .
Hata hivyo ni vyema kujua
kwamba ingawa kuna kiasi au kipimo Fulani cha maziwa ambacho mtoto anatakiwa
kupewa si kweli kwamba watoto wote hushiba kwa kipimo hicho.Watoto hutofautiana
ukubwa wa mwili kitu ambachi hufanya hata kula yao itofautiane.Kwa mantiki hiyo
basi ni wazi kwamba watoto wa rika moja si lazima wapewe kipimo sawa cha maziwa,tofauti
ya hatua tano juu ya kipimo cha kawaida huruhusiwa.
Ushauri
Nawashauri kina
mama,kuongea na madaktari wa watoto juu ya wakati sahihi wakumpa mtoto maji.Ni
vyema mkalijadili hili kwa pamoja na kuona wakati upi ni sahihi zaidi kumpa
mtoto maji kwa kuzingatia ubora au mapungufu ya afya yake.Kumbuka tu kwamba
ukosefu wa maji mwilini pia huzaa matatizo makubwa ya afya kwa mtoto.
Naamini makala hii
imekupa mwanga juu ya swala hili,na hata utakapoongea na daktari basi unaweza
bishana nae hapa na pale katika kuhakikisha anakupa jibu linaloeleweka.
Busara za Tolly.
Siku zote daktari wa
watoto anapokwambia jambo,jifunze kumuuliza kwanini kakwambia hivyo au kwanini
anaona hivyo.Mfano:Akikwambia usimpe mtoto maji ya adi afikishe miezi
nane.Muuliza: Kwanini?.Hii itakusaidia kuelewa Jambo kwa undani.
MAJI NI
UHAI
Comments
Post a Comment