Skip to main content

MADHARA YA KULA SUKARI





Sukari 
Wengi  wetu  tumeshasikia  ushauri  wa  kula  sukari kidogo,  ushauri  ambao  ni  mzuri  kiafya.

Lakini  licha  ya tahadhari  mbalimbali  zinazo  tolewa  na  wataalamu  wa  afya  kuhusu  madhara  yatokanayo  na  ulaji  mwingi  wa  sukari, bado  idadi  kubwa  ya  watu  hupenda  kutumia  sukari  kwa  wingi  kwa  njia  mbalimbali.

Utumiaji  wa  sukari  siyo  lazima  ile  sukari  nyeupe
( white )  au kahawia  ( brown )  pekee, bali  pia  hata  sukari  asilia  inayo patikana  kwenye  matunda, maziwa, asali, vinywaji baridi, pombe, baadhi  ya  nafaka  nakadhalika.

Hizo  zote  ni  aina  ya  sukari  ambazo  zinatofautiana  faida  na  madhara.

Wakati  viwanda  vya uzalishaji  sukari duniani  vinaongezela, tatizo  la  unene  kupita  kiasi  kwa  biandamu  nalo  linaendelea  kuongezeka.

Sukari  inahusika  kwa  kiasi  kikubwa  na  tatizo  la  kuongezeka  kwa  unene  wa  kupindukia  ( obesity).
Kwa  watu  wanene, ulaji wa  sukari  hata  kijiko  kimoja  tu  kwa  siku, huchangia  kwenye  tatizo.

Sukari  ni  ya  kuepukwa, siyo  tu  kwa  watu  wanene, bali  hata  kwa  watu  wengine  wenye  kujali  afya  zao.
Katika  kitabu  chake  kiitwacho  “ LICK THE  SUGAR HABIT ‘, Mwanalishe  Nancy  Appleton ( PhD), ameelezea  sababu  146  za  kwa  nini  sukari  hudhoofisha  afya  zetu.
Zifuatazo  ni  baadhi  ya  sababu  hizo  ;
i.                    Sukari  huweza  kuathiri  ukuaji  wa  homoni  mwilini  ( kitu  ambacho  ni  muhimu  kwa  kumfanya  mtu  kuishi  na  afya  njema  wakati  wote  )
ii.                  Sukari  ndiyo  chakula  cha  saratani  mwilini.
iii.               Sukari  huongeza  lehemu ( cholesterol )  mwilini.
iv.                Sukari  huweza  kusababisha  kizunguzungu  na  kudhoofisha  mwili  kwa  watoto.
v.                  Sukari  huweza  kudhoofisha  nguvu  ya  macho
vi.                Sukari  huweza  kuzuia  utembeaji  wa  protini  mwilini
vii.              Sukari  huweza  kusababisha  mzio  wa  chakula  (  Food  allergies )
viii.           Sukari   huchangia  ugonjw a wa  kisukari
ix.               Sukari  huweza  kusababisha  ugonjwa  wa  moyo.
x.                  Sukari  huweza  kuharibu, umbo la  vinasaba  vya  mwili  ( D.N.A )
xi.               Sukari  huweza  kusababisha utukutu, utundu  na  kukosa  umakini  kwa  watoto.
xii.             Sukari  huweza  kuchangia  kupunguza n kinga  ya  mwili  dhidi  ya  magonjwa  yatokanayo  na  wadudu  aina  ya  bacteria ( infectious  diseases )

Hizo  ni  baadhi  tu  ya  hizo  sababu  146. Je, kwa  kujua  sababu  zote  zilizo  thibitishwa  kuhusu  madhara  yatokanayo  na  sukari, kuna  sababu  gani  ya  kuendelea  kupenda  kutumia  sukari ?

Kitu  kizuri  pekee  kuhusu  sukari  ni  kwamba, kina  ladha  tamu na  tunapokula, tunajisikia  raha.  Hapa  ndipo  pahali  panahitajika  kuangaliwa  kwa umakini.

Kiasilia, mwanadamu  ana ladha  sita  tofauti  zikiwemo  za  uchungu, utamu, ukali,uchachu, na  ukakasi.

Hivyo  kuacha  kabisa  ulaji  wa  ladha  tamu, kunaweza  kusababisha   madhara  mengine  ya  kibaiolojia  na  ndiyo  maana  watu wengi  hushindwa  kujizuia  kutumia  sukari, hasa  kwa  watoto  ambao  kwao  huonekana  ni  jambo  lisilo  wezekana  kabisa  kuacha  kulamba  sukari.

Hata  hivyo, kuna  habari  njema  kuwa unaweza  kutumia  mbadala  wa  sukari  nna  kupata  ladha  ya  utamu  katika  vinywaji  au  vyakula  vyako  bila  kuwa  na  madhara.

Moja  ya  mbadala  wa  sukari  anaye  aminika  na  wengi  tangu  enzi na  enzi , ni  asali, ambayo unaweza  kuitumia  kwenye  vinywaji  mbalimbali  bila  kuwa  na  madhara.

Hata  hivyo, baadhi  ya  wataalamu  wanasema  kuwa asali  nayo  ina  ‘ fructose’ , huenda  ikawa  na  madhara  pia, ingawa  kwenye  vitabu  vya  dini  na  baadhi  ya  wanasayansi  wameilezea  asali  kama  kitu  kisicho na  madhara   mwilini  licha  ya  kuwa  nayo  ni  tamu  kama  sukari.
Sukari  ya  Stevia



Baadhi  ya   wanasayansi  wamependekeza  zaidi  mbadala  wa  sukari  kuwa  ni  “ Steviana  “ Xylitol”, ambavyo  vinatokana  na    mimea  na  majani, lakini  vina  ladha  ya  utamu  kuliko  hata  sukari.



Sukari  Ya  Xylitol

‘ Stevia’ na ‘Xylitol ‘  hutumika  zaidi  katika  nchi  za  Ulaya , Japan  na  Amerika  ya  Kusini, kwetu  Afrika  hazijulikani sana  na  sidhani  kama  zipo.

Jambo  la  msingi  ni  kujua  kwamba  sukari  tunaipenda, lakini  sio  chakula  kizuri  kama  tunavyo weza  kudhani, hivyo  tujitaidi  kuiepuka   kadri  tunavyo weza   kwa  kutumia  vyakula  mbadala  kama  asali, pale  tunaposhindwa  kabisa  kuiepuka, basi tutumie  kwa  uchache  sana.

CREDIT :  GAZETI  LA KISIWA, Toleo Na. 165, Desemba 6. 2013.

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA 

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka