Matango |
4.0
MAGONJWA SUGU YASIYO YA KUAMBUKIZA
Magonjwa
makuu sita yasiyo ya kuambukiza ni pamoja na: Ugonjwa wa kisukari, Magonjwa ya
moyo, Shinikizo kubwa la damu, Saratani, Magonjwa ya figo na Magonjwa sugu ya
njia ya hewa.
Sababu
zinazopelekea kuwepo kwa magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza:
Mtindo
wa maisha usiofaa unapelekea mtu kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza,
mtindo huu wa maisha usiofaa unahusisha mambo yafuatayo: ulaji usiofaa;
kutofanya mazoezi ya mwili; matumizi ya sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku;
matumizi ya pombe; na msongo wa mawazo.
4.1
Ugonjwa wa Kisukari
Ugonjwa
wa kisukari ni hali inayotokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi
kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu inayotokana na kongosho linaposhindwa
kutengeneza kichocheo cha insulin, au insulin iliyopo katika damu kushindwa
kufanya kazi kwa ufanisi.
Kichocheo
cha insulin ndicho kinachotumika kudhibiti kiwango cha sukari katika damu.
Kichocheo hiki ni muhimu sana katika kufanya sukari iweze kutumika mwilini ili
kupata nishati lishe. 5
Ugonjwa wa kisukari unapompata mtu huwa ni
wa kudumu, hivyo anahitaji kufuata taratibu za matibabu na maelekezo
atakayopewa na mtoa huduma wa afya kwa maisha yake yote.
4.1.1
Aina za kisukari:
Kuna
aina kuu mbili za kisukari ambazo ni :
Kisukari
kinachotegemea insulin ( type 1 diabetes)
Kisukari kisichotegemea insulin ( type 2
diabetes)
Kuna
aina nyingine ya kisukari ambayo huweza kujitokeza wakati wa ujauzito
(Gestational diabetes.)
Kisukari
kinachotegemea insulin:
Huwapata
zaidi watoto na wenye umri chini ya miaka 35. Katika aina hii ya kisukari seli
za kongosho zinazotengeneza insulin huwa zimeharibika hivyo kusababisha ukosefu
au upungufu wa insulin mwilini.
Kisukari
kisichotegemea insulin
Huwapata
zaidi watu wenye umri kuanzia miaka 45 na kuendelea. Katika aina hii ya
kisukari insulin ya kutosha inaweza ikatengenezwa katika kongosho lakini
haifanyi kazi hivyo mwili kushindwa kutumia sukari kwa ufanisi.
Kisukari
cha mimba
Ni
aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi ya wanawake wakati wa ujauzito.Hali ya
ujauzito husababisha ongezeko la baadhi ya vichocheo Kama Progesterone,
Estrogen, na free Cortisol ambavyo huongeza kiwango cha sukari katika damu.
Wakati
huohuo kichocheo cha Human Placental Lactogen huzuia insulin kufanya kazi kwa
ufanisihivyo kusababisha kiwango cha insulin kuongezeka katika damu.
Mwili
unaposhindwa kutengeneza insulin ya kutosha kupambana na ongezeko la sukari
katika damu kisukari cha mimba hutokea. Mara nyingi hutokea mimba ikiwa na umri
wa miezi mitano au zaidi na kwa kawaida huishawiki sita baada ya mwanamke
kujifungua. 6
4.1.2. Viashiria hatarishi vya
kupata ugonjwa wa kisukari
Kisukari
kinachotegemea insulin
Kurithi
katika familia, Magonjwa ya kongosho (kama saratani au uambukizo) ambayo huweza
kuua seli za kichocheo kinachotengeneza insulin, kupewa maziwa mbadala (ya kopo
au ya wanyama) au kumnyonyesha mtoto kwa muda mfupi, Mtoto akizaliwa na uzito
mkubwa kupita kiasi, Unene au uzito mkubwa utotoni.
Kisukari
kisichotegemea insulin
Uzito
uliozidi au unene uliokithiri, Shinikizo kubwa la damu, Mtindo wa maisha
usiofaa hususani kutofanya mazoezi, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, na
uvutaji sigara na bidhaa za tumbaku, Kuwepo kwa historia ya kisukari katika
familia, Umri zaidi ya miaka 45.
Kisukari
cha mimba
Kuwepo
historia ya kuwa na kisukari katika familia, Kuwahi kujifungua mtoto mwenye
uzito mkubwa, Mimba kuharibika mara kwa mara, Historia ya kisukari cha mimba,
Mkojo kuwa na sukari mara kwa mara, Kuzaa mtoto mfu, Uzito au unene
uliokithiri, Shinikizo kubwa la damu la muda mrefu, Umri zaidi ya miaka 35
4.1.3.
Dalili za ugonjwa wa kisukari
Dalili
za ugonjwa wa kisukari ni pamoja na:Kukojoa mara kwa mara, Kuhisi kiu sana,
Kuhisi njaa sana, Kuhisi uchovu wa mwili na kukosa nguvu bila ya kufanya kazi
,Kupungua kwa uzito wa mwili na kuwa mdhaifu, Kutoona vizuri,Kuhisi kizungu
zungu ,Baadhi ya viungo vya mwili kama vidole vya mikona na miguu kufa ganzi .
4.1.4.
Ushauri wa ulaji Kwa mgonjwa wa kisukari
• Kula mlo kamili angalau mara tatu kwa
siku, haishauriwi kukaa na njaa kwa muda mrefu.
• Kudhibiti kiasi cha nishati- lishe katika
chakula, kiasi kinategemea mahitaji ya mtu binafsi.
•
Kuongeza ulaji wa vyakula venye makapi mlo kwa wingi, kiasi kikubwa cha nishati
lishe kitokane na vyakula venye makapi mlo kwa
7
wingi ambavyo huyeyushwa na kufyonzwa
mwilini taratibu na hivyo kasi ya kuongezeka kwa sukari katika damu hupungua.
• Kupunguza kiasi cha mafuta, epuka mafuta
yenye asili ya wanyama na punguza kiasi cha mafuta mengine.
• Epuka sukari na vyakula venye sukari
nyingi kama vile soda, keki, biskuti, pipi, na asali, asilimia 80 ya asali ni
sukari
• Epuka kunywa pombe, pia haishauriwi
kunywa pombe kali kwani huleta madhara kwenye ini, usinywe pombe kabla ya kula
chakula kwani huweza kusababisha damu sukatiti ( hypoglycemia
• Kula tunda katika kila mlo, ikiwezekana
usimenye tunda na zingatia usalama wa chakula.
• Kula mboga mboga kwa wingi katika kila
mlo, chagua mboga mboga ambazo hazina kabohaidreti kwa wingi mfano mboga za majani
, nyanya matango, na saladi.
• Kupunguza uzito kama umezidi au dhibiti
uzito wa mwili, ni vyema kuwa na uzito unaoshauriwa kulingana na urefu wake.
• Kupanga utaratibu wa kula chakula na
matumizi ya dawa, kwa mgonjwa wa kisukari anayetumia dawa ni muhimu kupanga
utaratibu maalumu wa kula na kumeza dawa ili kuzuia kupungua kwa sukari katika
damu.
•
Epuka kukaa kwa muda mrefu bila kula chakula.
Comments
Post a Comment