HILI NDIO TUKIO LILILO WAKUTA MH. Mama ANNE MAKINDA, Mama GETRUDE MONGELLAH NA Mh. Mzee PAUL KIMITI KWENYE MKESHA WA KUUKARIBISHA MWAKA 1984.
Hayati Edward Moringe Sokoine. |
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Anne Makinda. |
Mh. Mama Getrude Mongellah. |
Mzee Paul Kimiti ambaye ndiye mwandishi wa makala haya yaliyo nukuliwa kutoka kwenye gazeti la Raia Mwema toleo na. 346. |
DIRA YANGU,
EDWARD SOKOINE NA MKESHA
WA MWAKA 1984.
Na.
PAUL KIMITI
Aprili 12,
mwaka huu ni
kumbukumbu ya miaka
30 tangu atutoke
mpendwa na mchapakazi
wa karne hii, Hayati
Edward Moringe Sokoine, ambaye alikuwa
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Mimi ambaye
nilifanya naye kazi, nadiriki kusema
kuwa Hayati Sokoine
alikuwa nguzo na
tegemo kubwa la
Mwalimu Nyerere, aliamini kwamba
watanzania hawawezi kuishi
kaika ulimwengu wa
karne hii kwa
kuendelea kunyonywa na
wafanyabiashara wachache ambao
walikuwa wakishabikia ulanguzi
wa bidhaa adimu.
Alifanya kazi
zake kwa kuongozwa
na sera za
chama na kuzisimamia
kwa nguzo zote.
Aliamini kuwa
asiposimamia sera hizo, basi
itaonekan
“
Chama legelege kitazaa
sera legele “.
Kwa kuzingatia
hilo, alijitoa mhanga kupambana
na walanguzi, wala rushwa na
wazembe kazini kwa
nguvu zake zote.
Hakumuonea aibu
mtu yeyote, mkubwa na
mdogo wote waliadhibiwa.
Ni wakati huo ambapo
operesheni wahujumu uchumi
ilianzishwa.
Alitumia muda
wake mwingi kuhimiza
uadilifu wa watumishi
wa ngazi zote
serikalini, na kutoa onyo
kwa wazembe wote.
Alitutaka watumishi
wote wa ofisi
yake tukubali tuwe
watumishi waadilifu wa
umma.
Kila
dakika, kila siku na
kila mwezi ni
muda wa utendaji
kazi za wananchi.
Kwa utaratibu
huo huo, alikuwa wakati
Fulani kwa jambo
la dharura, aliweza kutuamsha
kwa madhumuni ya
kupata ufumbuzi wa
jambo la dharura
lilipotokea.
Hakusubiri asubuhi,
viongozi wahusika walikuwa
wanaitwa wakati huo
huo usiku na
walikuwa wakihudhuria maana
licha ya kumheshimu
walikuwa wanamuogopa, hakuwa na
utani kwenye kazi za
nchi.
Pamoja na
hayo, nilijifunza kuwa wakati
wa uhai wake
alikuwa akimtanguliza Mwenyezi
Mungu kwa kila
jambo.
Alituasa tuwe
watumishi wa mfano
na mawaziri wa
mfano kwa kutojilimbikizia mali
na kutojifanya sisi
ni bora kuliko
wananchi wengine.
Alifikia hatua siku moja
wakati wa mkesha
wa mwaka mpaya, mwaka
1984, kututaka mawaziri wake
wote watatu
( Katika Ofisi
ya Waziri Mkuu ),
Mh. Anna Makinda (
Spika wa sasa wa
Bunge la Jamhuri
), Mh. Getrude Mongella na
mimi, kwenda kanisani kwenye
mkesha wa Kanisa
la Mtakatifu Joseph
( Dar Es salaam )
na kututaka kusoma
masomo ya usiku
huo kwa zamu.
Kila wakati
alituonya kuwa “
Ya Mungu mpe
Mungu na ya
Kaisari mpe Kaisari “
. Yote hayo alifanya
ili tusijione kuwa
sisi ni bora
zaidi kuliko wengine
mbele ya Mwenyezi
Mungu.
Alitaka tuendelee
kuwa watumishi wa
watu na viongozi wanaojali shida
za watu .
Mimi niliye
fanya kazi naye kwa
karibu zaidi nakiri kuwa
kipindi chote nilichokuwa
chini ya uongozi
wake ulio tukuka, amenisaidia sana
katika maisha yangu
na utendaji kazi
katika nyadhifa mbalimbali
za uwaziri, mkuu wa
mkoa na mbunge.
Kuwepo hapa
leo katika Bunge
Maalumu la Katiba ni
mojawapo ya ya
misingi aliyo nifundisha
chini ya Baba
wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere.
Daima amekuwa
dira ya maisha
yangu na nguzo ya mafanikio
katika maisha. Nazidi kumuombea
kwa Mungu. Furaha ya
milele umpe ee
Bwana na mwanga
wa milele umwangazie
apumzike kwa amani.
Paul
Kimiti ni msomaji
wa gazeti na
ni mjumbe wa
Bunge la Katiba . Mwaka 1982
hadi 1984 alikuwa
Waziri katika Ofisi
ya Waziri Mkuu
chini ya uongozi
wa Waziri Mkuu,Edward
Sokoine .
Makala haya
yanatoka kwenye gazeti
la Raia Mwema, toleo
Na. 346, Jumatano Aprili 9, 2014.
Comments
Post a Comment