Skip to main content

ARSENE WENGER AMTAKA DIMITAR BERBATOV



Arsene  Wenger.
 

Dimitar  Berbatov





ARSENE  WENGER  AMTAKA  DIMITAR  BERBATOV  ARSENAL.
KOCHA  wa  Arsenal, Arsene  Wenger  amemgeukia  mshambuliaji  wa  Fulham, Dimitar  Berbatov, kwa  ajili  ya  kuimarisha   safu  ya  ushambuliaji  ya  timu  yake  ambayo  inamtegemea  mshambuliaji  mmoja  tu, Olivier  Giroud.
Wenger  amekiri  kwamba  analazimika  kusajili  mshambuliaji  mpya  katika  dirisha  la   Januari  kwa  ajili  ya  kuongeza  matumaini  ya  Arsenal  kufanya  vizuri  katika  raundi  ya  pili  ya  Ligi  Kuu  England  pamoja  na  Ligi  ya  Mabingwa  Ulaya.
Hata  hivyo  kocha  huyo  Mfaransa  hataki  kutumia  pesa  nyingi  katika  dirisha  la  Januari  na  inadaiwa  kwamba  anamtaka  Berbatov  ambaye  staili  yake  ya  soka  inaendana  na  timu  yake  licha  ya  sasa  kutokuwa  katika  fomu.
Awali  Wenger  alipanga  kuwafukuzia  washambuliaji  Karim Benzema  na  Luis  Suraez, lakini  wote  hao  wawili  watapatikana  kwa  kiasi  kikubwa  cha  fedha  huku  Liverpool  ikionekana   haina  mpango  wa  kumuuza  staa  wao  kwa  timu  ya  Ligi  Kuu  England.
Msimu   huu  Berbatov, mwenye  umri  wa  miaka  32  amefunga  bao  tu  na  inadaiwa  kuwa  mwenyewe  anataka  kuondoka klabuni  hapo  katika  dirisha  la  Januari  na  klabu  hiyo  imepanga  kumruhusu  aondoke.
Wenger  anamtaka  mchezaji  huyo  akiamini  kuwa  anao  uwezo  wa  kufanikisha  azma  ya  klabu  yake  ya  kutwaa  ubingwa  wa  Ligi  Kuu  England  msimu  huu. Arsenal  inaonekana  kukaza  mwendo  katika  mbio  hizo.
CHANZO :  GAZETI  LA  MWANASPOTI, TOLEO  Na. 1440, Desemba  9, 2013.


Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...