.
Mtume na Nabii Nduminamfoo Munuo. |
HUKU akiwa na
matawi karibu nchi
nzima, na kanisa lake
likiwa linakua kwa
kasi, Mtume na Nabii
Nduminamfoo Munuo, wa kanisa
la Siloam ( Shika
Neno Tenda Neno ), ambaye awali
alianza kujiita Nabii
Eliya, hivi sasa amejiongezea
jina jingine akijiita
Mungu wa Majeshi.
Kwa mujibu wa
jarida liitwalo “
Neema Kubwa” lililotolea na
gazeti hili hivi
karibuni, Mtume na Nabii
Munuo pia anajiita
AD2, akidai yeye ndiye roho
ya Adamu wa
Pili, ambayo huleta uzima
kinyume na ya
Adamu wa kwanza
iliyoleta mauti.
Jengo kuu la ibada la kanisa
hilo liko maeneo
ya Makonde Mbezi
Beach.
Biblia katika 1 Wakorintho 15:45 inasema
“ Ndivyo ilivyo
andikwa, Mtu wa kwanza, Adamu
akawa nafsi iliyo
hain; Adamu wa mwisho ni
roho yenye kuhuisha “.
Mmoja wa waumini wake
anayesimamia jarida hilo, alisema
hakuna cha kushangaza
kwa nabii huyo
kuitwa Mungu wa
Majeshi kwa kuwa
ni jina alilolichagua
mwenyewe kwa ufunuo
maalumu.
Munuo, ambaye anaamini kuwa
huduma yake itaenea
dunia nzima, kwa vile
ndani yake ipo
roho ya Eliya, jina
linalo maanisha “ Mungu Mwokozi “
amewaaminisha wafuasi wake
kuwa siku moja dunia
nzima itaongozwa kidini
na yeye na
viongozi wengine wote
wa kidini watamwelewa
taratibu.
Baadhi ya mambo
tata ya kiimani
ambayo nabii Munuo
amewasadikisha maelfu ya
waumini wake ni
pamoja na kwamba
mafunuo yake ni
makamilifu na hairuhusiwi
kuyahoji wala kuyapima
na Biblia.
Sambamba na hilo, waumini hao ambao
pamoja na kiongozi
wao , wote huvaa mavazi
meupe wawapo ibadani
hawakubali kwa namna
yoyote kutumia Biblia
yenye jalada jeusi, na
badala yake huyachana
na kuweka ya
kwao meupe ambayo
ni rangi ya
nuru.
Ingawa waumini wa
Siloam wanaamini kwamba, mtu
anaweza kuandamwa na
mapepo kutokana na
sababu mbalimbali ikiwa
ni pamoja na
kuwa na majina
yenye mafungamano na mizimu, wanaamini kuwa
Shetani alifariki Novemba 4, mwaka
2008.
Kwa mujibu wa
mafundisho ya kanisa
hilo, Bustani ya Edeni
inayo tajwa katika
Biblia ilikuwa Tanzania, na
ndiko Adamu na mkewe
walikoishi ndiyo maana
kuna amani kuliko
mataifa mengi duniani.
Mmoja wa waumini
wake aliye bobea
katika mafundisho ya
kanisa hilo, ambaye pia ni
Mhariri, Bi. Scolastica Msewa, alimwambia mwandishi
wetu kuwa wanadamu
wote duniani asili
yao ni Tanzania, na
ndiyo maana mwanamke
wa Kiafrika anaweza
kuzaa mtoto wa
rangi yoyote duniani
wakati jamii za
weupe hawawezi kuzaa
mwafrika. “ Mungu
alikoanzia ni lazima
amalizie hapo hapo”’ alisema.
Waumini wa kanisa
hilo pia hutakiwa
kubadilisha majina yao
ya ukoo kwa
kuwa mengi ya
majina hayo yanabeba
laana.
Zaidi ya hapo
kwa mujibu wa
uchunguzi wa gazeti
hili, muumini huunganishwa katika
familia nyingine hapo
kanisani na hutengwa
na wazazi na
ndugu wa kimwili.
Wakati wa maombi
ni lazima muumini
ajiunganishe na madhabahu
kuu ya Nabii
Munuo ( Eliya
Mungu wa Majeshi
AD 2 ) ili yaweze
kusikilizwa.
Kituko kingine cha
wana Siloam, ni kwamba
wakati wanapo mwombea mgonjwa
mwenye mapepo au mizimu huyahamishia
hayo mapepo kwa
mmoja wao kisha
wanaanza kukemea na
huyo mmoja wao
baada ya kupagawa
hayo mapepo huongea
kupitia kwake.
CHANZO : Gazeti La
Nyakati, Toleo Na. 696, tarehe
30 Machi 2014.
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDelete