LadyJay Dee |
Malkia wa Muziki wa
Bongofleva, Mwanadada Judith Wambura
Habash , leo kupitia
ukurasa wa Facebook, amewataka mashabiki
wake na watanzania
kwa ujumla kuwa
makini na watu
wanao tumia jina
lake kujipatia fedha
kwa ulaghai kupitia mtandao wa Facebook.
Kwa mujibu wa Jide, watu
hao wamefungua ukurasa
(Page) kwenye mtandao wa
Facebook kwa kutumia
jina la LadyJay Dee
huku wakijinasibu kutoa
mikopo kwa watu
mbalimbali ambapo watu
wanao jitokeza kuomba
mikopo hutakiwa kutoa
kiasi fulani cha
pesa.
Jide ana funguka zaidi
kwa kusema :
“ Naskia hiyo page ya Jide wa
uongo imetengeneza mpaka tangazo la kwenye TV, humu mjini kuna mambo mengi
sana, watu wana njaa zao watafanya kila njia wapate pesa. “
HIKI
NDICHO ALICHO KIANDIKA
JIDE
Watu wanaendelea kuibiwa na wananilalamikia mimi, ndugu zangu
wapendwa kuweni makini sana, Mimi sina account yoyote inayotoa mikopo facebook...
Kuweni makini, kuweni makini. Narudia tena.
Nawashauri mwende CRDB Bank mkafungue account kama mnataka mikopo/ Bank ndio huwa zinatoa mikopo sio mimi.. Watu ni wezi sana wanatumia majina ya watu kujipatia pesa kwa ulaghai!!!!
Na nyie ndugu zangu mnaoibiwa, hivi tangu lini mikopo ikatolewa facebook???? Nilishaandika zaidi ya mara 3 kuwa sitoi mikopo mi natoa nyimbo na videos tuuu, lakini bado tu naendelea kupewa lawama kuwa nimewaibia watu, Jamaniiii eeeeeh!!
Naskia hiyo page ya Jide wa uongo imetengeneza mpaka tangazo la kwenye TV, humu mjini kuna mambo mengi sana, watu wana njaa zao watafanya kila njia wapate pesa.
Akili kichwani mwako.

Comments
Post a Comment