Wadau hii,
nimeitoa facebook, naona si vibaya
kama nita i-share
hapa ili nanyi
mpate kuisoma :
Mwanamke mjane kapiga simu redio moja ya Injili kuomba msaada
kwenye kipindi cha "Saidia Wajane na Yatima". Kuna tajiri mmoja
ambaye haamini kama Mungu yupo na anamuamini shetani akawa anasikiliza hicho
kipindi. Mama akasema alipo, tajiri akamwita msaidizi wake akamwambia nunua
vyakula mpelekee huyu mwanamke, akamtajia mtaa na namba ya simu. Akamwambia
ukifika mwambie huu msaada umetolewa na Ibilisi.
Msaidizi wa tajiri akanunua vile vyakula akapeleka. Alipofika akampa yule mwanamke, mwanamke akapokea; wakati anaingia ndani yule msaidizi wa tajiri akamuuliza: hutaki kujua huu msaada umetolewa na nani?
Mwanamke akamjibu; hapana. Mungu akishatoa amri hata ibilisi huwa anatii.

Comments
Post a Comment