Ukwaju
ni tunda ambalo wengi hulitizama kama dawa.Tunda hili linasifika kwa kusaidia
kutibu magojwa mbalimbali hii husababishwa na wingi wa virutubisho
vinavyopatikana katika tunda hili,hasa madini mwili.
Juisi
ya ukwaju
Watu
wengi hawapendi juisi ya ukwaju kwasababu ya
uchachu mkali na ambavyo inajitenga kwenye glasi (maji huja juu na ukwaju
hubaki chini).Unaweza kutengeneza juisi hii na isiwe na uchachu
mkali,wala isijitenge kwenye glasi .Juisi huwa nzito na tamu.
Mahitaji
- Ukwaju robo kilo
- Parachichi moja
–ukubwa wa kati
- Maji kwa kiasi
upendacho
- Sukari kwa ladha
upendayo
Njia
1.loweka
ukwaju kwenye maji ,acha uloane kwa saa moja.Tumia mwiko au kijiko kizito
kuchanganya na kuponda ukwaju.chuja na weka pembeni.
- Ukipenda kutumia
mikono,hakikisha umevaa glovzi za jikoni zakushikia vyakula ,si salama
kushika na mikono wazi (mara nyingi hutumika mara moja tu kisha unazitupa)
- Loweka ukwaju kama uliununua sokoni ukiwa na maganda
ukaumenya mwenyewe,kama umenunua ukwaju uliokwisha menywa,badala
yakuloweka hakikisha unachemsha ukwaju ukiwa na maji.Lengo ni kuuwa
vijidudu vinavyoweza leta magonjwa,kwani unakua umekaa wazi muda mrefu na
Hujui aliyeushika kama alikua na mikono safi.
2.Kata,menya
parachichi kisha saga na maji kiasi (tumia mashine yakusagia juisi).chuja
weka pembeni
- Usiweke
parachichi jingi sana,litakata ladha ya ukwaju,weka kiasi tu kwani lengo
la kuongeza parachichi ni ili kupunguza uchachu wa ukwaju na kuipa
juice uzito ili maji na ukwaju visitengane.
3.Katika
chombo kipana changanya juisi ya ukwaju na parachichi kwa pamoja,ongeza maji
adi upate uzito uupendao,ongeza sukari kwa kiasi upendacho kisha changanya adi
upate juisi nzuri.isiwe chachu sana,iwe nzito
kiasi na hakikisha umeweka sukari yakutosha.Chuja na Adi
hapa juisi tayari kwakunywa.
Ukipenda
weka frijini iwe baridi.juisi hii inafaa kwa watu warika zote na unaweza kunywa
wakati wowote.Kwa wagonjwa wa kisukari au wale ambao wanakwepa kunywa sukari
ili kupunguza uzito,unaweza kuweka asali badala ya sukari.
FAIDA ZA
JUISI YA UKWAJU
1.Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo
huzuia Saratani (cancer)
2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
3.Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
7.Husaidia kurahisisha choo (laxative)
8.Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
9.Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
10.Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

nina tatizo docter
ReplyDeletenina tatizo docter
ReplyDelete