Skip to main content

TOFAUTI KATI YA AKILI YA MWANAMUME NA MWANAMKE:



Zifuatazo ni baadhi ya tofauti kati ya akili ya mwanaume na mwanamke,tofauti ambazo kuzijua kwake kunaweza jaalia mafungamano yetu kuto kuwa na migongano mara kwa mara na tofauti baina yetu kupungua khususani kwa wanandoa.
1}Lugha:
Ni rahisi sana kwa mwanamke kujifunza lugha mpya kinyume na mwanamume,kwani ni vigumu kwake kujifunza lugha mpya.
Kutokana na hivyo mtoto wa kike kipindi cha utoto huwa ni mwelevu kulikoni mtoto wa kiume.

2}Kujishughulisha na jambo zaidi ya moja
kwa wakati mmoja:
Mwanamke anauwezo wa kutizama TV wakati huo huo akawa anazungumza katika simu au akawa anafanya moja ya kazi za nyumbani.
Hii ni kinyume na mwanamume,kwani yeye ubongo wake umepewa uwezo wa kufuatilia kitu kimoja tu,
hawezi kutizama TV wakati huo huo akawa anazungumza katika simu,utamuona anapunguza sauti ya redio au TV
wakati anapozungumza au anapoendesha gari.

3}Umahiri wa utatuzi na kutoa ufafanuzi:

Akili ya mwanamume inauwezo mkubwa na umahiri wa kutoa ufafanuzi au utatuzi wa tatizo.
Pindi atakapo letewa ramani au kupatwa na tatizo au kutakwa utatuzi juu ya tatizo fulani,utamuona ni mwepesi wa kufahamu na kutoa ufafanuzi na utatuzi wa tatizo hilo haraka.
Kinyume na mwanamke,
Utamuona ni mzito kiasi wa kukifahamu kile kilichopo katika ramani na kwa haraka haraka huenda kwake ikawa ni kiasi cha mistari tu.Vivyo hivyo upande wa matatizo mbali mbali yanayo mkabili.

4}Uendeshaji gari:

Mwanamume anauwezo wa kuendesha gari kwa kasi
na pindi anapokutana na kizuizi chochote au tatizo lolote barabarani,anauwezo wa kufikiri haraka na kukipita kizuizi hicho salama.
Ama upande wa mwanamke pindi akiwa katika mwendo wa kasi na akakubwa na kizuizi chochote au tatizo lolote humchukua muda katika kufikiri na kuto utatuzi wa jinsi gani atakikwepa kizuizi hicho.

5}Utatuzi wa matatizo:
Mwanamume pindi anapokubwa na matatizo,
akili yake moja kwa moja huyatenga matatizo hayo katika mafungu na kutoa utatuzi wa tatizo moja moja.
Kinyume na akili ya mwanamke,mara nyingi huwa haina uwezo huo, utakuta anarejea kwa watu wengine wampatie msaada dhidi ya tatizo hilo,
na daima humuhitaji mtu mwenye kumsikiliza,
na kiasi cha kumweleza tu tatizo lake yule anaye hisi anauwezo wa kumpatia utatuzi wa tatizo lake,
basi uzito wa tatizo lile kwake hupungua,sawa awe kapata utatuzi wa tatizo lile au hapana.

6}Uongo:
Mwanamume mara nyingi hufeli kumdanganya mwanamke iwapo kama atakuwa yupo mbele yake,
Kwani akili ya mwanamke inauwezo wa kugundua kiasi cha asilimia 70% ya alama za uso iwapo kama muhusika anasema kweli au anadanganya kutokana na harakati za mdomo na macho.
Na hii ni kinyume na mwanamume,kwani akili yake haijapewa uwezo huu wa kutambua kwa haraka,
kutokana na hivyo mwanamke anaweza mdanganya kiurahisi mwanamume nae yupo mbele yake.

7:Kudhibiti hisia
:
Mwanamke anazungumza sana,na pasina ya kufikiria.
Hali ya kuwa mwanamume hujitahidi kufikiria katika kila herufi anayo itoa,kutokana na hivyo mwanamume huwa si mzungumzaji sana kulikoni mwanamke.

Mwishoni twapenda kusema ya kuwa:
Mwanamume na mwanamke si vitu viwili vyenye kupingana bali kila mmoja anakamilisha upungufu wa mwenyewe,na haiwezekani mmoja wao kujitosheleza dhidi ya mwingine.



Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...