Skip to main content

SHULE NZURI YA SEKONDARI KWA WASICHANA.



Gili ni shule ya wasichana ya bweni tu, shule imesajiliwa na wizara ya elimu kwa namba S.4375 iliyopo Kibaha Maili Moja B, kilometa mbili kutoka barabara ya Morogoro. Kama ukiendesha gari kutokea Dar es Salaam utapita Maili moja na TAMCO halafu utaingia kulia ukiifuata barabara inayokupeleka Bagamoyo kutokea Kibaha.
Shule inatoa elimu kulingana na mtaala wa elimu wa Tanzania. Shule ina nafasi za masomo kidato cha kwanza katika michepuo ya Sanaa, Sayansi na biashara.
Mtazamo
Kuwaandaa wanafunzi wajitegemee, wawe wabunifu na wachapakazi.
Mafanikio ya shule:
Shule ya 36 kati ya 365 kwa kanda ya mashariki katika mitihani ya Taifa FII. 2012,
Shule ya 3 kati ya 48 kwa kibaha katika mitihani ya mock FII. 2012
Gili Shule ya Wasichana ya Bweni - Kibaha
Mikakati yetu.
• Kuwaongoza wanafunzi katika maadili mema.
• Kuwaongoza wanafunzi katika kutambua umuhimu wao.
• Kuendeleza uwezo walionao wanafunzi wa kutambua fursa mbalimbali katika maisha.
• Kuwasaidia wanafunzi katika kutambua majukumu yao katika jamii.
• Kuwapa wanafunzi uwezo wa juu katika kuelimika.
• Kuandaa mazingira mazuri kwa wanafunzi kupata elimu.
Wafanyakazi
Waalimu wote wana shahada. Pia wapo walezi wa watoto (matron) na nesi (muuguzi), mpokea wageni (receptionist), wapishi na walinzi.
Huduma zilizopo
• Jengo la utawala, madarasa, bwalo la chakula, mabweni, maabara na jiko lenye huduma ya LPG.
• Mabomba ya maji ya dawasco na maji ya kisima hivyo hakuna tatizo la maji.
• Umeme wa Tanesco pia jenereta hivyo upatikanaji wa umeme ni wa uhakika.
• Uwanja wa michezo, basketball, netball na handball.
• Shule ina fensi.
• Tuna vifaa vya huduma ya kwanza.
• Maabara ya kompyuta
• Chakula bora
Mazingira
• Bustani asilia, mazingira mazuri ya kusomea na kwa malezi ya mtoto.
• Eneo wazi na tulivu lenye mzunguko mzuri wa hewa.
Jinsi ya kujiunga
Tunapokea wanafunzi kila Jumatatu hadi Ijumaa kwa ajili ya Interview (Usaili). Usaili unafanyika shuleni na Fomu zinatolewa hapa shuleni na Msimbazi Centre au kwenye tovuti yetu www.gilisecondary.ac.tz .
Kwa usaili na jinsi ya kufika shuleni wasiliana nasi kwa namba:-
+255 714 477216, +255 787 320522
Email: mugili2006ltd@yahoo.com
Facebook: GiliSecondarySchool
Twitter: Gilisecondary
www.gilisecondary.ac.tz
 PRE FORM ONE INAANZA 1 OKTOBA 2013 KARIBUNI


Comments