Mwathirika wa Ugonjwa wa Manjano |
CHANZO, ATHARI , KINGA NA TIBA YA UGONJWA WA MANJANO.
Ugonjwa wa Manjano ambao hufahamika kitaalamu kama HEPATITIS B ni hatari sana na umesababisha vifo vya mamilioni ya watu duniani kote. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani ( W.H.O ) kuna zaidi ya wau Milioni 350 duniani ambao wameathiriwa na ugonjwa huu hatari kabisa na zaidi ya watu 620,000 hufa kila mwaka kwa ugonjwa wa Manjano.
CHANZO CHA UGONJWA WA MANJANO
Ugonjwa wa Manjano husababishwa na virusi viitwavyo “ Hepatitis B “ ( HBV ) ambavyo hushambulia zaidi ini la mwanadamu. Virusi hivi visipo tibiwa mapema hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha asratani ya ini ambayo hupelekea kifo.
MAMBO YASABABISHAYO MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA MANJANO.
Ugonjwa wa Manjano huambukizwa kwa njia zifuatazo :
i. Kujamiiana bila kutumia kinga.
ii. Kunyonyana ndimi
iii. Kuchangia damu isiyo salama
iv. Mama mjamzito mwenye ugonjwa huu anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa kujifungua.
v. Kuchangia vitu vyenye ncha kali kama vile wembe na sindano.
DALILI ZA UGONJWA WA MANJANO
Dalili za ugonjwa wa manjano huchukua muda mrefu kuonekana tangu maambukizi yatokee, na zinapo anza kuonekana wazi wazi, mgonjwa anakuwa amesha athirika kwa kiwango kikubwa sana. Dalili za ugonjwa huu ni kama ifuatavyo :
i. Uchovu wa mwili
ii. Kichefuchefu
iii. Mwili kuwa dhaifu
iv. Homa kali
v. Kupoteza hamu ya kula
vi. Kupungua uzito
vii. Kupatwa na maumivu makali ya tumbo upande wa ini.
viii. Kukojoa mkojo wa rangi nyeusi
ix. Macho na ngozi kuwa vya njano.
KINGA YA UGONJWA WA MANJANO
i. Kupatiwa chanjo ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu.
ii. Kutumia kinga wakati wa kujamiiana
iii. Kuacha kuchangia vitu vyenye ncha kali kama sindano, wembe n.k
iv. Kutochangia mswaki
v. Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
vi. Kuto ongezewa damu ambayo haijapimwa na kuthibitika kuwa salama.
TIBA YA UGONJWA WA MANJANO
Ugonjwa wa manjano hauna tiba isipokuwa mgonjwa akiwahi hospitali atapatiwa dawa za kupambana na virusi kuvipunguza nguvu za kupambana na ini., kupandikizwa ini ambapo ini lililoathirika huondolewa na kuwekwa jingine japo ni vigumu kupata ini salama.
Ukisha gundua kuwa umeambukizwa ugonjwa huu unashauriwa kuacha kutumia pombe, dawa za kulevya na vitu vingine vinavyo athiri utendaji kazi wa ini.
Comments
Post a Comment