Skip to main content

HUU HAPA MWAROBAINI WA TATIZO LA FOLENI, JIJINI DAR ES SALAAM.






Usafiri wa raha mustarehe.
Tungependa kukukaribisha kwenye huduma yetu ya Usafiri jijini kwa kutumia mabasi maalumu kwa sababu kuu tatu au zaidi.

1. Tunaamini wafanyakazi wanaotumia muda mrefu njiani kwa kutafuta usafiri, au kwa kukwama kwenye foleni wakati wakielekea makazini, huwa wanafika wamechoka tayari na hivyo kupelekea kuwa na umakini wa kiwango cha chini pamoja na kupunguza uzalishaji.

2. Kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu wakati ukiendesha gari, inaaminika kuwa ni mazingira yanayosababisha kiwango cha juu sana cha msongo, na ni sababu ya watu wengi kutokuwa na furaha kwa muda mwingi wawapo makazini.

3.Gharama za kuendesha gari kwa siku moja kwenye jiji la Dar es Salaam, kwenda kazini na kurudi zinakisiwa kuwa zaidi ya Tsh. 30,000/= kwa gari ya kawaida yenye viti vitano. Hii inamaana kuwa kwa kila kiti kimoja cha gari lako, kinakugharimu Tsh. 6000/=. Endapo unatumia kiti kimoja tu cha gari lako, inamaanisha unapoteza Tsh. 24,000/= kwa kila siku unapotumia gari lako kwenda kazini, kwa siku 20 za kazi ni sawa na Tsh. 480,000/= na ni zaidi ya Tsh. 5,760,000/= kwa mwaka zinazopotea kwa wewe kuendelea kutumia gari lako binafsi kwenda kazini na kurudi.

Kampuni ya City Ridez Travels & Tours ingependa kukuletea suluhisho la matatizo haya kwa ujumla wake. Lengo letu ni kupunguza idadi ya magari binafsi yanayotembea muda wa kwenda na kurudi kazini kwa kukuletea usafiri maalumu, wenye starehe, wakutegemewa na kwa gharama nafuu.

Hapa City Ridez Travels & Tours tunahusika na usafiri maalumu wa mabasi, kwa minajili ya kutoa njia mbadala ya kusafiri ukiwa ndani jiji. Kimsingi tukizingatia zaidi kwenye Ubora, Uaminifu na Usalama.

Njia tunazotoa Huduma kwa sasa.

TEGETA - POSTA - TEGETA (kupitia MWENGE)
GONGO LA MBOTO - POSTA - GONGO LA MBOTO
MBEZI KIMARA - POSTA - MBEZI KIMARA
MBEZI AFRICANA - POSTA - MBEZI AFRICANA  (kupitia Mbezi chini)
MBAGALA - POSTA - MBAGALA
TABATA SEGEREA - POSTA - TABATA SEGEREA
MWENGE - POSTA - MWENGE ( Kupitia Sinza )


Njia zinazotazamiwa baadae
MBAGALA KIJICHI - POSTA - MBAGALA KIJICHI
KUNDUCHI - POSTA - KUNDUCHI

Njia nyingine zitaongezwa kwa kuzingatia upatikanaji wa wateja na mahitaji

Gharama / Bei
Bei zetu zinatazamiwa kuwa ni bei nafuu kwa kua kila mtu analipa kwa kile anachotumia peke yake. Tiketi zetu zinapatikana kwa Tsh. 5500/= kwenda na kurudi kwa siku kwa njia fupi, na Tsh. 11000/= kwenda na kurudi kwa njia ndefu. Pia unaweza kujipatia tiketi za kwenda peke yake au kurudi kwa Tsh. 3300/=. Na kwa wale ambao wangependa kujipatia tiketi za wiki nzima (yaani siku 5) au mwezi mzima (yaani siku 20) tiketi hizi zina unafuu wa aslimia 10%. Tiketi zinapatikana kwa mawakala wetu au kwa kutumia simu yako ya mkononi. Au piga simu +255 715 400 666.

Tiketi hizi zinamaanisha kuwa tutakuchukua kutoka karibu na nyumbani kwako kukuleta mjini asubuhi na kukurudisha jioni, na kama unakaa mbali na barabara kuu, tutakupatia sehemu salama ya kuegesha gari lako bila wasiwasi.

Muda.
Tunahakikisha unakua mjini kila siku asubuhi kabla ya mida ya saa 1:00 asubuhi, hivyo basi tutakua tukiondoka maeneo tofauti jijini kwa muda tofauti kulingana na umbali na miundo mbinu ya eneo husika, (kuanzia mida ya 11:00 asubuhi na 12:30 asubuhi) vilevile tunatoa safari ya 7:30 asubuhi kwa wale wanaopenda kuchelewa kuingia mjini. 

Kwa jioni magari yanaondoka kuanzia saa 11:00 jioni na 11:30, vile vile kuna magari ya 1:30 usiku kwa wale wanaochelewa au wafanyakazi wa mabenki. (Unaweza kuwasiliana na mtoa huduma wetu ili kuangalia upatikanaji wa safari kuendana na mahitaji yako. +255 715 400 666)

Tiketi
Tunatoa aina mpya ya tiketi zinazowekwa QR codes kwa ajili ya usalama, na unaweza kuzipata kwa mawakala wetu, au kwa kununua mwenyewe kupitia namba yetu ya simu +255 687 644452 na utatumiwa tiketi yako kwenye simu yako ya mkononi, au barua pepe au hata kupitia mitandao ya kijamii baada ya kukamilisha malipo, na utatakiwa kuonyesha tu QR codes uliyotumiwa kwa ajili ya uthibitisho. Ni rahisi kiasi hicho. 

Kumbuka hautaweza kulipia ukiwa ndani ya gari, na kuna idadi maalumu ya wateja watakaohudumiwa kwa siku, hivyo ni muhimu kama utaweka siti yako mapema kuepuka usumbufu.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea ofisi zetu zilizoko kwenye jengo la NSSF Hifadhi house gorofa ya Saba, karibu na mnara wa askari, au ukapiga simu namba. +255 222 114 308 Mobile: +255 712 823 505 au barua pepe: cityridezsales@gmail.com, au tembelea kuras wetu wa facebook:www.facebook.com/cityridez


Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA