Skip to main content

MATUMIZI MBALIMBALI YA MAFUTA YA NAZI



 MATUMIZI  MBALIMBALI  YA  MAFUTA  YA  NAZI

1.   Mafuta  ya  nazi  kama  Make  Up Remover : Kama  umefanya  make  up na  unataka  kuondoa  unaweza  kufanya  hivyo  kwa  kutumia  mafuta  ya  nazi.  Chukua  pamba  chovya  kwenye  mafuta  ya  nazi  kasha  tumia  kusugua  kwenye  sehemu za  uso  ulizo   paka  make  up  yako.

2.    Kusafisha  uso  :   Paka  mafuta  ya  nazi  sehemu z a  shingoni  na  usoni  kisha  fanya  masaji halafu  jifute  kwa  kutumia  kitambaa  au  taulo.

3.    Kufanya  scrub  Ya  Mwili  Mzima  (  Body Scrub ) :   Chukua  vijiko  vitano  vikubwa  vya  sukari  kisha  changanya  na  vijiko  vitano  vikubwa  vya   mafuta  ya  nazi  kisha  koroga  mchanganyiko  wako  halafu  utumie  kufanyia  scrub

4.    Kufanya  Scrub  Ya  Usoni  (  Facial  Scrub ) : Changanya  mafuta  ya  nazi  na  amira au makande   pamoja  na  mdalasini  kasha  tumia  kufanya  scrub usoni .

5.   Kunyolea  ( Kushave ) :   Jipake  mafuta  ya  nazi  katika  sehemu  yenye  nywele  kisha  nyoa.

6.    Kujipaka : Unaweza  kutumia  mafuta  ya  nazi  kujipaka. Unaweza  kuongeza  na  marashi  ya  rose  ili  kuyafanya  mafuta  yawe  na  harufu  nzuri. Matumizi  ya  mafuta  ya  nazi  mwilini  huifanya  ngozi  yako  kuwa  na  afya  njema.

7.   Kuondoa  Makunyanzi :   Jipake  mafuta  ya  nazi   juu  ya  macho  ili  kuondoa  makunyanzi.

8.   Kuondoa  harufu  mbaya  ya  mwili : Matumizi  ya  mafuta  ya  nazi  husaidia  kuondoa  harufu  mbaya  ya  mwili. Tumia  kujipaka  mafuta  ya  nazi  mara  mbili  kwa  siku  asubuhi  na  jioni  na  baada  ya  wiki  tatu  au  nne, hautakuwa  tena  na  harufu  mbaya  ya  mwili. Ukiya changanya  pamoja  na  marashi  ya  waridi  utapata  matokeo  mazuri  zaidi.

9.   Kuogea ;  Changanya  mafuta  ya  nazi kwenye  maji  ya  oto  kisha  tumia  maji  hayo  kuogea.

10.                      Kutengeneza  sabuni  : Mafuta  ya  nazi  ni  moja  kati  ya  malighafi  muhimu  sana  katika  utengenezaji  wa  sabuni  za  aina  mbalimbali.

11.                     Kupigia  mswaki ;  Changanya  mafuta  ya   nazi  na  amira  ya  unga  kisha  tumia  kupigia  mswaki.

12.                      Kurutubisha  nywele : Mafuta  ya  nazi  yanajulikana  kama  “ Hair’s  Best  Friend ‘, unaweza  kurutubisha  nywele  zako  kwa  kutumia  mafuta  ya  nazi. Vile  vile  mafuta  ya  nazi  yanaweza  kutumika  kama  dawa  ya  kuulia  vijidudu  endapo  yatachanganywa  na   mafuta  mengine  ya  aina  tofauti  tofauti.

Comments

Popular posts from this blog

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

FAIDA KUMI ZA MTI WA MKOMAMANGA

Mti   wa   Mkomamanga   ni   mti   wenye   faida   nyingi   sana   katika   afya   ya   mwanadamu. Mti   huu   una   virutubisho –afya     mbalimbali   ambavyo   ni   muhimu   katika   afya   ya   mwanadamu.   Virutubisho   hivyo   vinapatikana   kwenye   magome, majani, mbegu, maganda   ya   matunda, juisi   ya   matunda   pamoja   na kwenye   maua   ya   mti   wa   mkomamanga. Zifuatazo   ni   faida   muhimu   za   mti   wa   mkomamanga : 1.           Maganda   ya   tunda   la   mkomamanga   yakichemshwa    hutoa   juisi    ambayo   hutumika   kama   dawa   ya   kufunga   kuhara. 2.   ...