Huko uchina ya kale kulikuwa na msemo usemao “ Kama una mikate miwili, uza mmoja na pesa utakayo ipata itumie kununua Maua “. Hapa kwetu Tanzania, miaka ya tisini na kushuka chini kulikuwa na imani iliyo jengeka miongoni mwa watu wengi kuwa maua huwavuta malaika wazuri ama ni makazi ya malaika wazuri na huleta bahati nzuri. Tulikuwa tukiamini kuwa, wazungu hupendelea kupanda maua mazuri kwenye nyumba zao ili kuwavutia malaika wazuri kwa ajili ya kuzilinda nyumba zao dhidi ya mambo mbalimbali mabaya.
Bustani ya Gethsemane. Hapa ni mahali ambapo Yesu Kristu na wanafunzi wake kama vile Petro, Yakobo na Yohana walifika kwa ajili ya kufanya sala na maombi. |
Tukirudi kwenye maandiko matakatifu, ni maua ndiyo yanayo tajwa kuufunika utukufu wa Mfalme Suleiman.
" Lakini nawaambieni, hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote
hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.
Mathayo 6 : 29 "
Maua ni rafiki mzuri wa watoto. Tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa kuwalea na kuwakuza watoto katika mazingira yenye maua mazuri ni jambo zuri na lenye faida kubwa sana kwa afya ya makuzi ya mtoto kuliko kutoku fanya hivyo.
Vilevile watoto wanao soma katika shule zenye mazingira mazuri na yenye maua mazuri ya kupendeza, hufurahia zaidi masomo jambo linalo wafanya wawe na ari ya kujifunza vizuri na kufaulu vyema.
"
Maua ni rafiki mzuri wa watoto. Tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa kuwalea na kuwakuza watoto katika mazingira yenye maua mazuri ni jambo zuri na lenye faida kubwa sana kwa afya ya makuzi ya mtoto kuliko kutoku fanya hivyo.
Vilevile watoto wanao soma katika shule zenye mazingira mazuri na yenye maua mazuri ya kupendeza, hufurahia zaidi masomo jambo linalo wafanya wawe na ari ya kujifunza vizuri na kufaulu vyema.
Tafiti mbalimbali za kisayansi zinaeleza kuwa maua yana nguvu kubwa sana katika uponyaji wa akili na nafsi ( mind & soul ) ya mwanadamu. Kuna connection kubwa sana kati ya utulivu wa akili ya mwanadamu na maua. Katika maua, kuna nguvu kubwa sana na ya ajabu ambayo ina very sensitive connection na akili & nafsi ya mwanadamu. Hata Yesu Masiha na wanafunzi wake kama Petro, Yakobo na Yohana walikuwa walikuwa wakipendelea kwenda kufanya maombi kwenye bustani ya Gethsemane ambayo inatajwa kuwa na maua mazuri na yenye kupendeza.
Maua yakitumika vizuri yanaweza kuwa chachu kubwa sana katika maendeleo ya maisha ya mwanadamu kwa sababu yana ifanya akili na nafsi ya mwanadamu kuwa na utulivu mkubwa, na siku zote akili yenye utulivu mkubwa ndio inayo weza kufanya maamuzi makubwa na mazuri.
Kama nyumba yako ina nafasi ya kutosha, unashauriwa kupanda maua ya aina mbalimbali. Kuishi katika nyumba iliyo na bustani yenye maua mazuri kutaifanya nyumba yako kuwa sehemu nzuri, tulivu na yenye kuvutia sana, jambo litakalo kufanya uwe na utulivu wa akili na furaha isiyo mithilika pindi uwapo katika mazingira ya nyumbani kwako.
Inaelezwa kuwa, maua yana nguvu ya ajabu inayo weza kuwa tiba kwa watu wanao kabiliwa na matatizo mbalimbali ya kisaikolojia.
Kama hiyo haitoshi, maua yanaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kuhusu mambo mbalimbali kama vile mapenzi, furaha, huzuni nakadhalika..
Malkia Cleopatra wa Misri ya kale, alitumia maua kufikisha ujumbe wa mapenzi kwa waume zake.
Kupitia blogu hii, tutakuwa tunaweka aina mbalimbali za maua pamoja na mambo ambayo maua haya yanayawasilisha.
Kwa kuwa kuna maua ya aina nyingi sana. Haitakuwa rahisi kwetu kuyaweka yote kwa siku moja, hivyo basi tutakuwa tukiweka taarifa kuhusu maua kadhaa kila siku.
Rose Thornless = Love at First Sight.
|
Stephanotis = Happiness in Marriage, Desire to Travel, Good Luck
|
Tulip : Love, Symbol of the Perfect Lover
|
Violet = Modesty, Faithfulness, Simplicity
|
Bittersweet = The Truth : Maua haya yanamaanisha ukweli. Sababu inayo yafanya maua haya kuwakilisha ukweli ni kwa sababu ya ladha yake chungu. |
Frangipani = Shelter, Protection
|
Comments
Post a Comment