Skip to main content

MWALIMU AUWAWA KWA RISASI MBELE YA WANAFUNZI WAKE.

Marehemu  enzi za  uhai  wake
Mwalimu  mmoja  wa  shule  ya  Chekechea  huko  Mpumalanga, South  Africa  ameuwawa  na  mumewe  kwa  risasi  wakati  akijiandaa  kuingia  darasani.
Askari  wakiutoa  mwili  wa  marehemu  tayari kwa  kuupakia  kwenye  gari.

Tukio  hilo lilitokea siku  ya  Jumatatu  ya tarehe 15  AGOSTI  2017.

Imeripotiwa  kuwa, tukio  hilo  la  kinyama  dhidi  ya  mwalimu  huyo  aiyetajwa  kwa  jina  la  Kate Chiloane  mwenye  umri  wa  miaka  30, limetendwa  na  mwanaume  mwenye  umri  wa  miaka 40, ambaye  anadaiwa  kuwa  mume  wa  marehemu.
Inaripotiwa  zaidi  kuwa mtekelezaji  wa  mauaji  hayo  mara  baada  ya  tukio hilo  alienda  hadi  nyumbani  kwake  na  kujiua  kwa  risasi.


Tukio  hili  limeripotiwa  kuzua  mshtuko na  taharuki  kubwa  kwa  wanafunzi  pamoja  na  waalimu  katika  shule  aliyo kuwa  akifanya  kazi  marehemu.
Siku moja  kabla  ya  kuuwawa  kwake, marehemu  kupitia  ukurasa  wake  wa  facebook, aliweka  ujumbe  ulio  someka kama  ifuatavyo :

Accept your past without regret. Handle your present with confidence. And face your future without fear. “


Mpaka  sasa  bado  haijajulikana  bado  ni sababu  ipi  hasa  iliyo mfanya  muuaji  kufanya  mauaji  hayo, ingawa  watu  wengi  wanaamini  huenda  likawa  limesababishwa  na  wivu  wa  kimapenzi.

Comments