Na Damas Makangale, MOblog kwa Msaada wa Mtandao
Mwanamke mmoja nchini Czech Republic ametolewa mawe
takribani sita katika tumbo lake baada ya kufanyiwa oparesheni kubwa ya
upasuaji na madaktari bingwa.
Madaktari wanasema alikuwa na hofu kubwa ya kuona
madaktari kwa sababu ni nusu kifo ilikuwa ni kufa au kupona.
Alikaa na tumbo hilo kwa miaka 47 na lilikuwa
likizidi kuvimba siku hadi siku ni mara 20 la tumbo la kawaida.
Wataalamu wanasema kwamba haijulikani kama atapata
nafuu ya haraka na moja kwa moja ila baada ya oparesheni uzito wake ulipungua
kwa kasi.
Mwanamke huyo raia wa Czesh alikuwa na takribani
mawe sita ambayo yalioonekana na kutolewa kutoka kwenye tumbo lake na ukubwa wa
tumbo ulikuwa mara ishirini la tumbo la kawaida.
Mwanamke huyo alifanyiwa oparesheni ya kuokoa
maisha yake katika hospitali ya mkoa wa Zlin mwezi uliopita.
Ilichukua upasuaji wa zaidi ya saa saba kuondoa
ukuaji ambao ni zaidi ya mita moja katika mduara wa kipimo cha kawaida.
Zdenek Adamik , mkuu wa Idara ya masuala ya uzazi
na magonjwa ya wanawake katika hospitali hiyo, alisema madaktari walikuwa
walishangazwa kwa nini mwanamke huyo akutafuta msaada wa matibabu mapema.
“Ni ajabu kwamba familia na marafiki wa karibu
hawakuweza kupeleka taarifa katika mamlaka za utabibu mapema au kuguswa na
matatizo ya mama huyo,” alisema mkuu huyo wa idara.
Chupa za Damu zilizotumika kumwogezea Damu mama
huyo wakati wa Oparesheni iliyodumu masaa saba.
CREDIT : MO DEWJI BLOG
Comments
Post a Comment