Skip to main content

AJIFUNGUA KWA MARA YA KWANZA AKIWA NA UMRI WA MIAKA HAMSINI NA SABA ( 57 ! )







Habari  hii  inaweza  kuwatia  nguvu  na  kuwapa  moyo  wanawake  wanaokabiliwa  na  changamoto  za  masuala  ya  uzazi  kama  vile  kutoshika  ujauzito huku  umri ukiwa  umeenda  na  ama  tatizo  la  kuchoropoka  kwa  ujauzito  mara  kwa  mara.




Mwanamke  mmoja  mwenye  umri  wa  miaka  57 (HAMSINI NA SABA  )  huko  nchini  Nigeria  amejifungua  watoto  mapacha , ukiwa  uzao  wake  wa  kwanza  toka  azaliwe.






Katika  ushuhuda  alio  utoa mbele  ya  kanisa  la   Pastor Tunde Bakare, the Overseer of The Latter Rain Assembly Church  jijini  Lagos  ambalo  linaongozwa  na  Pastor Tunde Bakare, mama  huyo  akiwa  ameambatana  na  mumewe  Mr. Dada, ameshuhudia  kuwa, yeye  na  mume  wake  walifunga  ndoa  mwaka  1993  wakati  huo  akiwa  na  umri  wa  miaka  32, na  kwa  kipindi  chote  hicho  cha  ndoa  yao, hawakufanikiwa  kupata  mtoto.





Familia  ya  Mr. & Mrs  Dada  walitumia  fursa  hiyo  kutoa  shukrani  zao kwa  Mwenyezi  Mungu  kwa  kuwabariki  mtoto.

Kutoshika  ujauzito  na  kuchoropoka  kwa  ujauzito  ni  matatizo  yanayo  toa   changamoto  kwa  wanawake  wengi  duniani.

Unaweza  kufahamu  namna  unavyo weza  kukabiliana  na  changamoto ya  kutoshika  ujauzito  kwa  kutembelea  link  hii  hapa  chini :


Na  kuhusu  tatizo  la  kuchoropoka  kwa  mimba, unaweza  kutembelea  link  hii  hapa  chini:

Comments