Komamanga: Maganda Ya Mkomamanga yaliyosagwa, yakichanganywa na habbat sodah ya unga, hutengeneza dawa nzuri ya asili ya kuondoa tatizo la vipele vya usoni ( chunusi ) |
Kuna idadi kubwa ya watu wanao kabiliwa na tatizo la vipele vya usoni
( Chunusi ). Kuwa na chunusi ni jambo lenye karaha sana, kwani linakufanya upoteze mvuto wako wa asili na hivyo kukukosesha raha.
Zipo njia mbalimbali za asili zinazo weza kutumika kutibu tatizo la chunusi na vipele vya usoni.
Ifuatayo ni miongoni mwa njia bora kabisa na ya uhakika itakayo kusaidia kuondokana na tatizo la Chunusi au vipele kwenye uso.
Habbat Soda : Hii ni Habbat Sodah Ya Mbegumbegu. Habbat Sodah iliyosagwa ndio inayo hitajika katika kutengeneza dawa ya asili ya kuondoa tatizo la vipele vya usoni ama chunusi. |
MAHITAJI :
i.
Habbat Sawdah
ya Unga iliyo
sagwa.
ii.
Nusu
kikombe ya maganda
ya komamanga yaliyo
sagwa.
iii.
Nusu
kikombe ya siki
ya tofaha(apple )
MATAYARISHO NA MATUMIZI
Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu)
kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple).
Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila siku usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubarid.
NJIA HII IMETUMIWA NA WATU WENGI NA IMEWASAIDIA SANA. JARIBU NA WEWE KUTUMIA NJIA HII UONE MAFANIKIO YAKE.
Kwa habari na taarifa mbalimbali kuhusu masuala ya tiba zitokanazo na dawa za mimea na vyakula lishe, endelea kutembelea : www.neemaherbalist.blogspot.com Na Kwa Msaada Wa Matibabu Kwa Njia Ya Dawa Za Mimea, fika NEEMA HERBALIST FOUNDATION, kituo Cha Utafiti & Msaada Wa Matibabu Kwa Njia Ya Dawa Za Mimea na Vyakula – Lishe. Gharama za Huduma Zetu ni Nafuu Sana.
Comments
Post a Comment