Tatizo La Kutokwa na Kinyama Sehemu Ya Haja Kubwa : Chanzo, Athari Zake na Tiba Yake .
Tatizo la kutoka na kinyama ama uvimbe katika sehemu ya haja kubwa hujulikana kama Bawasiri.
Katika lugha ya kitaalamu ugonjwa huu hujulikana kama haemorrhoids ilihali katika lugha ya kiingereza, hujulikana kama Piles.
Tatizo hili husababishwa na kuvimba, kuharibika na kuondoshwa katika eneo lake kwa mishipa ya damu katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
Tatizo hili huwaathiri zaidi watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu asilimia 50 ya idadi ya watu wote wako hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 50.
Aina Za Bawasiri :
Kuna aina mbili za bawasiri
Bawasiri ya nje:
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo.
Mara nyingine, mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina ya bawasiri ambayo kitaalam inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
Bawasiri ya ndani:
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Hutokana na kuvimba na kuharibika kwa vimishipa vya aina ya artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
-Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
-Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
-Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
-Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Je, bawasiri husababishwa na nini?
Chanzo chake kikuu kitaalam hakijulikani, ingawa mambo yafuatayo yanaweza kusababisha au kukuweka katika hatari ya kupata bawasiri:
i.
Tatizo
sugu la kuharisha
ii.
Kupata kinyesi kigumu
iii.
Ujauzito
iv.
uzito
kupita kiasi (obesity)
v.
Mazoezi
ya kunyanyua vitu vizito
vi.
Kuingiliwa kinyume
na maumbile
vii.
Umri
mkubwa
viii.
Mambo
yanayoongeza shinikizo katika utumbo mpana
kama kukaa muda mrefu mahali pamoja
ix.
Matumizi
ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu kuliko vya kuchuchumaa na kujisaidia kwa mda
mrefu wakati wa haja.
Dalili za bawasiri
i.
Damu
kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
ii.
Maumivu
au usumbufu wakati wa kujisaidia
iii.
Kinyesi kuvuja
iv.
kijiuvimbe
katika eneo la tundu la haja kubwa
v.
Ngozi kuwasha
katika eneo la tundu la haja kubwa
vi.
Na
kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa.
Matatizo
yanayoweza kutokana na bawasiri:Upungufu wa damu mwilini (Anaemia) na bawasiri iliyojikaba (Strangulated haemorrhoids)
Kipimo cha kidole cha shahada kwa njia ya puru (Digital Rectal Examination), Kipimo cha njia ya haja kubwa cha kutazama moja kwa moja (Proctoscope) na Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
Matibabu yake
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri, pia tiba mara nyingi si ya upasuaji, mfano mgonjwa ataelekezwa kukalisha eneo la haja kubwa katika maji ya vuguvugu kwa mda fulani, ipo tiba rahisi iitwayo Rubber band ligation
Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, njia hii hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
Tiba Ya Asili Ya Bawasiri :
Unaweza kujaribu mwenyewe mojawapo kati ya tiba zifuatazo. Kila tiba inajitegemea hivyo unahsuariwa kuanza na tiba moja kwanza na uangalie matokeo yake kabla ya kuhamia na tiba nyingine,usitumie tiba zote kwa wakati mmoja.
i.
Tiba 1
: Kula kijiko
kimoja cha chakula
cha unga wa Habbat-Sawdaa pamoja
na glasi
moja ya maji
mara mbili kwa siku
kwa muda wa
siku kumi na
nne.
ii.
Tiba
2 : MAKAL-ARZAK
Chukua 100grm kwa kila lita moja na robo ya
Chukua 100grm kwa kila lita moja na robo ya
maji (1250ml).
Chemsha mpaka ibakie lita moja kamili.
Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha kahawa (50ml) kutwa mara tatu (1×3) mpaka dawa imalizike.
N:B : Mgonjwa asitumie nyama nyekundu aina yoyote,asile pili pili na wala asitumie vitu vikali.Badala yake atumie kwa wingi mboga za majani,matunda,maziwa na samaki.
iii.
TIBA 3 : Changanya
unga wa Habat soda na Asali safi ya nyuki vipimo vya sawa kwa sawa.Halafu
kunywa kijiko kimoja kimoja mara kwa mara.Fuatilishia na kumywa maji glasi moja
(250ml) kila umalizapo kunywa hiyo dawa.
iv.
Tiba 4 : Jipake mafuta
ya Nyonyo kwenye utupu wa nyuma ambapo
ndipo bawasiri hutokea.Fanya hivyo mara kwa mara, kwa sababu huirudisha hiyo
bawasiri ndani.
Mbarika hujulikana vile vile kwa majina ya mbono,nyonyo au “castor oil”.
Mbarika hujulikana vile vile kwa majina ya mbono,nyonyo au “castor oil”.
Comments
Post a Comment