Mtu mwenye shinikizo kubwa la damu anashauriwa kuepuka matumizi ya chumvi. |
Shinikizo kubwa la damu
Shinikizo
kubwa la damu hutokea pale panapokuwa na ongezeko la nguvu ya msukumo wa damu
katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye viungo na
tishu mwilini.
Ukubwa
wa shinikizo kubwa la damu hutegemea wingi na nguvu ya msukumo wa damu kutoka
kwenye moyo na ukubwa wa mishipa inayopeleka damu mwilini.
Viwango vinavyoashiria shinikizo kubwa la damu mwilini
Blood
pressure machine (sphignomanometer) hutumika kupima shinikizo kubwa la
damu.Kipimo kinachochukuliwa kuwa ni kawaida ni 120/80 mmHg au chini yake. 8
Kiwango kinapokuwa 140/90 mmHg au zaidi hali
hiyo huwa ni shinikizo kubwa la damu.Ikumbukwe kuwa panaweza kuwepo tofauti
kati ya mtu na mtu.
Viashiria
hatarishi vya shinikizo kubwa la damu
Historia
ya shinikizo kubwa la damu katika familia, Umri wa zaidi ya miaka 40, Jinsi ya
kiume (huwapata wanaume zaidi kuliko wanawake),Uzito uliozidi kiasi, Msongo wa
mawazo, matatizo mengine ya kiafya mwilini kama magonjwa ya figo, matatizo ya
mishipa ya damu, magonjwa ya moyo, matatizo ya vichocheo mwilini, kisukari au
saratani.Matumizi ya baadhi ya dawa na Kutokufuata mtindo bora wa maisha.
Dalili za shinikizo kubwa la damu:
Kichwa
kuuma mara kwa mara hasa sehemu ya kisogo, Kizunguzungu, Kutokwa kwa damu
pumuani, Maumivu ya kifua, Moyo kwenda kasi wakati umepumzika, Kushindwa
kufanya mazoezi kwa kushindwa kupumua, Mapigo ya moyo kushuka wakati
umepumzika, na Uchovu wa mara kwa mara.
Ulaji unaoshauriwa kwa mtu mwenye shinikizo kubwa la damu:
• Kuepuka vyakula venye chumvi nyingi,
ikiwa ni pamoja na vile vilivyosindikwa kwa chumvi
• Kutumia viungo mbalimbali kuongeza ladha
ya chakula( vitunguu swaumu, tangawizi, mdarasini, )
• Kuepuka vyakula vyenye mafuta na sukari
nyingi
• Kula mlo kamili angalau mara tatu kwa
siku ukizingatia kula vyakula vya aina mbalimbali
• Kula matunda na mbogamboga kwa kiasi cha
kutosha katika kila mlo
•
Kutumia nafaka zisizokobolewa na vyakula vya jamii ya kunde kwa wingi.
Mbinu za kupunguza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu
• Kuepuka vyakula venye mafuta mengi,
sukari na chumvi nyingi
• Kuepuka mafuta yenye asili ya wanyama
•
Kuepuka vyakula vyenye lehemu kwa kiasi kikubwa
Comments
Post a Comment