Skip to main content

LE MUTUZ KUFUNGUA KITUO CHA TELEVISHENI.



William  Malecela  a.k.a  Lemutuz  (Kulia )




Taarifa  zilizo  tufikia  kutoka  kwenye  chanzo  cha  kuaminika, zinaeleza  kuwa Mjasiriamali  na  Mwanahabari  maarufu  nchini  Tanzania  anayekwenda  kwa   jina  la  William  Malecela  almaarufu  kama  Lemutuz , yupo  mbioni  kufungua  kituo  cha   televisheni  huko  mkoani  Morogoro.








William  Malecela  anafungua  kituo  hicho  cha  televisheni  kitakacho  itwa  AFRICA  SWAHILI  TELEVISION  chini  ya  kampuni  inayoitwa  AFRICA  SWAHILI  MEDIA  LIMITED   yenye  share  holders  watatu  ambao  ni  kampuni  ya   Delina  General    Enterprises wenye hisa 59.8%, Davis Mosha mwenye hisa 39.9% na  William  John  Malecela  mwenyewe ambaye  ana  hisa 0.19% 

Akitoa  maelezo  kuhusu   kufungua  kituo  hicho  cha  televisheni, Lemutuz   kupitia  mtandao  wa  Jamii  Forums  alisema 


 “……..baada ya kukaa nje miaka 30 ingekuwa kichekesho kama ningerudi bila mambo kama haya, hisa zangu kwenye kampuni hii sio ndogo kiasi hicho lakini sio tatizo walisema Rostam ana hisa ndogo Voda so sio la ajabu, otheriwise mimi sio mwizi wala fisadi, nilitumia kazi ya kuendesha malori kujisomesha elimu kubwa na sasa niemrudi ninaitumia kadri niwezavyo kujisaidia mimi mwenyewe kimaisha na wengine pia,

- Kwa mfano toka nimerudi:

1. NIMEFUNGUA BLOG AMBAYO SASA NI NIMEISAJILI NI KAMPUNI KAMILI NA INAAJIRI VIJANA 2 NA NATEGEMEA MIEZI SITA IJAYO TUTAAJIRI VIJANA 10 NA TUTAKUWA KILA MKOA WA TANZANIA.

2. TUMEFUNGUA HII KAMPUNI YA TV NA RADIO, AMBAYO SOON VYOTE VITAKUWA HEWANI, TUTAAJIRI VIJANA WENGI SANA.

3. KWA SASA NIMJIKITA KWENYE MRADI WA ICD-MBAGALA PROJECT.

4. NAIFANYIA KAZI OFFER YA KUWA NA KIPINDI MAALUM KWENYE TV MOJA MAARUFU HAPA NCHINI.

- KWA KWELI NINAMSHUKURU SANA MUNGU KWA YOTE HAYA, NINGEBAKI USA NISINGEFIKIA HAYA MAFANIKIO NA KESHO NITAKUWA ARUSHA TENA AMBAKO PIA NINA PROJECTS ZINAENDELEA……”

Comments

Popular posts from this blog

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

FAIDA KUMI ZA MTI WA MKOMAMANGA

Mti   wa   Mkomamanga   ni   mti   wenye   faida   nyingi   sana   katika   afya   ya   mwanadamu. Mti   huu   una   virutubisho –afya     mbalimbali   ambavyo   ni   muhimu   katika   afya   ya   mwanadamu.   Virutubisho   hivyo   vinapatikana   kwenye   magome, majani, mbegu, maganda   ya   matunda, juisi   ya   matunda   pamoja   na kwenye   maua   ya   mti   wa   mkomamanga. Zifuatazo   ni   faida   muhimu   za   mti   wa   mkomamanga : 1.           Maganda   ya   tunda   la   mkomamanga   yakichemshwa    hutoa   juisi    ambayo   hutumika   kama   dawa   ya   kufunga   kuhara. 2.   ...