Padri Alois Magabe akiombea wanafunzi waliokumbwa na pepo katika shule ya msingi Robanda. |
Wakazi wa kijiji hicho wakiombewa |
Mmoja wa watoto akiletwa kwa boda boda akiwa amepoteza fahamu kwa ajili ya kuombewa |
Mchungaji Samson
Wahika wa Kanisa
la Zion lililopo wilaya ya
Serengeti mkoani Mara
amewaambia waandishi wa
gazeti la wananchi
kuwa chanzo cha kuanguka
na kupagawa mapepo,
wanafunzi wa Shule
ya Msingi Ikomba
Robanda iliyopo wilayani
Serengeti ni majini
yapatayo ELFU MOJA
NA MIA MOJA
yaliyotumwa shuleni hapo
na mtu aliyemtaja
kwa jina la
Makonga kutoka Arusha.
Gazeti la
Mwananchi toleo Na. 5010 la
Aprili 10, 2014 linamnukuu
Mchungaji wahika akisema
kuwa kufuatia maombi
anayo yafanya amebaini kuwa chanzo
cha kuanguka na
kupagawa kwa watoto
hao ni majini
ya Freemason kwa
sababu watoto hushikana
vidole na kuonyesha
ishara ya Freemason, huku yakidai
yametoka baharini na
hayataki wasome.
“ Katika
mapambano ya maombi, yanadai kuna
mtu anaitwa Makonga
kutoka Arusha, anaishi kitongoji
cha Buravanyota ndiye ameyatuma..yanadai yapo 300
chooni, 200 darasani na
600 kwenye mashamba
ya waalimu “ alisema
Mchungaji huyo.
Mchungaji Wahika
aliongeza kwa kusema
“ Mengine
yanataja wazee watatu
wa kitongoji cha
Machengere ndiyo wanahusika “
Alidai kuwa
chanzo ni ibada
za sanamu hasa kuabudu
Machaba ambao ni
mzimu wao kwa sababu
nao ni pepo.
Comments
Post a Comment