Giligiliani Mboga. |
Giligiliani
ni kiungo cha kawaida sana,wengi tunakitumia jikoni kwenye mapishi
mbalimbali,Kinaharufu nzuri na ladha ya uchachu kwa mbali.Majani na mbegu za
giligiliani vyote hutumika kama viungo jikoni.
Giligiliani
inawingi wa Vitamini A, B6, C,B12,pia ina wingi wa madini chuma(iron),Calcium
na Magnesium
Giligiliani
inasifika kwakua dawa na kinga ya magonjwa mengi.Historia inaonyesha kwamba
Kiungo hiki kilitumika kama dawa tangu enzi za kale nchini Egypt.Hata
hivyo,tafiti za kisayansi za karne hii ya 21 zinathibitisha taarifa hizi
Giligiliani Mbegu |
Ni
vyema kujua kwamba tunaposema chakula Fulani ni dawa,basi maana yake ni kwamba
chakula hicho kinavirutubisho Fulani ambavyo huweza kukabiliana na ugonjwa
Fulani au laa kuupa mwili uwezo wa kukabiliana na kujikinga na ugonjwa Fulani
na si vinginevyo.
Hizi ni baadhi ya faida za giligiliani katika afya :
1.
Inawezesha
usagaji mzuri wa chakula mwilini,hutuliza tumbo na huondoa gesi
kwenye utumbo mwembamba ambayo mara nyingi husababishwa
na vyakula tunavyokula hivyo hupunguza utoaji gesi chafu (kunyampa) kwa
kiasi kikubwa sana
2.
Inazuia
magojwa ya tumbo yasabaishwayo na bacteria aina ya Salmonella.moja ya magonjwa
haya ni kuumwa tumbo na kuhara.
3.
Inazuia
Ugonjwa wa UTI.Yaani Urinary tract infection
4.
Inazui
kutapika na hali ya kuvurugika tumbo
5.
Inaondoa
gesi tumboni
6.
Inashusha
sukari kwenye damu.(lower blood sugar)
7.
Inapunguza
cholesterol mbaya mwilin
8.
Chanzo
kizuri cha nyuzi nyuzi zinazoitajika mwilini ili kuwezesha usagaji mzuri wa
chakula (Dietary fiber)
9.
Inawafaa
sana wanawake ambao hupata hedhi nzito
10.
Inaondoa
maumivu,muwasho,na uvumbe (anti inflammatory)
11.
Huondoa
chunusi na madoa kwenye ngozi
Unaweza
kuandaa giligiliani katika njia mbalimbali ili kuitumia kama dawa
- Kuondoa hedhi nzito.chemsha kijiko 1 cha
chai cha mbegu za giligiliani na maji vikombe viwili.Chuja kisha ongeza
sukari kidogo.Kunywa ikiwa yamoto au vuguvugu
- Kuondoa maumivu (Inflamation) chemsha
kijiko kimoja cha chai cha mbegu za giligiliani zilizosagwa na maji
kikombe kimoja.Chuja kisha kunywa ikiwa vuguvugu
- Kushusha
sukari na kushusha cholesterol.Kunywa chai ya giligiliani
(mbegu) mara kwa mara,pia tumia mbegu na majani ya giligiliani kwa wingi
kwenye chakula.
- Ili
kuondoa chunusi na madoa meusi.Twanga au sigina majani ya
giligiliani,chuja au kamua ili kupata maji yake.Pima vijiko vinne vya maji
ya giligiliani kisha changanya na kijiko 1 cha chakula cha manjano(Binzari
manjano).pakaa kwenye ngozi ,acha ikauke kisha osha au nawa na maji
vuguvugu.Onyo:usisugue ngozi
- Kutibu kuhara damu (dysentery).Changanya
vijiko 2 vya chai vya maji ya giligiliani na kikombe kimoja cha maziwa
fresh ambayo hayajatolewa krim
- Chai ya
giligiliani (mbegu) husaidia kuondoa au kutuliza asidi tumboni
Matumizi
ya mara kwa mara ya vyakula ambavyo ni tiba huupa mwili nafasi nzuri ya kuvuna
virutubisho na kupata tiba ya magonjwa mbalimbali.
Ni
vyema kujua kwamba asilimia kubwa ya vyakula na viungo tulivyonavyo majumbani
ni tiba ya magonjwa mbalimbali.Madawa na Tiba nyingi za kisasa pia
hutokana na mimea,virutubisho huvunwa kutoka kwenye mimea na vyakula na
kuchanganywa na Kemikali ili kutoa vidonge na madawa ya magonjwA mbalimbali.
HERI TIBA CHAKULA KULIKO
TIBA DAWA
CREDIT : www.tollyzkitchen.wordpress.com
Comments
Post a Comment