Pichani mwanamke akiondolewa vinyweleo kwa nta ya asali/ |
JINSI YA KUONDOA VINYWELEO VYA MIGUUNI KWA WANAWAKE.
Kuwa na vinyweleo sio tatizo la kiafya.
Hata hivyo, linapo kuja suala la urembo, kuwa na vinyweleo vingi sehemu za miguuni ni jambo linalo weza kuwa kwaza wanawake wengi ingawa sio wote.
Nasema sio wote kwa sababu wapo wanawake ambao vinyweleo vya miguuni vinawafanya wawe na mvuto wa hali ya juu sana.
Katika kuthibitisha hilo, wapo wanaume wengi tu ambao wanavutiwa sana na wanawake wenye vinyweleo vya miguuni.
Hivyo basi suala la eidha vinyweleo vya miguuni huwafanya wanawake kuvutia ama kuto kuvutia ni suala la mtu na mtu.
Kama wewe ni mwanamke mwenye vinyweleo miguuni na unataka kuviondoa, ipo dawa nzuri ya asili inayo weza kukusaidia.
Dawa hii inajulikana kama “ NTA YA SUKARI “ au “ NTA YA KIAJEMI “ na ni maarufu sana katika nchi za Mashariki ya Kati.
Inaelezwa kuwa, aina hii ya urembo imeanza kutumika huko Uajemi ( Irani ) tangu enzi za kale.
Wataalamu wa masuala ya vipodozi katika nchi za Ulaya na Marekani wameithibitisha dawa hii kuwa effective kwa kiwango cha hali ya juu sana.
Vipodozi vingi vya kizungu vina madhara makubwa kuliko faida , kwa sababu vina kemikali mbaya kama vile toxins, hormone disruptors na hata pesticides ambavyo vyote kwa pamoja vina athari mbaya kwa afya ya mwanadamu.
Ndio maana unashauriwa kutumia njia hii ya asili ambayo haita hatarisha afya yako wala fedha zako kwani ni rahisi na yenye gharama nafuu. Kwa mujibu wa kitabu
“ Habiba’s Diary of the Middle Eastern Countries “ urembo huu wa nta ya asali unatumika zaidi katika nchi za Misri na Lebanon
Tazama hapa chini namna ya kutengeneza “ Nta Ya Asali “ ambayo hutumika kuondoa vinyweleo.
MAHITAJI :
i.
Sukari
nyeupe au ya
kahawia kikombe kimoja.
ii.
Maji
vijiko viwili vya
chakula.
iii.
Juisi ya
Limao kijiko kimoja na
nusu cha chakula.
iv.
Chumvi (
Optional ) kijiko
kimoja cha chai.
MATAYARISHO YAKE :
Changanya vitu vyote vilivyo orodheshwa hapo juu kwenye sufuria na upashe kwenye moto wa kiasi.
Acha mchanganyiko wako utokote pamoja hadi utakapo onyesha rangi ya kahawia.
Koroga mchanganyiko wako taratibu.
Hakikisha chembe chembe zote za sukari zinayeyuka.
Baada ya kama dakika nane hivi, mchanganyiko wako utabadilika na kuwa kama syrup.
Kuwa muangalifu, usiuache uungue, uipue mara utakapo kuwa na rangi ya kahawia nyeusi.
Ukisha onyesha rangi nyeusi, zima moto au ipua kwani nta yako itakuwa imekamilika. Iache kwa dakika kadhaa ili ipoe.
MATUMIZI :
Tumia kujipaka kwenye sehemu zenye nywele, mara mbili kwa siku asubuhi na jioni. Fanya hivyo mpaka nywele zitakapo koma kuota ama kutokea kwenye eneo husika.
MUHIMU : Unashauriwa kuiweka nta yako kwenye chombo cha plastiki na kuihifadhi kwenye friji. Na utakapo hitaji kuitumia tena, ichemshe kwa sekunde kumi tu kwenye jiko la gesi , jiko la mafuta au microwave.
KWA MSAADA WA MATIBABU YA MATATIZO MBALIMBALI YA KIAFYA KWA NJIA YA DAWA ZA MIMEA, FIKA NEEMA HERBALIST FOUNDATION. Tunapatikana katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa simu 0766538384.
asanteee, swal langu lasema hyo nta naitumia ikiwa yamoto au yabalid
ReplyDeleteThnx...
ReplyDeleteJe havioti tena ukifanya hivy?
ReplyDeleteAxant ila ukitumia havtajirudia tena?n je unatumia kwa mda gan?
ReplyDeleteNashukuru sana lakini vinyweleo vinaisha kabisa au vitaota tena??
ReplyDeleteAsante sanaaa kwa Elimu
ReplyDeleteAsali inafaa??badala ya sukari?
ReplyDeleteJamn mbona vimerud tena
ReplyDelete