HILI NDIO JAMBO ALILO LIFANYA MKAPA NA KUPELEKEA MWALIMU ( NYERERE ) AMUITE NYUMBANI KWAKE ( MSASANI ) HARAKA SANA!
Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. |
MKAPA NA KUITWA
MSASANI.
“
MWAKA 1965 nilikubali
ombi la uongozi
wa Shirika la
Utangazaji la Tanganyika
( TBC) kusoma taarifa
ya habari kwa
lugha ya kiingereza.
Siku moja baada
ya kusoma taarifa
ya saa moja
usiku, ilipigwa simu chumba
cha habari, ikiniagiza niende
mara moja Msasani
( nyumbani kwa Mwalimu
) kwani Rais
alitaka kuniona.
Rais Mstaafu Mh. Mzee Benjamin William Mkapa. |
Moyo ulidunda
lakini nilipo wasili Mwalimu
alinituliza akaniambia anataka
nikubali wadhifa wa
kuwa Mhariri Mtendaji
wa magazeti ya
chama ( TANU ) ya
Nationalist na Uhuru “
Maneno hayo
ni ya Rais
wa Awamu ya
Tatu, Mzee Benjamin William
Mkapa, na yamo katika
waraka wake wa
Desemba 2011 alioliandikia
gazeti la Uhuru
wakati likisherehekea miaka
50 tangu lianzishwe.
Mbali ya
kuongoza magazeti hayo, Mzee Mkapa alipata
pia kuwa Waziri
wa Habari na
pia Waziri wa Mambo ya
Nje. Ali iongoza Tanzania
kama Rais kuanzia
mwaka 1995 hadi
2005. Nyerere alimpigia
kampeni ya nguvu
mwaka 1995 ambapo
alipata ushindi wa
kishindo.
Inatoka kwenye
gazeti la Raia
Mwema, toleo Na. 346,
Jumatano Aprili 9, 2 014.
Comments
Post a Comment