Skip to main content

Tunapotembea na sehemu za miili yetu zilizokufa....!




 .

Mzee mmoja, Salim Keni wa Makongorosi huko Chunya mkoani Mbeya, anasema kuwa siku moja alishangazwa sana na kauli ya mtoto wake wa miaka kumi. Anasema alikuwa amekaa nje ya nyumba yake jioni. Hapo alipokuwa amekaa alikuwa akiangalia jongoo. Jongoo huyo alikuwa ameumia sehemu yake ya nyuma, ambayo sasa ilikuwa imekauka, yaani imekufa.



Sehemu ya mbele ambayo ilikuwa ni nzima iliunganishwa na sehemu hiyo ya nyuma au ya mkia kwa kiuzi kidogo sana. Tunaweza kusema kwamba sehemu hiyo ya mkia ilikuwa inakokotwa na ile ya mbele. Hali hiyo ilimfanya jongoo yule kupata shida sana ya kusogea. Ukweli ni kwamba, hata kama sehemu ile ya nyuma ya jongoo yule ingeondolewa wala asingebaini, kwani ilikuwa sio sehemu ya mwili wake tena-ilishapoteza uhai.

Lakini aliendelea kuikokota kama vile bado alikuwa akiihitaji. Wakati Mzee Salim akimshangaa jongoo yule, mtoto wake huyo ambaye ni mtundu sana alifika hapo, ambapo naye alimuona jongoo huyo. Alikaa chini karibu na baba yake na kumkodolea macho kabla hajatoa kauli hiyo ya kushangaza. ‘Sasa baba, huyu mdudu si anapata shida bure, kwa nini asiache hii sehemu ya nyuma ili atembee vizuri, kwa sababu yenyewe imekauka…..’

Kabla baba yake hajajibu, mtoto yule alichukua kijiti na kutenganisha sehemu ya mbele na ile ya nyuma ya jongoo yule. Baada ya kufanya hivyo, jongoo yule aliweza kuongeza kasi ya kutembea na alionekana wazi kwamba amekuwa huru.

Mzee Salim alishikwa na butwa kwani hakuwa amepata muda wa kufikiri hivyo wakati akimtazama yule jongoo. Ni kweli kabisa, mtoto wake alikuwa amemfunulia kitendawili kikubwa sana cha maisha. Ya nini kutembea na sehemu ya mwili ambayo haina kazi, ambayo imekufa, ambayo angeweza kuiacha na kuwa huru zaidi?

Mtoto yule aliona wazi kabisa pamoja na akili yake ya kitoto kwamba, kama mdudu yule angemudu kuiacha sehemu ya mwili wake ambayo ilikuwa tayari imekufa angeweza kuishi katika uhalisia.

Uvumbuzi wa mtoto yule ni uzumbuzi wetu sote. Ni lini nasi tutaamua kuacha sehemu zetu ambazo zimekufa ili tuweze kuishi katika uhalisia? Sehemu zetu za miili zilizokufa ni zipi? Ni maumivu ya kimaisha yaliyopita. Ni mizigo ya mashtaka ya dhamira zetu na haja yetu ya kutaka kulipiza visasi. Ni masikitiko na majuto ya mambo yaliyopita, ambayo bado yanatuumiza hadi leo, mambo ambayo hayana maana yoyote tena kwetu.

Wengi wetu tunatembea au kuishi na mizigo mizito sana ya mambo yaliyopita, mambo ambayo ukweli ni kwamba hayana maana yoyote kwetu. Lakini kwa sababu tumeamua kutembea nayo, hutuzuia kwenda kama tunavyotaka, hutuzuia kufurahia maisha na hutuzuia kuwa huru katika mambo yetu mengi kimaisha.

Bila shaka tukiwa jasiri kama mtoto yule na kubaini sisi wenyewe kwamba tunatembea na sehemu zetu ambazo zimekufa, tutakuwa tayari kuziondoa na kuwa huru. Ni vizuri kujiuliza kama kuna mambo yaliyopita ambayo yanatuzuia katika kufanya na kufikia malengo yetu, ambayo yanatunyima furaha na kutufanya tujione kama watumwa. Je mambo hayo yana maana gani kwetu wakati yameshapita? Ni wazi yamekua, tunayabeba bure.

Kuna ambao wanalia hadi leo kufuatia vifo vya wapenzi wao vilivyotokea mika kumi iliyopita. Kuna wanaohangaika kutaka kulipa visasi vya yale mabaya waliyotendewa miaka kadhaa nyuma. Kuna wale ambao wanasumbuliwa na mawazo ya jinsi walivyofilisika au kusalitiwa na jamaa au wapenzi wao. Hii yote ni mizigo ya bure, ni sehemu za miili au maisha yao ambazo zimekufa, lakini wanaziburuza.

Nimekuwa nikiandika hapa mara kwa mara kwamba mambo yaliyopita hayapaswi kutuumiza, kutuondolea furaha na kutufanya tujihisi wanyonge na tusio na thamani, kwa sababu mambo haya hayana maana yoyote tena kwetu. Hata kama utafikiri kwa miaka mia kuhusu jambo fulani ambalo tayari limekutokea, huwezi kulibadili hata kwa chembe ndogo sana, sanasana unalipa uzito ili likutese zaidi.

Ili uishi hasa, uishi kwa kadiri ya utashi wa kanuni za kimaumbile, inakupasa uondoe sehemu ya mwili wako ambayo imeshakufa. Bila kuiondoa sehemu hiyo, ni lazima utaelemewa sana.

MAKALA  HAYA  YAMEANDIKWA  NA  MCHAMBUZI  KUPITIA   MTANDAO  WA  JAMII  FORUMS


Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA 

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka