Skip to main content

MWANAMKE MWENYE NDEVU AELEZEA CHANGAMOTO ANAZO KUTANA NAZO.



Queen Okafor
MWANAMKE  MWENYE  NDEVU  AELEZEA   CHANGAMOTO  ANAZO  KUTANA  NAZO.
Queen  Okafor ( 26 )  ni  mzaliwa  na  mwenyeji wa  jimbo  la  Anambra  nchini  Nigeria.  Mwanamke  huyu ni  mmojawapo  kati  ya  wanawake  wachache  duniani  wanao  kabiliwa  na  changamoto  ya  kuwa  na  ndevu  & garden love.   Akifanya  mahojiano  na   mtandao  mmoja  nchini  Nigeria, anasema  yeye  amerithi  hali  hii  kutoka  kwa  mama  yake  mzazi.  “  Nyumbani  kwetu  tumezaliwa  watano, wasichana  watatu  na  wavulana  wawili. Hali  ya w asichana  kuwa  na  ndevu  katika  familia  yetu  ni  jambo  la  kawaida “  Anasema   Queen.
Anaendela  kwa  kutaja  changamoto  anazo  kutana  nazo  kutokana  na  hali  yake  hiyo  ya  kimaumbile.


Queen  Okafor

Nakutana  na  changamoto  nyingi  sana. Miongoni  mwazo ni  pamoja  na  :
i.               Watu  kunishangaa  sana  kila  ninapokuwa  katika  maeneo  ya  public  kama  vile  kwenye  daladala  na  kwenye  matembezi  yangu  ya  kawaida.
ii.            Usumbufu  mkubwa  sana  kutoka  kwa  wasagaji  na  mashoga . Mashoga   huniona  kama  mwanaume  shoga. Nakumbuka  kuna  mwanaume  mmoja  anaye  jihusisha  na  mapenzi  ya  jinsia  moja  aliwahi  kunifuata  na kunipa  NAIRA  LAKI  TANO  ili  aniingilie  kinyume  na  maumbile. Hata  hivyo  nilimkatalia  kata  kata.



Kwa  upande  wa  wanawake  wasagaji, wao  wanasema  ninavutia  kama  mwanamke  na  kama  mwanaume, na  wamekuwa  wakinifuata  sana , wakiomba   nitoke  nao  kimapenzi  huku  ahadi  zao  zikiwa  ni  lukuki, lakini  hata  hivyo  nimekuwa  nikiwakatalia  kata  kata  kwa sababu  mimi  nimezaliwa  na  kuelelewa  katika   familia  yenye  maadili  ya  kikrsito.



iii.          Changamoto  nyingine  ambayo  ndio  kubwa  zaidi , ni  vitisho  kutoka  kwa  watu  wnao  jihusisha  na  kafara  (  RITUALISTS )  ambao  wamekuwa  wakiniwinda  kunitoa  kafara. Kuna  imani  potofu  ambayo  imejengeka  miongoni  mwa   watu  wanao  jihusisha  na  makafara  kwamba   kafara  ya  wanawake  wenye  ndevu  ina  nguvu sana. Jambo  hili  limekuwa  likinitia  hofu  sana  na  kunifanya  nishindwe  kutembea  kwa  uhuru  nikihofia  kukutana  na  watu  wa  namna  hiyo.



Hali  hii  ilinianza  nilipofikisha  miaka  21. Kusema kweli  sikuipenda  kabisa, hivyo  nikaanza  kutumia  dawa  mbalimbali  za  kizungu  na  za  kiasili  ili  kuondokana  na  tatizo  langu  lakini  wapi. Kuna watu  walinishauri  niwe  najifanyia  masaji  kwa   kinyesi  cha  chura, nikafanya  hivyo  sana  lakini  wapi, mwisho  wa  siku  nikaamua  kumuachia  Mungu  mwenyewe.



Queen  Okafor  anamalizia  kwa  kutoa  rai  kwa  NGOs  zinazo  jihusisha  na  masuala  ya  haki  za  wanawake, zianzishe  program  maalumu  za  kuwasaidia  wanawake  wenye   hali  ya  kimaumbile  kama  ya  kwake.

Vilevile  ametoa  wito  kwa watayarishaji wa  filamu  kutoka  Nollywood  kutengeneza  filamu  zinazo  elezea  changamoto  wanazo  kutana  nazo  wanawake  wenye   hali tofauti  za  kimaumbile  kama  yeye.



IMEKUSANYWA  KUTOKA  KWENYE  TOVUTI  MBALIMBALI   ZA  HABARI  NCHINI  NIGERIA.

Comments