Skip to main content

TANGAZO MAALUMU LA KUUZA VIWANJA KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI







Halmashauri  ya  Manispaa  ya  Kinondoni  ina  viwanja    katika  eneo  la  Mabwepande  ikiwa  ni  mwendelezo  wa  mradi  wa  upimaji  viwanja  20,000  jijini  Dar  es  salaam. Halmashauri  inatarajia  kuuza  fomu  za  maombi  ya  kununua  viwanja  vipatavyo  1010  kwa  utaratibu  ufuatao.

i.             Fomu  za  maombi  kununua  kiwanja  zitaanza  kutolewa  tarehe  14/04/2014  hadi  tarehe  28/04/2014  katika  ofisi  za   Manispaa  Mwananyamala.
ii.           Mwombaji  atalipia  ada  ya  maombi  kiasi  cha  shilibgi  elfu  thelathini  tu ( Tshs  30,000/=)  ( Fedha  hizo  hazitarejeshwa )
iii.         Mwisho  wa  kurudisha  fomu  na  kuziwasilisha  zikiwa  zimebandikwa  picha  3  za  passport  size  ni  tarehe  06/05/2014.

iv.         Wakazi  wenye  nyumba  na  mashamba  ndani  ya  eneo  la  mradi  ambao  walitambuliwa  kabla  ya  zoezi  la  upimaji  kuanza, nao  wanatakiwa  kununua  fomu  za  maombi  kwa  utaratibu  ule  ule  ulio  ainishwa  hapo  juu.

v.           Waombaji  watakao  pendekezwa  kuuziwa  viwanja  watapaswa  kulipa  malipo  yote  ndani  ya  siku 14  baada  ya  kukabidhiwa  Ankara  za  malipo, baada  ya  muda  huo  maombi  hayatashughulikiwa  na  kiwanja  kitatolewa  kwa  mwombaji  mwingine.

vi.         Ukubwa  wa  viwanja


UJAZO  WA JUU ( HD )
UJAZO  WA  KATI ( MD )
UJAZO WA CHINI ( LD )
400 sqm -600sqm
600sqm-1200sqm
1201sqm-2500sqm

JEDWALI   LA  UFAFANUZI   WA  GHARAMA.
S/N
Aina  Ya  Matumizi
Kiasi Tshs/mita za mraba
1.
Makazi
10,000/=
2.
Makazi  na Biashara
15,000/=
3.
Biashara
25,000/=
4.
Huduma  za  Jamii
10,000/=
5.
Ibada/Kuabudia
10,000/=
6.
Viwanja  vyenye  nyumba  ( kwa  wenye  nyumba  walio  tambuliwa  kabla  ya  upimaji   )
5,000/=
7.
Petrol  Station
MNADA
8.

Viwanda  vidogo
( servive  trade  )
30,000/=

Imetolewa  na  MKURUGENZI  MANISPAA  KINONDONI.

Comments