Gharama za
sherehe ya harusi
ni jambo linalo
waumiza maharusi wengi
wanao tarajia kufunga
ndoa .
Hata hivyo,
maharusi na familia za
maharusi wakiamua kiweka
mambo ya kuonyesha
ufahari pembeni, wanaweza
kufanya sherehe ya
harusi kwa gharama
ndogo sana.
So
far mpaka sasa, harusi
iliyo ripotiwa kufanyika
kwa gharama ndogo
kuliko zote nchini
Tanzania ni iliyo
fungwa na wanandoa
Bw. Charles Kanyema
( 29 ) na Bi. Honoratha Paschal
( 28 ).
Sherehe ya ndoa hiyo
iliyofungwa katika Parokia
ya Morogoro mjini, mnamo
mwezi Juni mwaka
2013 iligharimu kiasi
cha Shilingi Elfu
Arobaini na Tano
tu za n kitanzania (
Tshs.45,000/=). Kwa habari
zaidi kuhusu wanandoa
hawa unaweza kutembelea
link hii hapa chini; http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/waenda-kufunga-ndoa-kwa-bodaboda-warudi-kwa-miguu
Katika mada
iliyo jadiliwa kwenye
mtandao mmoja wa
kijamii nchini kuhusu
gharama za kufanya
harusi kwa bei
nafuu, maoni mbalimbali yalitolewa
na watu mbalimbali.
Yafuatayo ni
baadhi ya maoni
hayo, na ambayo naamini
yanaweza kuwa msaada
kwa maharusi wanao
jiandaa kufunga ndoa
hivi karibuni.
Shilingi Milioni
Tano, inatosha kufanya harusi kubwa sana ya watu 120 hadi 150. Kuna
harusi ilifanyika 22.02.2014 jamaa walitumia 9.2million harusi ya watu around
300 ilikua bomba balaa. tulikunywa na kula nyama mwanzo mwisho na kamati yao
ikatoa zawadi fedha taslim 1.270m kama zawadi. Mimi mwenyewe nilikua impressed sana
maana nategemea kufunga ndoa mwaka huu na niliambiwa ukionanan na wenye ukumbi
wanaweza kukupangia kila kitu. Ukumbi wenyewe Princess hall Sinza.
Mtoa maoni
mwingine alisema :
Katika
harusi yangu nilifanya hivi, nilifanya 201O ilikua hivi
1.Budget haikuzidi milioni 4, nyingi zilienda kwenye chakula
2.Sikutoa kadi hata moja ya mchango
2. niliamua iwe casual, kwa hiyo sikuhangaika kutauta profesional MCs, badala ya kuchangisha afu kumlipa MC, tulitengeneza ratiba kisha marafiki zangu wachache, wakasaidia kusema chochote kwa kupokezana.
3. Badala ya kuchanga pesa kukodi magari, tulitumia magari ya friends, niliomba rafiki zangu wengine wachukue maids, mwingine bibi harusi, mwingine mama mkwe..kwa gari zetu hizi hizi za kawaida.
1.Budget haikuzidi milioni 4, nyingi zilienda kwenye chakula
2.Sikutoa kadi hata moja ya mchango
2. niliamua iwe casual, kwa hiyo sikuhangaika kutauta profesional MCs, badala ya kuchangisha afu kumlipa MC, tulitengeneza ratiba kisha marafiki zangu wachache, wakasaidia kusema chochote kwa kupokezana.
3. Badala ya kuchanga pesa kukodi magari, tulitumia magari ya friends, niliomba rafiki zangu wengine wachukue maids, mwingine bibi harusi, mwingine mama mkwe..kwa gari zetu hizi hizi za kawaida.
Mtoa maoni
mwingine aliingia ndani
zaidi na kutoa
mchanganuo wa gharama
za sherehe ya
harusi. Alitoa mawazo
yafuatayo :
1.Ukumbi=1,000,000
2.Mapambo=1,000,000
3.Vinywaji bia 3@=330,000
4.Chakula plate 12000=600,000
5.Mc & Music=600,000
6.Magari-
Wazazi pande zote mbili=300,000
7.Gari-Maharusi=400,000
8.Coaster(Waalikwa)=
150,000.
Daaah nlisahau hela ya keki, sasa tusiivuruge hela ya dharura; twende tuvunje pale kwenye gari ya Maharusi, chanja 200,000 hapo afu tuitupie kwenye cake, ibaki 200,000 Gari safi na simple
Jumla kuu =4,380,000
Balance=620,000(Dharura)
2.Mapambo=1,000,000
3.Vinywaji bia 3@=330,000
4.Chakula plate 12000=600,000
5.Mc & Music=600,000
6.Magari-
Wazazi pande zote mbili=300,000
7.Gari-Maharusi=400,000
8.Coaster(Waalikwa)=
150,000.
Daaah nlisahau hela ya keki, sasa tusiivuruge hela ya dharura; twende tuvunje pale kwenye gari ya Maharusi, chanja 200,000 hapo afu tuitupie kwenye cake, ibaki 200,000 Gari safi na simple
Jumla kuu =4,380,000
Balance=620,000(Dharura)
Mtoa
maoni mwingine alitoa
mchanganuo wa harusi
yake, ambayo aliifanya kwa
gharama ya kawaida.
Natoa mchanganuo wa harusi tuliyofanya
sisi. Ukumbi 600,000 unawekewa viti vya plastics na kupambiwa (750,000 unapata
executive chairs) sisi tuliweka viti vya plastics (600,000) mapambo tulipamba
simple standard kwa (600,000), usafiri wakwe tuliwapa hela 150,000 watafute
usafiri wao wenyewe maharusi 300,000 wazazi 130,000, keki ndafu moja 200,000,
Champaign 6 (72,000), MC na music 500,000, Picha 750,000, chakula cha watu 160
(ng'ombe mkubwa 560,00, kuku 20 kwa 100,000, kuchoma nyama kupika wali mweupe
na pilau na ndizi za kuchemsha 780,000) vinywaji (1,934,00) jumla ilikua
6,800,000
Na mwingine, akaelezea kuhusu
bajeti ya wedding reception yake
kama ifuatavyo :
Budget ya my wedding reception was
around 2million, it was a simple one ilifanyika nemax royal hotel, kinondoni. Waalikwa
walikuwa 60. Kulikuwa hakuna kamati wala sikumchangisha mtu hata senti
Mgawanyo wa budget:
1. chakula 20,000@plate X 60=1.2m
2.vinywaji 3 beers/person @ 2500X60=450000
3.mapambo bi harusi=100,000
4.gari ya wakwe=60,000(from a good friend).
5.cake=100,000
6. still pictures=150,000
7. champaignes(non alcoholic)2@9000=18000
Total 2.078m.
note; mc alikuwa one of my sisters, mziki pale ukumbini kulikuwa na speakers, so tulikuja na laptop yetu my bro akawa dj. Pia hatukulipia gharama za ukumbi maana tulielewana na wenye ukumbi coz vinywaji na chakula tulichukua pale pale. Pia hatukuwa na gharama za kupamba ukumbi;ila walituwekea nice chairs and tables zilizopambwa na vitambaa gari tuliyotumia maharusi ilikuwa a friend's car
Ni matumaini yangu kuwa, makala yatawasaidia maharusi ambao wanajiandaa kufunga ndoa hivi karibuni na wanafikiria kufanya sherehe ya harusi kwa gharama ndogo.
MUNGU
AWABARIKI SANA NA
NINAWATAKIA MAANDALIZI MEMA.
Comments
Post a Comment