NAMNA YA KUONDOA ASIDI INAYOSABABISHA KIUNGULIA KWENYE MAHARAGE-Epukana na kiungulia na tumbo kujaa gesi.
Maharage
ni moja ya vyakula ambavyo mimi hukwepa kula nje ya nyumbani ,naweza kula
maharage nje ya nyumbani kwangu endapo tu ninauakika na ambavyo mpishi
kaandaa maharage hayo,kwa maana nyingine nakula kama yameandaliwa na
ndugu,jamaa na marafiki ambao ninauhakika na uandaaji wao.
Hii
yote ni kwasababu maharage yasipoandaliwa vizuri hunipa kiungulia kikali sana
kwa muda mrefu na wakati mwingine tumbo hujaa gesi na kuninyima raha.
Maharage
ni chanzo kizuri cha protini daraja B(protini itokanayo na mimea)na Nyuzinyuzi.
Asidi
aina ya Phytic au phytates ipatikanayo kwenye maharage ikutanapo na
madini mwili kama zinc,copper,calcium,magnesium namadini chuma
husababisha tatizo la kiungulia na tumbo kujaa gesi kwa baadhi ya watu,tatizo
hili huwasumbua zaidi wale wasiokula Nyama na vyakula vitokanavyo na
wanyama(vegeterians)kwani vyakula vyao hua na asidi nyingi ya
phytic.
Tafiti
zilizofanywa na American Dietetic Association zinaonyesha kwamba huwezi toa
asidi yote ya phytic kwenye maharage ila unaweza kuipunguza kwa kiasi
kikubwa kwa kuloweka maharage kwenye maji.
Wengi
mnaloweka maharage kwenye maji ili kuyalainisha na kufanya yaive haraka wakati
wakupika,Lakini msichojua ni kwamba kuloweka huko hupunguza asidi ya
Hyptic kwenye maharage ambayo ni chanzo cha kiungulia kwa wengi,asidi
hiyo pia hutonesha vidonda vya tumbo na kuleta maumivu makali kwa wale wenye
tatizo la vidonda vya tumbo.
Ulowekaji
wa maharage kwa muda mrefu
Watu
wengi wamezoea kuloweka maharage usiku na kuyapika siku inayofatia,ikimaanisha
yanalowekwa kati ya masaa manane hadi kumi na nane.Ingawa kuloweka huku
kumezoeleka kwa wengi.
Tafiti
zinaonyesha kwamba,njia hii ya ulowekaji wa maharage ni hatari sana kwa
afya kwani hutoa nafasi, mazingira sahihi na muda mrefu kwa
vijidudu viletavyo magonjwa vipatikanavyo kwenye maharage kuzaliana
na kukua .
Ingawa
maharage hupikwa kwa muda mrefu na kwa moto mkali bado haitoshi kuuwa vijidudu
vya aina yote,bakteria watengenezao sumu au spore mara nyingi hubakia hai na
huweza kua chanzo cha magonjwa kwa mlaji wa maharage hayo.Ukiamua kutumia
njia hii,basi loweka maharage na uyaweke ndani ya friji ili kupunguza uwezekano
wa vijidudu hao kuzaliana kwenye maharage.
Ulowekaji
wa maharage kwa muda mfupi-Njia iliyo bora
Kuloweka
maharage kwa muda mfupi ni njia nzuri na bora zaidi ya kupunguza asidi ya
phytic kwenye maharage,kwani huipunguza kwa kiwango kikubwa na kwa haraka zaidi
kuliko njia ya kuloweka maharage kwa muda mrefu.
Njia
hii fupi kwa upande mwingine haitoi nafasi ya vijidudu viletavyo magonjwa
kuzaliana kwenye maharage,na huokoa muda kwani huchukua muda mfupi.
Ulowekaji
huu huchukua kati ya saa moja adi manne na si zaidi,ni uamuzi wa mpishi
kuchagua aloweke masaa mangapi,ata hivyo ni vyema kujua kwamba ukiloweka kwa
masaa manne utatoa kiasi kikubwa cha phytic kuliko ukiloweka kwa saa
moja.
Njia.
1.Pima
kiasi cha maharage unachotaka kuandaa/kupika,mfano:vikombe vinne.(nashauri
utumie kikombe kupima)kariri idadi ya vikombe ulivyopima
2.Chambua
maharage ili kuondoa maharage mabovu,mawe na uchafu mwingine wowote
3.Osha
maharage,adi yawe safi.
4.Kwa
kutumia kikombe ulichopimia maharage ,pima maji mara mbili ya kipimo cha
maharage na uweke kando.mfano:kwakua tumepima maharage vikombe vinne,tutapima
maji vikombe nane.(vikombe vya maji,mara mbili ya vikombe vya maharage)
5.Katika
sufuria weka maharage na kisha ongeza maji uliyopima
6.Bandika
maharage jikoni yachemke kwa dakika mbili tu.Hesabu dakika mbili kuanzia
pale yanapoanza kutokota na sio dakika mbili kuanzia ulipoyabandika
jikoni.Epua jikoni baada ya dakika hizo kuisha.
7.Acha
kwa kati ya saa moja adi manne(kutokana na muda ulionao)
Muonekano
wa maharage baada ya masaa manne
8.Chuja
maji yote kwenye maharage.
Maji
yaliyochujwa kwenye maharage.maji haya yamebeba phytic iliyotoka kwenye
maharage.
9.weka
maharage kwenye sufuria, ongeza maji ,bandika jikoni kisha chemsha adi
maharage yaive.
Maharage
yaliyoiva,baada ya kuchemshwa
Baada
ya kuivisha maharage ,unaweza kuyapika au kuyaunga katika namna upendayo.
Maelezo
ya ziada.
Ingawa
njia hii hupunguza phytic kwa kiasi kikubwa sana na hutosha
kufanya mtu asipate kiungulia au tumbo kujaa gesi,kuna wale wenzangu ambao hata
iyo hyptic kidogo sana iliyobaki kwenye maharage inatosha kuwapa kiungulia.Ipo
namna ya kukata nguvu ya hiyo phytic kidogo iliyobaki na kufanya maharage yawe
mazuri zaidi.Nitakueleza hilo katika makala ijayo.
Ipe
familia yako kilicho bora zaidi.
CREDIT : www.tollyzkitchen.wordpress.com
Comments
Post a Comment