Sigara |
JINSI YA KUACHA SIGARA KWA TIBA ASILIA
Mwaka mpya wa 2014 ndio umeanza hivyo. Je moja kati ya malengo yako ya mwaka huu, ni kuacha kuvuta sigara ? Kama jibu ni ndio, umepanga kutumia njia gani ili kutimiza lengo lako hilo?
Umepanga kutumia dawa za kizungu zilizo tengenezwa kwa kemikali kama vile Nicotine Replacement Products au Cold Turkey ?
Umepanga kutumia dawa za asili kama vile Kudzu ama Mkataasigara ?
Au utaweka nadhiri ya kuachana kabisa na suala la uvutaji sigara?
Uvutaji wa sigara unachukuliwa kama moja wapo kati ya vyanzo vikuu vya vifo duniani.
Kitu kizuri kuhusu kuacha sigara, ni kwamba, unaweza kuacha sigara wakati wowote ule, haijalishi umekuwa ukivuta sigara kwa muda mrefu kiasi gani kwani tafiti mbalimbali za kisayansi zina eleza kuwa, pindi tu utakapo acha kuvuta sigara, mapafu yako yataanza ku repair athari zilizo sababishwa na uvutaji wa sigara na hatimaye kurudi katika hali yake ya kawaida kana kwamba haukuwahi kujihusisha na uvutaji wa sigara.
Zipo njia mbalimbali za kusaidia kuachana na uvutaji wa sigara zikiwemo njia za matumizi ya dawa za kizungu na zile za asili.
Kama unataka kuachana na matumizi ya sigara kwa njia za asili, tumia vitu vifuatavyo :
1. Mbegu za Oti
Mbegu za Oti zina kiasi kikubwa sana cha fibre, omega-3 fatty acids, madini ya Potassium na folate.
Utumiaji wa mbegu za Oti utasaidia katika kupunguza kiasi cha kolestrol mbaya pamoja na kusafisha arteries, jambo linalo saidia kupunguza uwezekano wa kushambuliwa na magonjwa ya moyo.
Vile vile, mbegu za Oti zina kemikali zijulikanazo kama Avenathramides ambazo zinasaidia kupunguza stress, kuimarisha mfumo wa neva, na kupambana na shinikizo la damu.
Faida zote hizi ni muhimu sana kwa wavutaji sigara ambao wapo katika hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa ya moyo.
Utumiaji wa mbegu za Oti unaweza kumsaidia moja kwa moja mvuta sigara kuacha kuvuta tena kwani unamsaidia mtumiaji kutokuwa na hamu ya kuvuta sigara.
2. PILIPILI KICHAA
Utumiaji wa pilipili kichaa ni dawa nzuri sana itakayo kusaidia kuachana na uvutaji sigara.
Pilipili inasaidia kuusafisha mfumo wa upumuajina kuufanya usiendelee kuwa sensitive na addictive na tumbaku na hivyo kukusaidia kuondoa kiu ya kuvuta sigara.
Unashauriwa kutumia walau pilipili kichaa moja kwa siku.
Unaweza kutumia kwenye chakula au kwa kuila nzima nzima.
Ili kupata matokeo ya haraka na uhakika zaidi, chukua pilipili kichaa, ikate kate katika vipande vidogo vidogo, kisha iweke kwenye glasi ya maji ya moto, koroga na kunywa.
Fanya hivyo mara moja kwa siku kwa muda wa siku ishirini na moja, na kwa hakika, utaachana kabisa na utumiaji wa sigara.
3. GINSENG : Mmea wa Ginseng umethibitishwa kisayansi kuwa na uwezo wa kupambana na kemikali iitwayo Neurotransmitter Dopamine ambayo inasababishwa na Nicotine.
Dopamine ndio inayo mfanya mtu ajisikie raha baada ya kuvuta sigara na kumfanya kuwa addicted na nicotine.
Kijiko kimoja cha chai cha unga wa Ginseng kwa muda wa siku ishirini na moja , kitakusaidia kuachana na uvutaji wa sigara.
4. St. John’s Wort : Mmea huu hutumika zaidi katika kutibu mshuko wa moyo, hata hivyo imethibitika kisayansi kuwa, mmea wa St. John’s Wort una uwezo mkubwa sana wa kuwasaidia watu kuacha kuvuta sigara.
Katika utafiti mmoja, watu 24 wanao vuta sigara moja au zaidi kwa siku, walipatiwa dawa hii mara mbili kwa siku, pamoja ushauri nasaha. Baada ya wiki kumi na mbili, watu 9 kati yao walifanikiwa kuacha sigara.
5. HERBAL CIGARETTES
Herbal Cigarrettes zinaweza kutumika kama mbadala wa sigara za kawaida. Herbal cigarettes hazina kemikali kali kama ilivyo kwa sigara za kawaida.
Faida kubwa ya Herbal Cigarettes ni kwamba hazi kufanyi uwe addicted.
Herbal Cigarettes hazina Nicotine. Zinatengenezwa kwa kutumia mimea kama vile mint ( mnanaa ), mdalasini na karafuu.
6. Lobelia : Matumizi ya mmea huu humsaidia mtu aliye topea kwenye uvutaji wa sigara kuweza kuachana na tabia hiyo hatarishi kwa afya yake.
7. Hyssop : Matumizi ya mmea huu humsaidia mtu aliye topea kwenye uvutaji wa sigara kuweza kuachana na tabia hiyo hatarishi kwa afya yake
8. Valerian : Matumizi ya mmea huu humsaidia mtu aliye topea kwenye uvutaji wa sigara kuweza kuachana na tabia hiyo hatarishi kwa afya yake
NINI KIFANYIKE BAADA YA KUFANIKIWA KUACHA KUVUTA SIGARA.
Utakapo fanikiwa kuachana na uvutaji wa sigara, ni muhimu ukaanza kufanya jitihada za kujitibu athari ambazo umezipata kutoka na uvutaji wa sigara.
Unaweza kujitibu athari ulizo zipata kutokana na uvutaji wa sigara kwa kufanya diet maalumu, mazoezi , meditation na kulala vizuri. Uvutaji wa sigara huharibu Vitamin C mwilini, na Vitamini C ni muhimu sana katika kupambana na sumu mwilini.
Hivyo basi ni muhimu kuongeza kiasi chako cha Vitamin C kwa angalau kuanzia Mg. 5000-20,000 kwa siku. Vilevile Vitamin E na A ni muhimu sana katika ku tibu athari zilizo sababishwa na uvutaji wa sigara kwenye seli na membranes zako.
Madini mengine muhimu ni coenzyme Q10. Madini haya ni muhimu sana katika kulinda mapafu na moyo huku yakiongeza Oygen kwenye ubongo wako.
Kwa msaada zaidi,tuandikie :
neemaherbalist@gmail.com AU Tupigie 0766538384
maelezo yako yamenipa matumaini nijukumu langu kuangalia nitafanikiwa kiasi gani shukuran
ReplyDeleteUnatumiaje mbegu za oti na zikoje!?
ReplyDeleteJe una bidhaa hizi ambazo umezitaja hapa
ReplyDeletejamani nasumbuliwa na matatizo ya vidonda vya tumbo pia nimekuwa mwathirika wa matumizi ya ugoro naombeni ushauri na tiba pia
ReplyDelete