Katika hali isiyo ya kawaida, watu wa mji wa Kaharisi nchini Uturuki wameshuhudia tukio la ajabu la kuzaliwa kitoto kichanga cha miezi saba baada ya mama yake kunyongwa.
Kwa mujibu wa
mtandao wa Intaneti wa Televisheni ya
Al Alam, toto huyo wa kiume amezaliwa
akiwa na afya nzuri.
Habari zaidi
zinasema kuwa, daktari wa gereza aliukimbilia
mwili wa Sabah Mosilibasa, mwenye umri wa miaka
28 baada ya kujifungua mtoto huyo, huku
akikata roho.
Aidha habari
zinasema kuwa, hadi mwanamke huyo anatiwa
kitanzi, hakuna aliyekuwa anajua kwamba alikuwa
na ujauzito wa miezi saba kutokana na
unene wa mwili wake, suala ambalo limezidi
kuwashangaza watu.
Sabah alihukumiwa
kifo baada ya kupatikana na hatia
ya kumuua kwa sumu mumewe na watoto
wake wawili na alisalia gerezani kwa muda
wa miezi mitatu akisubiri hukumu dhidi yake.
Duru za habari zinasema
kuwa, watu walishangaa baada ya kuwekwa
kamba ya kitanzi shingoni mwake na
kufyatuliwa kitanzi kama ishara ya
kumalizika adhabu hiyo, lakini Mosilibasa
aliendelea kutikisika miguu licha ya kwamba
adhabu hiyo ilikuwa imeshatekelezwa dhidi yake.
Muda mchache
baadaye alizaa mtoto wa kiume ambaye
awali alidhaniwa kuwa naye ameshakufa, lakini
baada ya kumsaidia pumzi mtoto huyo aliweza
kupumua na kisha kupiga kelele.
CREDIT : GAZETI LA
KISIWA, Toleo Na. 165, Desemba 6. 2013.
Comments
Post a Comment